Home » » MTANGAZA NIA UBUNGE LUDEWA AANGUKIA PUA NAFASI YA NEC ,ASEMA HATAKI TENA KUGOMBEA‏

MTANGAZA NIA UBUNGE LUDEWA AANGUKIA PUA NAFASI YA NEC ,ASEMA HATAKI TENA KUGOMBEA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
aliyeshindwa ujumbe wa NEC Ludewa Injinia Zephania Chaula  akiangana na mbunge  Deo  Filikunjombe baada ya  kushindwa katika nafasi  hiyo ,Chaula alikuwa ni mmoja wa wana CCM waliokuwa  wakitaka kuwania ubunge jimbo la Ludewa
Chaula akiagana na mshindi mzee Nkwera 
 Mkuu  wa wilaya ya  Ludewa Antonia Choya akimkabidhi  hati ya  shukrani mbunge wa Ludewa  Deo Filikunjombe (kushoto)




 Mjumbe  wa  mkutano huo Bw  Choya  akipiga  kura
 Wajumbe  wakishiriki  kupiga  kura
 

 Wajumbe  wakishiriki  kupiga kura
 Mgombe  Chaula  akishukuru kwa  kushindwa
 Injinia  Chaula  akimpongeza mshindi mzee Nkwera
Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe  akipiga  kura  kumchangua mjumbe wa NEC Ludewa
 
 Mkuu  wa  wilaya ya  Ludewa  Deo  Filikunjombe akikabidhiwa hati ya  shukrani ya kushiriki mbio  za Mwenge  toka kwa mkuu wa wilaya ya  Ludewa Antonia Choya ,hati  iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Njombe
Na MatukiodaimaBlog


MBIO  za  ubunge jimbo la  Ludewa  mkoani  Njombe zimeishia hewani  kwa mtangaza  nia wa  wanafasi  hiyo Injinia  Zephania  Chaula  baada ya  kuambilia  kura 11 pekee katika nafasi ya mjumbe  wa Halmashauri  kuu ( NEC) Taifa kutoka  wilaya ya Ludewa  aliyokuwa akiwania dhidi ya katibu msaidizi  wa mbunge wa  jimbo la Ludewa  Hilaly  Nkwera  aliyeibuka mshindi kwa  kupata  kura 138 kati ya  kura  zote halali 151 zilizopigwa .

Huku mgombea  huyo aliyeshindwa katika nafasi hiyo ya Ujumbe wa NEC Injinia Chaula  akiapa  kutogombea tena nafasi hiyo kwa madai kuwa ni mara ya pili sasa anashindwa  vibaya  katika  mchakato  wa  kuwania nafasi hiyo ambapo awali alishindwa mgombea  wa darasa  la  saba marehemu Elizabeth Haule .

Uchaguzi  huo  mdogo  wa  kuziba nafasi ya  mjumbe  wa  NEC  iliyoachwa  wazi na aliyekuwa  mjumbe wa nafasi hiyo Elizabeth Haule  aliyefariki  dunia mapema mwaka  huu ,ulifanyika  mwishoni mwa  wiki  hii kwa  kuwashirikisha  wagombea  hao  wawili kabla ya mgombea  mwingine ambae ni mbunge  wa  jimbo la Ludewa Deo  Filikunjombe  kuandika barua ya  kujitoa katika  kinyang'anyiro  hicho akiwapisha wagombea  hao  wachuane  kutokana na yeye  kudai  kuwa atachukua fomu ya kugombea tena  ubunge  wa  jimbo  hilo la Ludewa .

Akitangaza  matokeo  hayo ya  uchaguzi msimamizi  mkuu  wa uchaguzi huo  Lucas Nyanda  ambae ni katibu  wa  jumuiya  ya  wazizi wa CCM mkoa  wa Njombe  ,alisema  kuwa  jumla ya  wajumbe  waliopaswa  kushiriki katika  uchaguzi  huo ni 164 ila   wajumbe  halali  walioshiriki ni 151 na kati ya  wajumbe  hao kura 2  ziliharibika  huku Injinia Chaula akipata  kura 11 na mshindi wa nafasi hiyo Bw  Nkwera  akipata  kura 138

Awali  mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Bw  Filikunjombe  ambae alikuwa ni mmoja kati ya  wana CCM watatu  ambao majina  yao yalirejeshwa  kuwania nafasai hiyo alisema  kuwa analazimika  kujitoa katika  nafasi hiyo  ili  kupisha wanachama  hao wawili  ambao wamemzidi  umri  ili  kuweza  kupambana  na  yeye ataendelea  kuwa kuwatumikia  wananchi  wa Ludewa katika nafasi ya  ubunge pekee.

Akiwashukuru wajumbe kwa ushindi  huo  wa nafasi ya ujumbe wa NEC Bw  Nkwera ambae  kitaaluma ni mwalimu na pia amepata  kuwa mwenyekiti wa Halmashauri ya  wilaya ya Ludewa na mwenyekiti wa madiwani wa mkoa wa Njombe na Iringa  alisema kuwa amefurahishwa na imani  kubwa ambayo wana CCM wameionyesha  kwake  kwa  kumchagua  kuwa mwakilishi wao katika vikao  vya  kitaifa .

Bw  Nkwera  alisema wana CCM Ludewa waamini  kuwa nafasi hiyo hawajakosea  kumpa na kamwe  hatawaangusha kwani atahakikisha anawatumikia  vema katika vikao  vya  juu kwa kuanza na  safari ya  kumpata mgombea wa nafasi ya  Urais wa CCM ambae atakuwa ni chaguo la  wana CCM wote wa Ludewa .

Huku  Chaula mbali ya  kuwashukuru kwa  kura  11 alizopata bado  alisema  kuwa hatakuwa tayari  kuendelea  kugombea tena kwani yawezekana kabisa  Mungu hajapenda  yeye  kuwa  kiongozi wa kisiasa bali ametaka  aendelee  kuwa mtaalam .


“Nasema haya kutoka moyoni mimi ni mwanachama hai wa chama cha mapinduzi na nakipenda chama change hivyo naahidi sitagombea tena katika maisha yangu nafasi hii ya UNEC  kutokana na ukweli kuwa nahisi siasa inanikataa maana kila nikigombea nashindwa hivyo ngoja nifanye kazi nyingine pia nampongeza  sana mshindi Mzee  Nkwera katika utendaji wake ndani ya chama”,alisema Mhandisi Chaula.


  Wakati  huo  huo serikali  ya  mkoa  wa Njombe kupitia mkuu wa mkoa wa Njombe Dr  Rehema Nchimbi imempongeza kwa  kumpa hati ya shukrani  mbunge  wa  jimbo la Ludewa  Bw  Filikunjombe kwa  ushiriki  wake  mkubwa katika kufanikisha  mbio  za mwenge katika  mkoa  huo kwa kuwa mbunge  pekee  kushiriki  mbio  za mwenge na kuchangia vizuri .

Akikabidhi hadi  hiyo mbele ya  wajumbe wa mkutano wa Halmashauri  kuu , mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Anatory Choya aliweza kumtunuku hati hiyo ya  heshima mbunge wa jimbo la Ludewa  Filikunjombe kwa kushiriki kimamirifu katika mbio za mwenge wa Uhuru ndani ya mkoa wa Njombe.

Akitoa cheti hicho Bw.Choya alisema kuwa kutokana na ushiriki alioufanya mh.Filikunjombe katika mbio cha mwenge wa Uhuru mkuu wa mkoa wa Njombe na ofisi yake wameona wampatie cheti cha heshima Filikunjombe kwani ni mbunge pekee aliyeshiriki katika mbio hizo za Mwenge katika mkoa wa Njombe.

MWISHO 

© 2015 Microsoft Terms Privacy & cookies Developers English (United States)

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa