Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
|
kada wa CCM anayeomba kuteuliwa kugombea ubunge jimbo la Ludewa kepten mstaafu Jacob Mpangala ambae leo amezomewa mkutanoni na kuokolewa kichapwa baada ya kujinadi kwa kutumia lugha za matusi na uongo dhidi ya mbunge Deo Filikunjombe |
|
mbunge Filikunjombe akiwapungia mkoano wananchi wa mndindi baada ya kujinadi |
|
wananchi wa kata ya Ibumi wakiwa wametuliwa wakimsikiliza kwa makini mbunge Filikunjobe wakati akiomba kura zao |
|
Filikunjombe akisisitiza jambo wakati akiomba kura kwa wananchi wa Ibumi leo ,wananchi hao walivuruga mkutano huo baada ya mtia nia mmoja kupanda jukwaani na kutoa taarifa za uongo na matusi ya nguoni dhidi ya mbunge wao |
|
Filikunjombe akiwashukuru wananchi wa Ibumi kwa imani yao kwake |
|
mratibu wa zoezi la kuwanadi wagombea kwa wana ccm John kiowi akitangaza kuvunja mkutano huo baada ya kuibuka vurugu .
Na matukiodaima BLOG
KATIKA kile kinachoonyeshwa kuwa wananchi wa Ludewa kumkubali mbunge wa jimbo hilo Deo Filikunjombe kuendelea kuongoza jimbo hilo kwa awamu nyingine leo wana CCM na wananchi wa kata ya Ibumi wamemzomea mmoja kati ya watia nia ubunge wa jimbo hilo na kutaka kumchapa wakati wa mkutano wa watiania hao kujinadi kwa wananchi baada ya mtiania huyo kepten mstaafu Jacob Mpangala kutumia maneno ya uongo na lugha chafu dhidi ya mbunge huyo wakati akiomba kura .
Tukio hilo limetokea majira ya saa 11 jioni katika viwanja vya ofisi ya CCM kata ya ibumi wakati mgombea huyo ambae alikuwa wa mwisho kujieleza na kuomba kura kujikuta akishishwa jukwaani kwa kuzomewa huku baadhi ya wananchi wakimsogelea kwa lengo la kutaka kumpiga kwa madai ni muongo na anatumika kumchafua mbunge wao na mmoja kati ya vigogo wa CCM ambae alikuwa akitaka ubunge wa jimbo hilo.
Kabla ya mtia nia huyo kukutwa na tukio hilo la kuzomewa na kutaka kupigwa tayari mbunge Filikunjombe alikuwa ameanza kujieleza na kuwaeleza wananchi hao kazi ambazo amepata kuzifanya na kazi ambazo anataraji kuzifanya kwa awamu ya pili iwapo watamchagua tena katika kinyang'anyiro hicho
Akijinadi kwa wananchi hao huku akishangiliwa na kwa kuitwa jembe letu ,Filikunjombe alisema kuwa amejitahidi kufanya kazi kubwa kulingana na uwezo wake na atakuwa muongo mbele za Mungu na wananchi hao iwapo atajisifu kuwa amemaliza kero zote za wananchi wa Ludewa ila anajivunia kuwepo kwa maendeleo makubwa ukilinganisha na wabunge waliopita na yale yaliyofanywa na wabunge wenzake.
'' Ndugu zangu natambua nimefanya mengi kulingana na uwezo wangu na kulingana na wabunge wenzangu waliotangulia ila sipendi kuwadanganya kuwa matatizo ya wana Ludewa nimeyamaliza yote ......kupanga ni kuchagua na mimi nilichagua kuanza na mambo makubwa mawili likiwemo na kuanza kwa miradi mikubwa ya mchuchuma na liganga ambayo wakati wowote kabla ya Rais Dr Jakaya Kikwete hajamaliza muda wake atafika kuweka jiwe la msingi la uanzwaji na ujenzi wa viwanda hivyo .....lakini pia juu ya miundo mbinu tayari ujenzi wa barabara ya lami umeanza na mengine mengi ambayo hajakuwemo katika ahadi zangu ili nilifanya kulingana na uhitaji wa wananchi wangu'
Filikunjombe ambae muda wote wakati akijinadi wananchi walishindwa kujizuia kushangilia mbali ya kuzuiwa kufanya hivyo alisema kuwa matumaini yake ni kuona kasi ya maendeleo katika jimbo hilo inazidi kupaa zaidi ya hapo na kuwa ushirikiano ambao wananchi wameonyesha kwake kwa kipindi kilichopita ndio ambao anategemea wataonyesha kwake kwa kumchagua kwa kura nyingi zaidi siku ya Augost 1 mwaka huu wakati wa kura za maoni .
Hata hivyo aliwataka wana ccm na wananchi wa Ludewa kujiepusha na kauli za uongo ambazo zinatolewa hivi sasa na baadhi ya wagombea ambao wanatumika kumchafua na badala yake kubaki na msimamo wao wa kushirikiana nae kuendelea kuleta maendeleo zaidi .
katika hali isiyo ya kawaida wananchi hao waliomba kurusiwa kumshingalia ama kumpa zawadi mbunge huyo kama pongezi zao kwa kazi kubwa aliyoifanya japo mratibu wa zoezi hilo la kuwatembeza watia nia hao alizuia kuwa taratibu haziruhusu .
Hali ya mkutano huo ilionekana ni shwari hadi mtia nia wa pili injinia zephania chaula alipopanda jukwaani na kujinadi na kuulizwa maswali yake matatu na kujibu kisha kuomba kura zake ila upepe ulibadilika ghafla alipopanda mpangala ambae alionyesha kuwa na jazba zaidi na badala ya kuwaeleza wananchi atafanya nini alianza kubeza maendeleo yaliyofanywa na mbunge huyo pamoja na kutumia lugha za matusi ya nguoni kumshambulia mbunge kbala ya wananchi kupandwa na hasira na kuanza kumzomea na wengine waklitawanyika katika mkutano huo huku baadhi yao wakipangwa na jazba na kumshusha mgombea huyo jukwaani kwa kutishia kumpiga.
Wananchi hao walifikia hatua hiyo baada ya mtia nia huyo ambae ni mara yake ya kwanza kufika katika kata hiyo kudai kuwa kazi za maendeleo zilizofanywa na mbunge katika kata hiyo na zile za ujenzi wa lami amezifanya yeye huku akitukana matusi ya nguoni mbele ya watoto na wananchi hao hali iliyopandisha hasira na kumshusha jukwaani kabla ya mratibu wa zoezi hilo kulingilia kati na kumpokonya kipasa sauti na kumtaka akae katika kiti na kuzuia kuulizwa maswali na kuvunjwa mkutano huo kwa usalama wa mgombea huyo ambae alionyesha kuwakwaza wananchi kabla ya wao kuhamaki na kutaka kumchapa.
Wakizungumza kwa jazba wananchi hao akiwemo mzee Joachim Luoga walisema kuwa wamesikitishw sana na hatua ya mtia nia huyo kutumia vibaya jukwaa na kutukana matusi ya nguoni badala ya kueleza sera zake kwa wana Ludewa na kuwa wao kama wazee walimtaka aombe radhi ila amnegoma na kuwa wanakiomba chama cha mapinduzi kumwondoa mtia nia huyo katika mchakato huo kwani anavuruga sifa ya chama.
Mratibu wa zoezi hilo la kuwazungusha watia nia hao John Kiowi akizungumza na wananchi hao mbali ya kuwaombra radhi kwa kauli za matusi za mtia nia huyo bado alisema watia nia wote walionywa kuepuka lugha chafu badala ya kunadi sera zao na kuwa kilichomkutano Mpangala ni matokeo ya kutoheshimu taratibu na hivyo wamelazimika kuvunja mkutano huo ili kuokoa usalama wake.
Hali ya upepo wa kisiasa katika jimbo la Ludewa bado ni ngumu zaidi kwa watia nia hao wawili kutokana na wananchi kuonyesha imani yao na mbunge Filikunjombe na kila mkutano ambao akianza kuomba kura mbunge Filikunjombe wananchi wote hutawanyika huku wakiimba nyimbo za jembe letu kama ishara ya kumuunga mkoano na kumpongeza mbunge huyo kwa kazi aliyoifanya .
|
|
0 comments:
Post a Comment