Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda apokea mitambo ya kisasa ya kutengenezea barabara na miundombinu mingine kwa ajili ya Halmashauri ya Mji wa Njombe

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akipokea mfano wa Ufunguo kutoka kwa Mkurugenzi wa kamapuni ya GF Trucks & Equipment Ltd ya jijini Dar es Dar es Salam Bw. Imran Karmali baada ya makabidhiano ya Mitambo ya Kisasa ya kutengeneza Barabara na miundombinu kwa ajili ya Halmashauri ya Mji wa Njombe. Mitambo hiyo imenunuliwa kwa gharama ya Tsh. Million 700 kwa makubaliano maalum ya mkopo nafuu usiokuwa na riba. Kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd Mehboob Karmali na aliye kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Njombe George Mkindo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akijaribu mojawapo ya mitambo hiyo mara baada ya kukabidhiwa rasmi kwa ajili ya Halmashauri ya Mji wa Njombe. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa kamapuni ya uuzaji mitambo hiyo ya Jijini Dar es Salaam ya GF Trucks & Equipment Ltd Bw. Imran Karmali.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifurahia mojawapo ya mitambo ya kisasa ya kutengenezea barabara na miundombinu mingine iliyonunuliwa na Halmashauri ya Mji wa Njombe kutoka Kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo Imran Karmali, Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Bw. Mehboob Karmali na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Njombe George Mkindo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkabidhi mfano wa Ufunguo wa Mitambo hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa Njombe George Mkindo mara baada ya kuipokea kutoka kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd ambayo ndio walioiuzia Halmashauri hiyo mitambo hiyo.
Spika wa Bunge akitoa shukrani zake kwa uongozi wa Kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd kwa kuiwezesha Halmashauri ya Mji wa Njombe kupata Mitambo ya kisasa ya kutengenezea barabara na miundombinu mingine iliyonunuliwa na Halmashauri ya Mji huo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimsikiliza kwa makini Afisa Mauzo Mwandamizi wa kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd Mhandisi Juma Hamsini alipokuwa akielezea ubora wa mitambo ya kampuni hiyo kabla ya kumkabidhi rasmi Mhe. Spika kwa ajili ya Halmashauri ya Mji wa Njombe. Mitambo hiyo imenunuliwa kwa gharama ya zaidi ya Milion 700 za Kitanzania kwa makubaliano ya mkopo usiokuwa na riba kutoka Mfuko wa Halmashauri ya Mji wa Njombe. Kulia kwa Mhe. Spika ni Mwenyekiti wa Kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd Mehboob Karmali na walioko kushoto ni watendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo wakiongozwa na George Mkindo (mwenye koti)Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Njombe George Mkindo akitoa pongezi zake kwa kampuni ya uuzaji wa mitambo ya ujenzi ya GF Trucks & Equipment Ltd baada ya kukubali kuizia Halmashauri yake Mitambo ya kutengenezea barabara na miundombinu mingine katika Halmashauri ya Mji wa Njombe kwa Mkopo usio kuwa na Riba wa kiasi cha Million 700 za Kitanzania.
Mhe. Makinda akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kupokea mitambo hiyo.
Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.

SEMINA YA SIKU YA MAWASILIANO NA HABARI JAMII DUNIANI YAFANA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA MANYUNYU MKOANI NJOMBE

 Viongozi wa TCRA ,Walimu na wanafunzi wakielekea ukumbini katika sherehe hizo 

Wadau Mbali mbali wakisikiliza wakati Semina hiyo inaendelea jana
Kaimu Meneja wa mawasiliano Kanda Ndugu Asajile akiwafundisha wanafunzi umuhimu wa vifaa mbali mbali vya Digital
 Wanafunzi wa Shule ya Manyunyu Mkoani Njombe wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi 

 Wanafunzi wa Shule ya Manyunyu Mkoani Njombe wakionesha vipaji vyao katika sherehe hizo 


 Shule ya Sekondari ya wasichana Manyunyu wakikabidhiwa Tv ya kisasa yenye inch 32 LCD


Baadhi ya zawadi walizo kabithiwa shule ya wasichana ya Manyunyu Mkoani Njombe 

Mgeni Rasmi akimkabidhi zawadi mwanafunzi aliye jibu maswali vizuri Hidaya Mapunda aliyepata Laptop ya kisasa 

 Mwanafunzi Hidaya Mapunda akiwaonesha wenzake Laptop yake 
 Mgeni Rasmi katika Sherehe hizo akiendelea kukabidhi zawadi mbali mbali Shuleni hapo 
 Wanafunzi walio Hudhuria katika Sherehe hizo za Siku ya mawasiliano 
 Mgeni Rasmi akipanda Mti shuleni hapo mara baada ya kumaliza shughuli zote 

Habari kamili itawajia siku ya Sherehe zenyewe 
Picha zote na Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu Blog





WASICHANA WA SHULE YA SEKONDARI MANYUNYU NJOMBE WAFAIDIKA NA SEMINA YA KUTUMIA KOPYUTA NA UMUHIMU WA MFUMO WA DIGITAL

Wasichana wa shule ya sekondari ya wasichana manyunyu mkoani njombe wakimsikiliza mwana sayansi wa masafa
Peter Kihogo kutoka mamlaka ya mawasiliano kanda ya nyanda za juu kusini

Mwanasayansi wa masafa Peter Kihogo akiendelea kuwaelimisha wasichana wa shule ya sekondari manyunyu juu ya umuhimu wa mawasiliano na faida zake katika masomo na shughuli mbalimbali za kila siku katika jamii

Katibu muhtasi mamlaka ya mawasiliano kanda ya nyanda za juu kusini Frida Msese akipeana ushauri na wasichana wa shule ya sekondari manyunyu

Wanafuzi wakiwa makini kumsikiliza mwanasayansi wa masafa


Mkuu wa shule ya ya sekondari manyunyu  Adolphina Katembo akiwashukuru waedesha semina ya mawasiliano na habari jamii toka mamalaka ya mawasiliano kanda ya nyada za juu kusini kuichagua shule yao kuwa mojawapo ya shule katika kupewa semina hiyo ya mawasiliano duniani

MWANAMKE ASWAKWA KWA KUTOROSHA MTOTO NA FEDHA TSH.MILIONI 15 MAKAMBAKO NJOMBE

Mwanamke Queen Daniel Chonya (26) anayedaiwa kumtorosha mtoto na kukimbia na kiasi cha shilingi milioni 15 za mumewe






Mtoto anayedaiwa kutoroshwa




Mwanamke mkazi wa mji wa Makambako wilaya ya Njombe mkoa wa Njombe Queen Daniel Chonya (pichana juu) anatafutwa na mume wake mfanyabiashara wa mji wa Makambako Timoth Mbuma kwa tuhuma za kumtorosha mtoto pamoja na kukimbia na kiasi cha fedha kiasi cha shilingi milioni 15.


Akizungumza na mtandao huu wa http://www.francisgodwin.blogspot.com/ mfanyabiashara huyo Bw Mbuma amesema kuwa mwanamke huyo ametoroka na mtoto wa kiume mwenye mwaka mmoja na miezi mitano anayeitwa Given au Juniour na kuwa mwanamke huyo mkazi wa Malangali wilaya ya Mufindi ambaye ameishi naye kwa miaka minne sasa katika eneo la Mwembetogwa mji wa Makambako.




Ameongeza kuwa kabla ya kutoweka yeye na mkewe huyo hapa kuwa na ugomvi wowote na kuwa machi 19 siku ya jumatatu asubuhi ambapo alimuita dukani kwa ajili ya kutumwa bank ya NBC kupeleka fedha kiasi cha shilingi milioni 15 .


Baada ya kupewa fedha hizo alikwenda nyumbani na kufungasha baadhi ya vitu kama nguo na vyombo na kutoweka na kuwa mwanamke huyo anasemekana yupo jijini Mwanza ama jijini D'Salaam na kuwa hadi sasa tukio hilo limeripotiwa polisi kwa kumbukumbu namba MKB/RB/709/12 na kuwa kwa yeyote mwenye taarifa anaweza kutumia namba 0752242464 au 0786505524 ama 0655505524 kuwa kubwa hapa anahitaji mtoto na kuwa mtu yeyote mwenye taarifa sahihi alipo mwanamke huyo atazawadiwa donge nono



TAKUKURU NJOMBE YAMNG'ANG'ANIA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA LUDEWA

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ludewa Mhe. Matei Kongo

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wilayani Ludewa mkoani Njombe jana imempandisha mahakamani Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Matei Kongo na kusomewa mashtaka upya ya kuomba na kupokea rushwa kiasi cha shilingi 100,000 kati ya shilingi 300,000 alizokuwa akiomba


Akisoma upya mashtaka mbele ya Hakimu mkazi Wilaya ya Ludewa Fredrick Lukuna mwendesha mashtaka wa TAKUKURU mkoa wa Njombe Malekano Richard aliiambia mahakama ya Hakimu mkazi Wilayani hapa kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Machi
12 mwaka huu katika bar na Hotel ya Merland Ludewa mjini.


Katika kosa la kwanza Bwana Malekano alisema mshtakiwa huyo ambaye pia ni diwani wa kata ya Luilo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa aliomba
kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Samsoni Mwaipugile ili aweze kumpa
upendeleo katika zabuni mbalimbali ikiwemo kusambaza kompyuta na tenda
za ujenzi wa majengo.


Malekano aliiambia mahakama kuwa kosa la pili linaangukia katika
kifungu namba 15(1)(A) cha taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa,
na kwamba kwa nyakati tofauti kati ya disemba mwaka jana na machi
mwaka huu mshtakiwa Kongo aliomba rushwa ya shilingi milioni tatu
ambapo machi 12 mwaka huu alipokea kiasi cha shilingi laki moja
kupitia kwa wakala wake Aidani Luoga zilizotolewa na Samsoni
Mwaipugile mkazi wa Dar-es salaamu.


Hata hivyo mshtakiwa Mathei Kongo mbele ya mahakama alikana kuhusika
na makosa yote yanayomkabili.


Aidha mwendesha mashtaka Marekano Richard aliiambia mahakama kuwa
upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika na kuiomba
mahakama ipange tarehe ya kusikilizwa.


Kesi hiyo imeahirishwa hadi mei 9 mwaka huu itakapokuja kusikilizwa na
dhamana ya mshtakiwa itaendelea.


Mshitakiwa huyo amesomewa upya shitaka hilo kutokana na awali kufikishwa kimakosa katika mahakamani ya Mwanzo na kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kisheria kusikiliza kesi hiyo imelazimika kusomwa upya katika mahakama hiyo ya hakim mkazi wa wilaya ya Ludewa .
Habari kwa Hisani ya Francis Godwin

Rais Jakaya Kikwete amwapisha Asery Msangi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe

 Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Kapt Asery Msangi kuwa Mkuu wa Mkoa
wa Njombe katika sherehe zilizofanyika leo asubuhi Ikulu jijini Dar es
salaam
Picha Kwa Hisani Ya Father Kidevu Blogu

KIFO CHA DIWANI WA CCM LUDEWA NI PIGO KWA CCM


Madiwani wa Ludewa 
Na Francins Godwin- NjombeDIWANI wa kata ya Mlangali wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Rudolph Chaula (CCM)ambaye pia alikuwa ni meneja wa Chama cha kuweka na kukopa cha Mlangali (SACCOS) ameamua kujinyonga ndani ya ofisi yake ya udiwani akidaiwa kukwepa madeni .


Diwani Chaula alijinyonga usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake Mlangali na kudaiwa kuacha ujumbe wa maandishi wenye utata mkubwa.


Imeelezwa kuwa chanzo cha diwani huyo kujinyonga ni kutokana na kuzidiwa na mzigo wa madeni kutoka katika Chama cha kuweka na kukopa cha Mlangali ( SACCOs) ambako alikuwa ni meneja.


Mmoja kati ya wanachama wa Mlangali Sacos ambaye hakupenda kutajwa jina lake katika vyombo vya habari kwa kuwa si msemaji wa Chama hicho alisema kuwa siku mbili nyuma walifika wakaguzi na kufanya ukaguzi katika Chama hicho cha ushirika na kubaini kuwepo deni kubwa lisilojulikana mkopaji.


" Mheshimiwa diwani wetu ambaye alikuwa ni Mhasibu ( meneja kwa sasa) katika SACCOS hiyo kabla ya wakaguzi hao alikuwa ni mchangamfu kupita kiasi ila baada ya wakaguzi kuja alionekana ni mtu mwenye Msongo mkubwa wa mawazo jambo ambalo liliwafanya wananchi wengi kuingia na Shaka juu ya usalama wa fedha zao" alisema


Kuwa Mlangali SACCOS kilikuwa ni moja Kati ya vyama vya ushirika vyenye nguvu kubwa katika wilaya ya Ludewa ila baada ya Mhasibu wao huo kuingia katika siasa kwa kugombea udiwani mwaka 2010 ndipo Chama kilianza kuyumba zaidi .




Hata hivyo alisema kuwa juzi mchana diwani huyo alionekana mitaani majira ya saa 7 mchana akitafuta kusajili lini yake ya simu ila hakufanikiwa kufanya hivyo akatoweka kusikofahamika.


Hata hivyo alisema kutokana na kutoonekana kutwa nzima usiku ndipo walipomkuta akiwa amejinyonga kwa Kamba katika chumba chake ambacho alikuwa akitumia Kama ofisi.


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangalla amethibitisha kwa njia ya simu kutokea kwa tukio hilo na kuwa taarifa zaidi itatolewa .

JUST IN: DIWANI WA CCM LUDEWA AJINYONGA USIKU HUU


Marehemu Rudolph CHaula a.k.a Kacheche kushoto



Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Ludewa mkoa mpya wa Njombe kimepata pigo kubwa kufuatia diwani wake wa kata ya Mlangali Rudolph Chaula maaarufu kwa jina la Kacheche kujinyonga .


Taarifa ambazo mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com umezipata hivi na kuthibitishwa na katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Eva Degeleki zinadai kuwa diwani huyo amekutwa akiwa kajinyonga katika moja kati ya vyumba vya nyumba yake ambavyo katika enzi ya uhai wake alikuwa akitumia kama ofisi yake ya udiwani.

Katibu huyo wa CCM Ludewa amesema kuwa hadi sasa hana taarifa za chanzo cha kifo chake ila anataarifa ya kujinyonga kwa diwani huyo na kuwa amepokea taarifa hiyo mida ya saa 8.15 usiku huu kujulishwa juu ya kifo hicho.


Imedaiwa kuwa diwani huyo toka mida ya mchana familia yake ilikuwa ikimsaka bila mafanikio baada ya wageni kufika kumuulizia na jitihada za kutafuta huku na kule zilimezao matunda usiku huu baada ya kuwa na wazo la kuvunja chumba hicho na kumkuta diwani huyo akiwa kajinyonga.
Taarifa zaidi inakuja

Kwa hisani ya Francis Godwin mzee wa matukio daima blog

Welcome to Njombe Region Tanzania




Coming Soon
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa