Home » » KIFO CHA DIWANI WA CCM LUDEWA NI PIGO KWA CCM

KIFO CHA DIWANI WA CCM LUDEWA NI PIGO KWA CCM


Madiwani wa Ludewa 
Na Francins Godwin- NjombeDIWANI wa kata ya Mlangali wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Rudolph Chaula (CCM)ambaye pia alikuwa ni meneja wa Chama cha kuweka na kukopa cha Mlangali (SACCOS) ameamua kujinyonga ndani ya ofisi yake ya udiwani akidaiwa kukwepa madeni .


Diwani Chaula alijinyonga usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake Mlangali na kudaiwa kuacha ujumbe wa maandishi wenye utata mkubwa.


Imeelezwa kuwa chanzo cha diwani huyo kujinyonga ni kutokana na kuzidiwa na mzigo wa madeni kutoka katika Chama cha kuweka na kukopa cha Mlangali ( SACCOs) ambako alikuwa ni meneja.


Mmoja kati ya wanachama wa Mlangali Sacos ambaye hakupenda kutajwa jina lake katika vyombo vya habari kwa kuwa si msemaji wa Chama hicho alisema kuwa siku mbili nyuma walifika wakaguzi na kufanya ukaguzi katika Chama hicho cha ushirika na kubaini kuwepo deni kubwa lisilojulikana mkopaji.


" Mheshimiwa diwani wetu ambaye alikuwa ni Mhasibu ( meneja kwa sasa) katika SACCOS hiyo kabla ya wakaguzi hao alikuwa ni mchangamfu kupita kiasi ila baada ya wakaguzi kuja alionekana ni mtu mwenye Msongo mkubwa wa mawazo jambo ambalo liliwafanya wananchi wengi kuingia na Shaka juu ya usalama wa fedha zao" alisema


Kuwa Mlangali SACCOS kilikuwa ni moja Kati ya vyama vya ushirika vyenye nguvu kubwa katika wilaya ya Ludewa ila baada ya Mhasibu wao huo kuingia katika siasa kwa kugombea udiwani mwaka 2010 ndipo Chama kilianza kuyumba zaidi .




Hata hivyo alisema kuwa juzi mchana diwani huyo alionekana mitaani majira ya saa 7 mchana akitafuta kusajili lini yake ya simu ila hakufanikiwa kufanya hivyo akatoweka kusikofahamika.


Hata hivyo alisema kutokana na kutoonekana kutwa nzima usiku ndipo walipomkuta akiwa amejinyonga kwa Kamba katika chumba chake ambacho alikuwa akitumia Kama ofisi.


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangalla amethibitisha kwa njia ya simu kutokea kwa tukio hilo na kuwa taarifa zaidi itatolewa .

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa