Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Ally Daud-MAELEZO
WAFANYABIASHARA
wa viumbe pori hai wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli kufungulia biashara ya viumbe hao kutokana na
kusitishwa Machi mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii Jumanne
Magembe.
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Viumbe pori hai Bw. Salim
Mussa amesema kuwa wanamuomba Mh. Rais Magufuli aingilie kati swala
hilo na kupata ufumbuzi wa kudumu wa kuendelea na biashara hiyo ya
viumbe kwa maendeleo yao na uchumi wa taifa.
“Tunakuomba
Mh. Rais Magufuli uingilie kati swala hili na kutupatia ufumbuzi wa
kudumu ili kuendlea na biashara ya viumbe pori hai bila ya usumbufu wa
mara kwa mara kwani biashara hii ipo kwa mujibu wa sheria , taratibu na
kanuni za nchi” alisema Bw. Salim.
Aidha
Bw. Salim amesema kuwa maamuzi hayo yanaweza kusababisha hasara kubwa
kwa jumuiya ya wafanyabiashara wa viumbe hivyo na uchumi wa nchi kwa
ujumla kwani muongozo haujatolewa tangu kusitishwa kwa biashara hiyo mwezi machi mwaka huu.
Kwa
upande wake Msemaji wa wafanyabiashara wa viumbe pori hai Bw. Enock
Balilemwa amesema kuwa kusitishwa kwa biashara hiyo imepunguza kiwango
cha ajira kwa kiasi cha watanzania milioni moja ambao asilimia 95
wanaishi vijijini.
“kusitishwa
kwa biashara hii ya viumbe pori hai imefanya watanzania takribani
milioni moja hasa wakazi wa vijini asilimia 95 kukosa ajira jambo ambalo
linapelekea wananchi hao kukosa uwezo wa kujikimu kwa maisha ya kila
siku” alisema Bw. Balilemwa.
Biashara
hiyo ya viumbe pori hai inayojumuisha Vyura, wadudu, ndege,mijusi na
tumbili, zoo na mashamba ya wanyapori ilianza kabla ya uhuru sambamba na
leseni zingine za uwindaji wa kitalii ambayo mpaka sasa inatambulika
kwa sheria namba 5 ya mwaka 2009.