Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKUU wa Wilaya ya Makete mkoani Njombe, Daud Yassin amewaambia
wananchi wa wilaya hiyo kwamba Uchaguzi Mkuu umekwisha na sasa
kilichobaki ni wananchi na viongozi wa ngazi zote kuiunga mkono kwa
dhati Serikali inayotekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), chini
ya Rais John Magufuli.
Yassin alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na wananchi katika
Kata ya Iwawa wilayani humo na kuwataka kumpa ushirikiano kwa pamoja,
ili kutekeleza ilani hiyo pamoja na kuijenga Makete yao.
“Uchaguzi Mkuu umekwisha na sasa kilichobaki ni kwetu sote kuiunga
mkono Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli ili kutekeleza ilani yake,
kusaidiana naye katika kutimiza yote aliyoyaahidi kuwafanyia
Watanzania,” alieleza.
Alisema hadi sasa Rais Magufuli ameonesha moyo wa dhati wa
kuwatumikia wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vyao, hivyo
anahitaji kuungwa mkono na wana Makete ili maendeleo yaweze kupatikana.
“Kinachotakiwa kwa sasa ni kuungana kwa pamoja na kushirikiana ili
wilaya yetu izidi kusonga mbele,” alieleza na kuongeza kuwa milango ipo
wazi kwa yeyote mwenye ushauri au maoni, ama mwenye kero yoyote afike
ofisini kwake na atasikilizwa.
CHANZO ; HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment