Wakulima watataelimu ya kuboresha mazao, kilimo mikoa mitatu ya nyanda za ju kusini

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Abiud Gamba mmoja wa menejimenti ya ACTN
 Mkurugenzi wa ACTN Said Komwa


Washiriki wa mafunzo ya kuboresha kilimo mikoa mitatu ya 
Njombe, Ruvuma na Iringa

WAKULIMA kutoka katika vikundi mbalimbali kutoka halamashauri za Namtumbo wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma, Ludewa Mkoani Njombe na halmashauri ya Mufindi Mkoani Iringa wametakiwa kuhakikisha wanahifadhi vizuri mazao yao ili kuingiza katika ushindani wa soko la mazao yao na kuhakikisha wanasafisha na kukausha vizuri.

Wito huo umetolewa na Frank Mhando kutoka kampuni ya Agra inayojishughurisha na kuwasaidia wakulima kuinuka kiuchumi, kwa kuboresha mazao yao kutoka kilimo hadi mavuno wakati wa semina kwa wakulima hao iliyoandaliwa Taasisi ya African Conservation Tillage Network, (ACTN) na kufanyika Njombe mjini.

Alisema kuwa wakulima wengi wamekuwa wakilalamika masoko hamna kitu kinacho shusha bei ya mazao ni kutokana na kuto kuwapo kwa utunzaji bora wa mazao na kushindwa kuyaweka katika hali ya usafi.

Mhando alisema kuwa wakulima wengi wamekluwa wakaweka mazao yao katika hali ya uchafu kitu kinacho wakimbiza wanunuzo na kuleta malalamini ya kuto nunuliwa kwa mazao hayo.

Alisema kuwa; “Wakulima wamekuwa walikusanya mahidi yaliyo vunjika vunjika na mazuri kitu kinacho kimbiza wateja kwani nao wakinunua kwako watashindwa kuuza kwa kuwa sio masafi, lakini kama utaweka katika hali ya usafi utaweza kupoata wateja kwa bei nzuri.

Aidha kwa upande wao wakulima kutoka Songea, Namtumbo, Ludewa na Mafinga wamesema kuwa kwa kupata elimu hiyo waliyo itata wataendeleza kilimo chao kwa kwenda kufuiata kanuni za uhifadhi, usafi wa mazao, na kulima kilimo hifadhi ili mashamba yao kuwa imara na kurutubika.

Wamesema kupitia elimu hiyo wataenda kuielimisha na jamii inayo wazunguka ili nako kujitahidi kulima kilimo hifadhi na kuweka safi mazao yao kwa kuhufadhi bira kuweka viwatilifu vya maji ili kuwa na mazao yenye usalama.

Akifunga mkutano huo Mkurugenzi wa ACTN, Said Komwa alisema kuwa wakulima wajitahitu kulima kilimo hifadhi kwaajili ya kujipatia kipato maradufu ya wanavyo pata sasa na kuwa kilimo hifadhi hulinda shamba na kusisitiza kuchambua mazao yao ili mnunuzi asipate mashaka na mazao yao.
Alisema kuwa wakulina wanawajibu wa kuhufadhi kwa pamoja mazao yao ili kupata wateja wa jumla kuliko kuuza mazao mmoja mmoja na hatimaye kufikia malengo yao ya kuwa na maisha bora.

WANANCHI LUDEWA WAMZOMEA MGOMBEA UBUNGE AOKOLEWA KUPIGWA KISA UONGO KUMTUKANA FILIKUNJOMBE‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

kada wa CCM anayeomba  kuteuliwa  kugombea ubunge jimbo la Ludewa kepten mstaafu Jacob Mpangala ambae leo amezomewa mkutanoni na kuokolewa  kichapwa baada ya kujinadi kwa kutumia lugha za matusi na uongo dhidi ya mbunge Deo  Filikunjombe 
mbunge Filikunjombe akiwapungia mkoano  wananchi wa mndindi baada ya  kujinadi
wananchi wa kata ya Ibumi  wakiwa  wametuliwa wakimsikiliza kwa makini mbunge Filikunjobe wakati akiomba  kura  zao
Filikunjombe  akisisitiza jambo wakati akiomba kura kwa wananchi wa Ibumi leo ,wananchi hao walivuruga mkutano  huo baada ya mtia nia mmoja kupanda jukwaani na kutoa taarifa  za uongo na matusi ya nguoni dhidi ya mbunge wao
Filikunjombe akiwashukuru wananchi wa Ibumi kwa imani yao kwake
mratibu wa  zoezi la kuwanadi wagombea kwa wana ccm John kiowi akitangaza kuvunja mkutano  huo baada ya kuibuka vurugu .

Na matukiodaima BLOG

 KATIKA kile  kinachoonyeshwa  kuwa wananchi  wa Ludewa kumkubali mbunge wa  jimbo  hilo Deo Filikunjombe kuendelea kuongoza  jimbo  hilo kwa awamu  nyingine leo  wana CCM na  wananchi  wa kata  ya Ibumi wamemzomea mmoja kati ya watia nia ubunge wa jimbo hilo na  kutaka kumchapa wakati wa mkutano wa  watiania hao kujinadi kwa  wananchi baada ya mtiania  huyo kepten mstaafu Jacob Mpangala kutumia maneno ya uongo na  lugha chafu dhidi ya mbunge huyo  wakati akiomba kura .

Tukio   hilo  limetokea majira ya saa 11 jioni katika   viwanja vya ofisi ya  CCM kata ya  ibumi wakati mgombea  huyo ambae alikuwa wa  mwisho kujieleza na kuomba  kura kujikuta akishishwa  jukwaani kwa kuzomewa huku baadhi ya wananchi wakimsogelea  kwa lengo la kutaka  kumpiga kwa madai ni muongo na anatumika kumchafua mbunge  wao na mmoja kati ya vigogo  wa CCM ambae alikuwa akitaka ubunge wa  jimbo  hilo.


Kabla ya  mtia nia  huyo  kukutwa na tukio  hilo la  kuzomewa na kutaka kupigwa tayari mbunge  Filikunjombe alikuwa ameanza  kujieleza na kuwaeleza  wananchi hao kazi ambazo amepata  kuzifanya na kazi ambazo anataraji kuzifanya kwa awamu ya  pili iwapo watamchagua tena katika  kinyang'anyiro  hicho 


Akijinadi kwa wananchi hao huku akishangiliwa na kwa kuitwa jembe letu ,Filikunjombe alisema  kuwa amejitahidi kufanya kazi kubwa  kulingana na uwezo wake na  atakuwa muongo mbele za Mungu na  wananchi hao iwapo atajisifu kuwa amemaliza kero  zote za  wananchi wa Ludewa ila anajivunia kuwepo kwa maendeleo makubwa ukilinganisha na wabunge  waliopita na yale yaliyofanywa na wabunge  wenzake.

'' Ndugu  zangu  natambua  nimefanya mengi  kulingana na uwezo wangu na kulingana na wabunge  wenzangu  waliotangulia ila sipendi kuwadanganya  kuwa matatizo ya  wana Ludewa nimeyamaliza  yote ......kupanga ni kuchagua na mimi nilichagua kuanza na mambo makubwa mawili likiwemo na kuanza kwa miradi mikubwa ya mchuchuma na liganga ambayo  wakati wowote kabla ya Rais Dr Jakaya Kikwete hajamaliza  muda  wake atafika  kuweka  jiwe la msingi la uanzwaji na ujenzi wa viwanda   hivyo .....lakini  pia juu ya miundo mbinu tayari ujenzi wa barabara ya lami umeanza  na mengine mengi ambayo hajakuwemo katika ahadi  zangu  ili  nilifanya kulingana na uhitaji wa  wananchi wangu'


Filikunjombe ambae  muda  wote  wakati akijinadi  wananchi  walishindwa  kujizuia  kushangilia mbali ya kuzuiwa kufanya  hivyo alisema  kuwa matumaini yake ni kuona kasi ya maendeleo katika  jimbo  hilo  inazidi kupaa zaidi ya hapo na  kuwa ushirikiano ambao wananchi  wameonyesha kwake kwa  kipindi  kilichopita  ndio ambao  anategemea  wataonyesha  kwake kwa kumchagua kwa kura  nyingi  zaidi siku ya Augost 1 mwaka huu wakati wa  kura  za maoni .

Hata  hivyo  aliwataka  wana ccm  na  wananchi wa Ludewa  kujiepusha na kauli  za uongo ambazo  zinatolewa  hivi  sasa na baadhi ya wagombea ambao wanatumika  kumchafua na badala  yake  kubaki na msimamo  wao wa  kushirikiana nae kuendelea  kuleta maendeleo  zaidi .

katika hali  isiyo ya kawaida wananchi hao  waliomba kurusiwa  kumshingalia ama  kumpa  zawadi  mbunge huyo kama pongezi zao kwa kazi kubwa aliyoifanya  japo mratibu wa  zoezi  hilo la kuwatembeza  watia nia hao alizuia kuwa  taratibu haziruhusu .

Hali ya mkutano huo  ilionekana ni shwari hadi mtia nia wa pili injinia zephania chaula alipopanda jukwaani na kujinadi na kuulizwa maswali yake matatu   na  kujibu kisha  kuomba  kura  zake  ila upepe  ulibadilika  ghafla  alipopanda  mpangala ambae alionyesha  kuwa na jazba  zaidi na badala ya  kuwaeleza wananchi atafanya nini  alianza kubeza maendeleo yaliyofanywa na mbunge   huyo pamoja na kutumia  lugha za matusi ya nguoni kumshambulia mbunge kbala ya  wananchi kupandwa na hasira na  kuanza kumzomea na wengine  waklitawanyika katika mkutano  huo huku baadhi yao wakipangwa na jazba na kumshusha mgombea  huyo jukwaani kwa kutishia  kumpiga.

Wananchi hao  walifikia hatua  hiyo  baada ya mtia  nia huyo ambae ni mara  yake ya kwanza  kufika katika  kata  hiyo kudai  kuwa kazi za maendeleo  zilizofanywa na mbunge katika kata  hiyo na zile za ujenzi wa lami amezifanya yeye huku akitukana matusi ya nguoni mbele ya watoto na  wananchi hao hali  iliyopandisha hasira na kumshusha jukwaani  kabla ya mratibu wa zoezi hilo kulingilia kati na kumpokonya kipasa  sauti na kumtaka akae katika kiti na kuzuia kuulizwa maswali na kuvunjwa mkutano  huo kwa usalama wa mgombea  huyo ambae alionyesha  kuwakwaza  wananchi kabla ya  wao kuhamaki na kutaka kumchapa.

Wakizungumza kwa jazba  wananchi  hao akiwemo mzee Joachim Luoga walisema  kuwa  wamesikitishw sana na hatua ya mtia  nia huyo  kutumia  vibaya  jukwaa na kutukana matusi ya nguoni  badala ya  kueleza sera  zake kwa wana Ludewa na kuwa wao kama  wazee  walimtaka aombe radhi ila amnegoma na kuwa wanakiomba  chama cha mapinduzi kumwondoa mtia nia huyo katika mchakato  huo kwani anavuruga sifa ya  chama.


Mratibu wa zoezi hilo la  kuwazungusha watia nia hao John Kiowi akizungumza na  wananchi hao mbali ya  kuwaombra  radhi kwa kauli za matusi za mtia nia  huyo  bado alisema  watia nia  wote  walionywa  kuepuka  lugha  chafu badala ya  kunadi  sera  zao na kuwa kilichomkutano Mpangala ni matokeo ya kutoheshimu taratibu na  hivyo wamelazimika  kuvunja mkutano  huo ili  kuokoa usalama  wake.

Hali ya  upepo  wa kisiasa katika jimbo la Ludewa bado ni ngumu zaidi kwa  watia nia  hao wawili kutokana na wananchi kuonyesha imani yao na mbunge Filikunjombe na kila mkutano ambao akianza  kuomba  kura mbunge Filikunjombe wananchi wote  hutawanyika   huku wakiimba nyimbo za jembe letu kama ishara ya kumuunga mkoano na  kumpongeza mbunge  huyo kwa kazi aliyoifanya .



MTANGAZA NIA UBUNGE LUDEWA AANGUKIA PUA NAFASI YA NEC ,ASEMA HATAKI TENA KUGOMBEA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
aliyeshindwa ujumbe wa NEC Ludewa Injinia Zephania Chaula  akiangana na mbunge  Deo  Filikunjombe baada ya  kushindwa katika nafasi  hiyo ,Chaula alikuwa ni mmoja wa wana CCM waliokuwa  wakitaka kuwania ubunge jimbo la Ludewa
Chaula akiagana na mshindi mzee Nkwera 
 Mkuu  wa wilaya ya  Ludewa Antonia Choya akimkabidhi  hati ya  shukrani mbunge wa Ludewa  Deo Filikunjombe (kushoto)




 Mjumbe  wa  mkutano huo Bw  Choya  akipiga  kura
 Wajumbe  wakishiriki  kupiga  kura
 

 Wajumbe  wakishiriki  kupiga kura
 Mgombe  Chaula  akishukuru kwa  kushindwa
 Injinia  Chaula  akimpongeza mshindi mzee Nkwera
Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe  akipiga  kura  kumchangua mjumbe wa NEC Ludewa
 
 Mkuu  wa  wilaya ya  Ludewa  Deo  Filikunjombe akikabidhiwa hati ya  shukrani ya kushiriki mbio  za Mwenge  toka kwa mkuu wa wilaya ya  Ludewa Antonia Choya ,hati  iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Njombe
Na MatukiodaimaBlog


MBIO  za  ubunge jimbo la  Ludewa  mkoani  Njombe zimeishia hewani  kwa mtangaza  nia wa  wanafasi  hiyo Injinia  Zephania  Chaula  baada ya  kuambilia  kura 11 pekee katika nafasi ya mjumbe  wa Halmashauri  kuu ( NEC) Taifa kutoka  wilaya ya Ludewa  aliyokuwa akiwania dhidi ya katibu msaidizi  wa mbunge wa  jimbo la Ludewa  Hilaly  Nkwera  aliyeibuka mshindi kwa  kupata  kura 138 kati ya  kura  zote halali 151 zilizopigwa .

Huku mgombea  huyo aliyeshindwa katika nafasi hiyo ya Ujumbe wa NEC Injinia Chaula  akiapa  kutogombea tena nafasi hiyo kwa madai kuwa ni mara ya pili sasa anashindwa  vibaya  katika  mchakato  wa  kuwania nafasi hiyo ambapo awali alishindwa mgombea  wa darasa  la  saba marehemu Elizabeth Haule .

Uchaguzi  huo  mdogo  wa  kuziba nafasi ya  mjumbe  wa  NEC  iliyoachwa  wazi na aliyekuwa  mjumbe wa nafasi hiyo Elizabeth Haule  aliyefariki  dunia mapema mwaka  huu ,ulifanyika  mwishoni mwa  wiki  hii kwa  kuwashirikisha  wagombea  hao  wawili kabla ya mgombea  mwingine ambae ni mbunge  wa  jimbo la Ludewa Deo  Filikunjombe  kuandika barua ya  kujitoa katika  kinyang'anyiro  hicho akiwapisha wagombea  hao  wachuane  kutokana na yeye  kudai  kuwa atachukua fomu ya kugombea tena  ubunge  wa  jimbo  hilo la Ludewa .

Akitangaza  matokeo  hayo ya  uchaguzi msimamizi  mkuu  wa uchaguzi huo  Lucas Nyanda  ambae ni katibu  wa  jumuiya  ya  wazizi wa CCM mkoa  wa Njombe  ,alisema  kuwa  jumla ya  wajumbe  waliopaswa  kushiriki katika  uchaguzi  huo ni 164 ila   wajumbe  halali  walioshiriki ni 151 na kati ya  wajumbe  hao kura 2  ziliharibika  huku Injinia Chaula akipata  kura 11 na mshindi wa nafasi hiyo Bw  Nkwera  akipata  kura 138

Awali  mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Bw  Filikunjombe  ambae alikuwa ni mmoja kati ya  wana CCM watatu  ambao majina  yao yalirejeshwa  kuwania nafasai hiyo alisema  kuwa analazimika  kujitoa katika  nafasi hiyo  ili  kupisha wanachama  hao wawili  ambao wamemzidi  umri  ili  kuweza  kupambana  na  yeye ataendelea  kuwa kuwatumikia  wananchi  wa Ludewa katika nafasi ya  ubunge pekee.

Akiwashukuru wajumbe kwa ushindi  huo  wa nafasi ya ujumbe wa NEC Bw  Nkwera ambae  kitaaluma ni mwalimu na pia amepata  kuwa mwenyekiti wa Halmashauri ya  wilaya ya Ludewa na mwenyekiti wa madiwani wa mkoa wa Njombe na Iringa  alisema kuwa amefurahishwa na imani  kubwa ambayo wana CCM wameionyesha  kwake  kwa  kumchagua  kuwa mwakilishi wao katika vikao  vya  kitaifa .

Bw  Nkwera  alisema wana CCM Ludewa waamini  kuwa nafasi hiyo hawajakosea  kumpa na kamwe  hatawaangusha kwani atahakikisha anawatumikia  vema katika vikao  vya  juu kwa kuanza na  safari ya  kumpata mgombea wa nafasi ya  Urais wa CCM ambae atakuwa ni chaguo la  wana CCM wote wa Ludewa .

Huku  Chaula mbali ya  kuwashukuru kwa  kura  11 alizopata bado  alisema  kuwa hatakuwa tayari  kuendelea  kugombea tena kwani yawezekana kabisa  Mungu hajapenda  yeye  kuwa  kiongozi wa kisiasa bali ametaka  aendelee  kuwa mtaalam .


“Nasema haya kutoka moyoni mimi ni mwanachama hai wa chama cha mapinduzi na nakipenda chama change hivyo naahidi sitagombea tena katika maisha yangu nafasi hii ya UNEC  kutokana na ukweli kuwa nahisi siasa inanikataa maana kila nikigombea nashindwa hivyo ngoja nifanye kazi nyingine pia nampongeza  sana mshindi Mzee  Nkwera katika utendaji wake ndani ya chama”,alisema Mhandisi Chaula.


  Wakati  huo  huo serikali  ya  mkoa  wa Njombe kupitia mkuu wa mkoa wa Njombe Dr  Rehema Nchimbi imempongeza kwa  kumpa hati ya shukrani  mbunge  wa  jimbo la Ludewa  Bw  Filikunjombe kwa  ushiriki  wake  mkubwa katika kufanikisha  mbio  za mwenge katika  mkoa  huo kwa kuwa mbunge  pekee  kushiriki  mbio  za mwenge na kuchangia vizuri .

Akikabidhi hadi  hiyo mbele ya  wajumbe wa mkutano wa Halmashauri  kuu , mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Anatory Choya aliweza kumtunuku hati hiyo ya  heshima mbunge wa jimbo la Ludewa  Filikunjombe kwa kushiriki kimamirifu katika mbio za mwenge wa Uhuru ndani ya mkoa wa Njombe.

Akitoa cheti hicho Bw.Choya alisema kuwa kutokana na ushiriki alioufanya mh.Filikunjombe katika mbio cha mwenge wa Uhuru mkuu wa mkoa wa Njombe na ofisi yake wameona wampatie cheti cha heshima Filikunjombe kwani ni mbunge pekee aliyeshiriki katika mbio hizo za Mwenge katika mkoa wa Njombe.

MWISHO 

© 2015 Microsoft Terms Privacy & cookies Developers English (United States)
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa