WATU watatu wamekufa mkoani
Njombe katika matukio tofauti likiwemo la ajali iliyosababisha mwanafunzi
kupoteza maisha na wengine wawili kujinyonga.
Kamanda wa polisi mkoani Njombe kamishna msaidizi wa polisi Fulgence Nginyani
amesema katika tukio la kwanza, la april 19 saa 11 jioni katika maeneo ya
uwanja wa polisi makambako, mwanafunzi aliyetambuliwa kwa jina la jina la Helen
Mwitula (9) mwanafunzi wa shule ya msingi Mwembetogwa darasa la tatu
alikufa baada ya kugongwa na gari.
Kamanda Ngonyani amesema,ajali hiyo ilisababishwa na gari lenye namba T. 809
BHC double Cabin pick-up mali ya kampuni ya Jah- People investment Ltd.
ya mjini makambako lililokuwa likiendeshwa na dereva Seily Mtafya (28) ambapo
katika ajali hiyo hiyo,mwanafunzi mwingine Joyce mwakipesile (9) amelazwa
katika...
Afariki kwa kupigwa na kuvunjwa viungo vya mwili
MTU mmoja mwanaume amekufa wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya
ya Kibena mkoani Njombe, baada ya kukutwa akiwa amepigwa na watu wasio julikana
mjini Makambako.
Kamanda wa polisi,kamishna wa polisi mkoani humo, Fulgence Ngonyani, amemtaja
mtu huyo kuwa ni Peles Sanga (33) mkazi wa mji mwema makambako ambaye Aprili 10
saa 10 alfajiri alipokutwa katika pipeline akiwa amevunjwa miguu yote miwili,
na mkono wa kulia kisha kutelekezwa eneo la tukio.
Kamanda Ngonyani amesema, mtu huyo aliokotwa na wasamalia kisha kufikishwa
katika kituo cha afya ambapo alihojiwa na kueleza bayana kuwa alitoka
matembezini na kuvamiwa na watu watatu ambao walivalia makoti meusi
marefu,ambao baada ya kumjeruhi walitokomea kusiko julikana.
Marehemu alifikishwa kibena na kuanza matibabu ambapo...