Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akizungumza katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa watu waliofanya vizuri
katika usafi wa Mazingira leo jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.
Ulisubisya Mpoki akizungumza juu ya Wizara ilivyojipanga katika suala la
usafi wa mazingira katika ya kukabidhi tuzo kwa watu waliofanya vizuri
katika usafi wa Mazingira leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy
Mwalimu akikabidhi Ufunguo wa Gari kwa Mwenyekiti wa Halmshauri Njombe,
Valentino Hongoli baada ya kuobuka mshindi wa jumla wa usafi wa
mazingira katika kampeni ya usafi, Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
akifurahi na washindi walioshinda pikipiki katika kampeni ya usafi wa
mazingira katika usafi wa mazingira katika hafla iliyofanyika leo.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Halmashauri ya Njombe wakiwa katika picha ya pamoja
na gari waliloshinda katika usafi wa mazingira katika hafla iliyofanyika
leo.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
HALMASHAURI
ya Wilaya ya Njombe imeibuka kuwa mshindi wa Jumla wa usafi wa
mazingira na kuifuta historia ya usafi wa mazingira Halmashari ya Moshi
kwa kushika.
Halmashauri ya Njombe imepata asilimia 97 ya usafi wa mazingira na kufuatia Halmashauri ya Iringa Mjini kwa asilimia 81.1 .
Akizungumza
leo wakati wa kutoa tuzo kwa halmashauri ,Manispaa, Majiji, Miji
pamoja na Vijiji ,Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa Halmashauri ya Njombe haijaripoti hata
mgonjwa wa kipindupindu hata mmoja tangu ugonjwa huo ulipotiwe Agasti
mwaka jana.
Amesema
kuwa Halmashauri hiyo imeweza kuwa na vyoo bora kwa asilimia 95 katika
vijiji yake pamoja na kuwa viaa vya kunawia mikono katika vyoo hivyo.
Halmashauri
ya Njombe imepata tuzo ya gari aina ya Land Cruiser Hardtop, Kombe,
Cheti,pamoja pikipiki katika vijiji vitatu ambavyo vimefanya vizuri
katika suala la usafi wa mazingira.
Jiji
la Mbeya limeweza kuibuka mshindi wa kwanza katika majiji kati ya
majjiji manne kutokana na kufanya usafi wa mazingira kwa kuweka mifumo
ya uhifadhi takataka.
Tuzo
ya jijji la Mbeya ni kikombe ,pikipiki pamoja na cheti huku Halmshauri
ya Mji mdogo wa Tundunduma nao ukiibuka kuwa mshindi wa usafi wa
mazingira kwa upande wa miji.
Halmashauri
zingine zilizopa tuzo hizo ni Kahama,Mpanda ,Kondoa huku Mkoa wa Dar
es Salaam ikimbulia Wilaya Moja ya Kinondoni ambapo zimetunikiwa tuzo ya
vikombe, pikipiki pamoja na vyeti.
Kwa
upande wa Hospitali za Rufaa iliyoongoza ni Mount Meru ikifuatia na
Hospitali ya Amani katika nafasi ya pili huku Hospitali ya Morogoro
ikishika nafasi ya tatu.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema katika mashindano yajayo
walioshinda watakuja kuishangilia Dar es Salaam na hawataondoka na
vikombe hivyo na gari.
Amesema
kuwa kuna jitihada ambazo zinafanyika za kuhakisha jiji la Dar es
Salaam linakuwa safi na hatavumiliwa mtu ambaye anachafua mazingira.
KWA HISANI YA MICHUZI BLOG
0 comments:
Post a Comment