Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wameendelea na ziara
ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya Wizara husika
ambapo mwishoni mwa wiki hii walitembelea miradi ya umeme vijijini,
mkoani Njombe.
Miradi
waliyotembelea Wajumbe hao ni pamoja na wa ujenzi wa njia ya umeme wa
msongo wa kilovolti 220 kutoka Makambako hadi Songea na usambazaji umeme
kwenye vijiji vya mikoa ya Njombe na Ruvuma.
Vilevile,
Kamati ilitembelea maeneo ya vijiji mbalimbali mkoani Njombe ambako
miradi ya umeme vijijini inatekelezwa kupitia Wakala wa Nishati Vijijini
(REA) Awamu ya Pili.
Aidha,
Kamati ilipata fursa kuzungumza na baadhi ya wananchi wa vijiji husika
ambako miradi hiyo ya umeme inatekelezwa na kusikiliza maoni yao.
Baada
ya ziara mkoani Njombe, Kamati hiyo itatembelea Mkoa wa Mbeya, eneo la
Kiwira katika Mradi wa Makaa ya Mawe na baadaye itaelekea Biharamulo
kukagua mgodi wa dhahabu wa Tulawaka.
Awali,
Kamati ilifanya ziara mkoani Mtwara ambapo ilitembelea Mtambo wa
kuchakata gesi asilia wa Madimba pamoja na Kiwanda cha kutengeneza
Saruji cha Dangote. Pia, Wajumbe wa Kamati hiyo walitembelea machimbo ya
Tanzanite yaliyopo Mirerani mkoani Manyara.
Mkandarasi
anayesambaza umeme vijijini kwa Mkoa wa Njombe, kutoka Kampuni ya Lucky
Exports Ltd (wa tatu kutoka kushoto), akimwonesha na kumpa maelezo
kuhusu transfoma iliyofungwa katika Kijiji cha Isindagosi – Njombe,
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Ussi
Pondeza, wakati wa ziara ya kamati hiyo mkoani humo hivi karibuni
kukagua miradi ya umeme vijijini.
Meneja
wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Njombe, Mhandisi
Emmanuel Kachewa (mwenye suti ya bluu-kushoto), akiwapa maelezo wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, kuhusu sehemu ya
kuchukulia umeme (taping point) iliyopo kijiji cha Italahumba – Njombe,
wakati wa ziara ya Kamati hiyo kukagua miradi ya umeme vijijini mkoani
humo hivi karibuni.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Njombe ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Anatory
Choya, akiwasilisha taarifa fupi ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo
ya Mkoa wake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini,
walipotembelea mkoani humo hivi karibuni kukagua utekelezwaji wa miradi
ya umeme vijijini.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini,
Profesa James Mdoe (wa pili kutoka kulia) akijadiliana jambo na Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anatory Choya (kulia), wakati wa ziara ya Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini (hawapo pichani), mkoani humo
hivi karibuni, kukagua utekelezwaji wa miradi ya umeme vijijini. Wa
kwanza kushoto ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje.
Mwananchi
kutoka Kijiji cha Ihanzutwa – Njombe, Karison Mgoba akitoa maoni yake
kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, kuhusu utekelezwaji
wa miradi ya umeme vijijini, hususan katika kijiji chake.
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wakiwa katika ziara
kukagua miradi ya umeme vijijini mkoani Njombe hivi karibuni.
Meneja
wa Mradi wa Ujenzi wa Njia ya Umeme wa Msongo wa Kilovolti 220 kutoka
Makambako hadi Songea, Mhandisi Didas Lyamuya, akiwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa mradi huo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na
Madini, wakati Wajumbe wa Kamati hiyo walipokuwa ofisini kwa Mkuu wa
Mkoa wa Njombe, kabla ya kutembelea miradi ya umeme vijijini
inayotekelezwa mkoani humo.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Ussi
Pondeza, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Isindagosi – Njombe
kuhusu miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa mkoani humo, wakati wa
ziara ya Kamati hiyo hivi karibuni. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Profesa James
Mdoe.
Mmoja
wa wananchi katika kijiji cha Isindagosi – Njombe, akitoa maoni yake
kuhusu utekelezwaji wa miradi ya umeme vijijini kwa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Nishati na Madini, wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara mkoani
humo hivi karibuni kutembelea miradi ya umeme vijijini.
Baadhi
ya Maafisa wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwaongoza Wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, kutembelea miradi ya
umeme vijijini inayotekelezwa mkoani Njombe hivi karibuni.