Na Matukiodaima Blog , Ludewa
WAKATI
wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) jimbo la Ludewa mkoani
Njombe kesho jumanne wanapiga kura za maoni ili kumpata mgombea wa
ubunge atakayezipa pengo lililoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa
jimbo hilo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita na na mgombea
ubunge marehemu Deo Filikunjombe ,wananchi wa jimbo hilo wameomba
wajumbe wa CCM kurudisha jina la mdogo wa marehemu Bw Philip
Filikunjombe ili akawatumikie bungeni.
Wakati
mchungaji wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKT) usharika
wa Ludewa mjini mchungaji Tafuteni Mwasonya akidai kuwa tayari Mungu
amekwisha wapatia wananchi wa Ludewa mbunge hivyo wagonje taratibu
za kidunia zifanyike.
Kwani
alisema anaetoa uongozi ni Mungu na kikubwa kwa wananchi wa Ludewa
wanapaswa kuomba kwa Mungu badala ya kusikiliza wanadamu na
kuongeza kuwa wanaemtaka ni yule ambae anaijua Ludewa vizuri na
mwenye kuwaletea maendeleo .
Wakizungumza na mtandao wa www.matukiodaima.co.tz
kwa nyakati tofauti wananchi hao walisema kuwa imani na
matumaini yao ni kuona wajumbe wa mkutano wa CCM wanamchagua Philip
Filikunjombe kuendeleza mipango mbali mbali ya kimaendeleo iliyoachwa
na marehemu Filikunjombe.
Kwani
wamesema kuwa Philip ambae alikuwa ni msaidizi na mratibu wa
mipango ya jimbo hilo wakati wa uhai wa kakake Filikunjombe
wanaimani kuwa ataweza kuwatumikia vema kama ilivyokuwa kwa kaka
yake hivyo ili kuweza kuwafuta machozi yao juu ya maendeleo ya jimbo
hilo wanaomba jina la Philip kuweza kuchaguliwa .
John
Haule mkazi wa Mavanga akiungumza kwa niaba ya wananchi wenzake
alisema kuwa ni wagombea zaidi ya watano wamejitokeza ila kwa
wote hao bado wao kama wananchi wa jimbo hilo ambae wanaona
anaweza kuwatumikia ni Filikunjombe .
"
Tunaomba sana kama ingekuwa ni wananchi tunaamua ni nani awe
mbunge wetu basi tusingehitaji kupiga kura za maoni kwa kauli moja
tungempa Philip Filikunjombe .....ila kwa kuwa ni taratibu ndani ya
CCM na sehemu ya Demkrasia basi tunalazimika kuzama katika maombi
kuona azma yetu inatimia kwa kumpata yule tulie mtegemea baada ya
kifo cha kipenzi chetu Deo"
Jumla
ya makada 10 wa CCM waliochukua na kurejesha fomu na wanataraji
kuchujwa katika mchakato huo wa ndani ya CCM ili kumpata mmoja
atakapambana na mgombea wa Chadema mbali ya Philip Filikunjombe
wengione ni Edgar Lugome.Johnson Mgimba,Emmauel Mgaya, James Mgaya,
Jackob Mpangala, Saimon Ngatunga, Evaristo Mtitu, , Deo Ngalawa na
Zephania Chaula,
Kwa
upande wake Bw Philip akielezea vipaumbele vyake iwapo
atachaguliwa katika mchakato huo wa kura za maoni ndani ya chama na
wananchi kumchagua kuwa mbunge wao kwanza ni kuendelea mipango yote
iliyoachwa na marehemu ambayo mipango mingi anaitambua na kuwa suala
la nidhamu na uwajibikaji katika kazi kwake litakuwa ni msingi wa
kweli wa kuwaletea wana Ludewa maendeleo .
Alisema
Ludewa mbali ya kumpoteza mbunge wao bado wanayonafasi ya kuamua na
kumchagua ili kuendeleza yote mazuri kwa ajili ya maendeleo yao na
kuona kasi ya maendeleo katika wilaya hiyo inaendelea kukua kwa kasi
na kuwaomba wana CCM kumwamini kwani hata waangusha na kuwa anachoomba
wana CCM kumkopesha kura zao za ndio ili ndani ya miaka mitano awe
kuwalipa maendeleo .
ELIMU
wakili
wa mahakama kuu, mtafiti shahada uzamivu, katika sharia (PHD) Chuo
Kikuu huria cha Tanzania , Shahada ya uzamili katika sharia (LLM), Chuo
kikuu cha Stratchclyde, Uingereza, Diploma ya juu ya Mafunzo ya sheria
kwa vitendo, Chuo cha Mafunzo ya Uwakili Tanzania, Dar es Salaam 2012,
Stashada ya sheria (LLB), 2007 Chcha Tumaini Iringa, Cheti cha Lugha ya
Kifaransa. Chuo kikuu cha Blida, Algeria 2004, Cheti cha Uandishi wa
Habari, Dar es Salaam School of Journalism 2003.
Elimu
ya kidato cha sita, shule ya sekondari Mzumbe 2002, Elimu ya Sekondari,
Njombe Sekondari 1999, Elimu ya Msingi, Shule ya msingi Ludewa mjini
1995.
UZOEFU WA KAZI.
mwanasheria
mwandamizi, Mamlaka ya ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) 2012 mpaka sasa,
Mkufunzi wa sheriaKikuu Huria cha Tanzania, 2010-2012, Mkufunzi wa
Sheria, Chuo kikuu cha Matakatifu Augustino 2010-2912, Mkufunzi wa
Sheria Chuo kikuu Tumaini Iringa 2007-2010.
UJASILIAMALI NA BIASHARA BINAFSI.
Mkurugenzi
na mmiliki wa Kampuni ya uwakili wa Reliance Legal Consultants, Dar es
Salaam, Mkurugeni mmiliki wa kampuni ya usafiri ya Matatu Logistics, Dar
es Salaam na Mkurugenzi na mdau wa Kampuni ya Jumbo Camera House, Dar
es Salaam.