Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa Bw Stanley Kolimba akiweka shada la maua katika kaburi ya mwenyekiti wa DP mchungaji Mtikila leo
Viongozi wa kitaifa wa DP na mkoa wa Iringa na Njombe wakiwa katika kaburi la Mtikila
Mmiliki wa mtandao huu wa matukiodaima Bw Francis Godwin wa pili kushoto akimhoji Live kupitia radio Country Fm naibu katibu mkuu wa DP Taifa Bw Abduli Mluya juu ya kifo cha Mtikila
Wananchi wa kijiji cha Milo Ludewa wakitazama Chopa aliyotumia Deo Filikunjombe kufika msibani hapo leo |
ACT Wazalendo na DP waungana katika msiba wa Mtikila |
Mwenyekiti wa DP mkoa wa Iringa na mgombea ubunge jimbola Iringa mjini Robart Kisinini kushoto akiungana kubeba jeneza lenye mwili wa Mtikila |
mkuu wa mkoa wa Njombe Dr Rehema Nchimbi kulia akiwa na Deo Filikunjombe mgombea ubunge jimbo la Ludewa na mbunge aliyemaliza muda wake katikati kushoto ni msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi leo wakati wa mazishi ya Mchungaji Mtikila
Mchungaji Patrick Mgaya aliyekuwa safari moja na marehemu Mtikila wa pili kulia akiwa katika mazishi hayo
Waombolezaji wakiwa msibani
Filikunjombe akitoa salamu zake wakati wa mazishi ya Mtikila
Wananchi wakimsikiliza Filikunjombe
Filikunjombea akitoa mkono wa pole kwa wafiwa katikaati ni mjane Bi Jojina Mtikila
Filikunjombe akiwasili msibani kwa chopa
Jaji Francis Mutungi kushoto Bw MGaya na Askofu Mtetemela na Filikunjombe wakiwa msibani
Filikunjombe akijiandaa kubeba jeneza
Mjane wa Mtikila akiweka shada la maua
Na MatukiodaimaBlog
MWENYEKITI wa chama cha DP mchungaji Christopher Mtikila azikwa kijijini kwake Milo Wilaya ya Ludewa
mkoani Njombe vilio vyatawala aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ludewa Deo
Filikunjombe na Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi
watao ya Moyoni wasema alikuwa kiungo mhimu katika Taifa .
Wakati Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Mutungi akiwataka
watanzania hasa viongozi wa vyama vya siasa kumuenzi Mchungaji Mtikila
kwa kuenzi Amani wakati huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu octoba 25
mwaka huu ,Filikunjombe asema mbali ya ukorofi wa Mtikila kwa kile
alichokiamini ila kwake alikuwa ni mshauri mkubwa wa Ubunge wake katika
jimbo la Ludewa.
Wakitoa salamu za rambi rambi wakati wa mazishi hayo
yaliyofanyika leo kijijini kwake Milo Wilaya ya Ludewa ,Jaji Ntungi
alisema kuwa katika Enzi zake marehemu Mtikila alikuwa akisimamia kile
anachokiamini.
Alisema kuwa mbali ya misimamo yake
ya kusimamia alichokiamini bado alikuwa ni mtu wa kujenga hoja na ambae
hakupenda kuhatarisha Amani ya nchi hakuwa anapenda njia za mkato
katika kupata majibu ya kile asichokiamini.
" Njia za mkato marehemu hakupenda kabisa kwani hata Kama jambo la
kutisha ambalo wengine huogopa yeye alikuwa tayari kwenda mahakamani
kusaka Haki yake bila kuhatarisha Amani ya nchi Mimi nafikiri kila mmoja
akafuata misingi yake katika kudai Haki bila kuvuruga amani naamini
tutafanikiwa
"
Alisema kuwa kuna mapungufu yanaweza kujitokeza ila Jambo la msingi kila
mmoja kutanguliza kwanza amani ya nchi badala kuipa kisogo Amani na
kupenda machafuko katika nchi"
Hivyo aliwataka watanzania bila kujali
itikadi zao za vyama kuendelea na siasa huku wakitanguliza Amani ya nchi.
Mbunge aliyemaliza muda wake wa jimbo la Ludewa ambae ni mgombea Ubunge
wa jimbo hilo Bw Filikunjombe alisema kuwa pamoja na Mchungaji Mtikila enzi za uhai wake alisimamia jambo ambalo
alikuwa akiamini ila
kwake amekuwa msaada mkubwa katika ushauri wa kuwatumikia wananchi wa
Ludewa .
Alisema Mchungaji Mtikila hakuwa tayari kumuunga mkono mbunge wa Ludewa
ambae hakuwa msaada wa kimaendeleo kwa wananchi ila kwa upande wake
alikuwa akimuunga mkono na hata kutosimamisha mgombea katika jimbo la
Ludewa.
"
Mchungaji Mtikila hakuwa tayari kuungana na mbunge asiyefanya Kazi za
maendeleo jimboni Ludewa ila kwangu alikuwa akiniunga mkono na hata
kunipingeza kwa Kazi nzuri ..... Kicho chake ni pigo kubwa kwa Taifa
hasa kwa wana Ludewa ambao tulijivunia sana uwepo wake"
Hata hivyo
alisema njia pekee kwake ya kumuenzi Mchungaji Mtikila ni kuendelea
kuwatumikia vema wananchi wa Ludewa kwa kuleta maendeleo zaidi Kama
alivyohitaji katika uhai wake.
Filikunjombe alisema katika kuamini kwake na kusimamia anachokiamini
hadi mauti inamkuta alikuwa akitetea kuwepo kwa nchi ya Tanganyika na
ndio maana kazikwa na bendera ya Tanganyika na kudai kuwa hakuna na kosa
kupigania Tanganyika kwani Tanganyika inahitajika.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr Rerema Nchimbi alisema kuwa Mkoa wa Njombe
umepoteza kiongozi makini na kuwa katika kumuenzi ni vema kwa vyama vya
siasa kuendesha kampeni za amani na utulivu zaidi na kuwa wakati taifa
linaelekea katika uchaguzi mkuu ni vema kila chama kumuenzi Mtikila kwa
kulinda Amani .
Naibu Katibu mkuu wa DP Taifa Abdul
Mluya alisema kuwa suala la kifo cha mwenyekiti wake ni utata mtupu na
bado wanaendelea kuchunguza.
Wakati
huo
huo Chopa ya Filikunjombe aliyotumia kufaria kwenda katika mazishi hayo
iliwafanya wananchi kuacha kusikiliza Salam mbali mbali za viongozi na
kukimbilia kutazama na kumlaki Mgombea huyo Ubunge jimbo la Ludewa.
0 comments:
Post a Comment