Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu
wa Mkoa wa Njombe Mh. Dk. Rehema Nchimbi akifungua kikao kazi cha
biashara ya kilimo kwa kongani ya Ihemi iliyoandaliwa na SAGCOT
(Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania) kwa ushirikiano na
UONGOZI Institute (Taasisi ya Uongozi Afrika kwa Maendeleo Endelevu)
mapema leo Iringa mjini. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Kilimo wa TCCIA Bi. Magadalena Mkocha, Mwenyikiti wa Bodi ya
Agricultural Council of Tanzania Dk. Sinare Y. Sinare, DC wa Iringa Mh.
Angeline Mabula, DC wa Mufindi Mh. Mboni Mhita na Katibu Mkuu Kiongozi
mstaafu Philemon Luhanjo.
Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Philemon Luhanjo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa bodi ya UONGOZI
Institute akitoa salaam kwa niaba ya taasisi hiyo wakati wa ufunguzi wa
kikao kazi cha biashara ya kilimo kwa kongani ya Ihemi inayoendelea
Iringa mjini. UONGOZI Institute imeshiriki katika kuwezesha kikao kazi hicho.
Mkurugenzi
Mtendaji wa SAGCOT Bw. Geoffrey Kirenga akitoa utangulizi wa mada ya
biashara ya kilimo kwa nyanda za juu kusini. Mkutano huu wa siku mbili
unakutanisha viongozi wa serikalini, sekta binafsi, mashirika ya
kimataifa pamoja na wakulima kwa ajili ya kujadili kuhusu kuboresha
biashara ya kilimo nchini kwa nyanda za juu kusini.
Picha
ya pamoja ya wageni waalikwa na washiriki wa kikao kazi cha biashara ya
kilimo inayoendelea Iringa mjini. Mada zinazojadiliwa ni pamoja na
wajibu wa viongozi katika kuleta mageuzi katika kilimo.
0 comments:
Post a Comment