Chama
cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini 'Tanzania Bloggers
Network' - TBN kinapenda kuwajulisha wanaotaka kujiunga na chama hicho kuwa
fomu za kujiunga zinatolewa. Wahusika ni wamiliki na waendeshaji wote wa
mitandao ya kijamii (blogs na forums) Tanzania na Watanzania wanaofanya kazi
kama hiyo nje ya nchi.
Sifa
kuu kwa mwanachama ni kuwa na blog ambayo ina umri wa miezi sita tangu ianze
kuendeshwa mfululizo. Kwa wa kazi wa Dar es Salaam wenye sifa ambao wanataka
kujiunga fomu hizo zinapatikana kwenye Ofisi za Muda za Tanzania Bloggers
Network (TBN) kwenye Jengo la Dar Free Market lililopo mkabala na Barabara ya
Ally Hassan Mwinyi.
Mwanachama
muitaji wa kujiunga kabla ya fomu atatakiwa kutoa shs 25,000/- ikiwa ni
Kiingilio cha mwanachama, shs 15,000/- yakiwa ni malipo ya ada ya miezi mitatu
kwa mwanachama na shs 10,000/- ikiwa ni malipo ya kadi ya TBN kwa mwanachama
(utambulisho). Jumla kuu kila mwanachama anatakiwa kulipa shs 50,000/- na
kupewa risiti halali ya malipo ya TBN.
Fomu
zitatolewa siku za kazi kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni. Zoezi la
utoaji fomu litasimamiwa na Mweka Hazina wa TBN, Shamim Mwasha (0767418941).
Fomu pia zinapatikana Ofisi za Michuzi Media, mjini Jengo refu karibu na
Hospitali ya Ocean Road ghorofa ya pili.
Kwa
wanachama wa mikoani utaratibu unafanywa namna ya kusambaza fomu hizo mara moja
na wanachama watalipa moja kwa moja benki ya NMB kwenye akaunti ya TBN.
Utaratibu unafanywa kupata viongozi wa kanda wa muda watakaoratibu usajili kwa
kushirikiana na viongozi wa muda wa TBN taifa. Viongozi wa muda wa mikoa na
kanda watapewa maelekezo namna ya kusimamia na kuratibu zoezi la kujiunga
uwanachama wa TBN.
Mikoani TBN itagawanyika kwa kanda, yaani Kanda ya Pwani (ikijumuisha mikoa ya Tanga na Pwani yenyewe), Kanda ya Zanzibar (ikijumuisha Unguja na Pemba), Kanda ya Dar es salaam, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (inayojumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Rukwa, Simiyu), Kanda ya Kusini (jumuisha mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma), Kanda ya Kati (mikoa ya Dodoma, Tabora, Morogoro na Singida), Kanda ya Magharibi (inayojumuisha mikoa ya Kigoma na Rukwa), Kanda ya Ziwa (yenye mikoa ya Kagera, Geita, Mara na Mwanza), na Kanda ya Kaskazini (inayojumisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara).
Kwa
wahitaji unaombwa kuchukua fomu yako mapema kwani usajili wa wanachama wa TBN
utafanyika kwa muda wa wiki tatu kisha zoezi hili litafungwa ili kutoa fursa
kwa viongozi na kamati husika kutathmini wanachama waliopatikana na
litafunguliwa tena baada ya miezi sita.
NB;- Kwa watakaohitaji katiba ya TBN watapewa pia ofisini coppy, lakini coppy hiyo ataigharamia wenyewe. Utaratibu unafanywa wa kuichapa kwenye soft coppy na zitatumwa mikoani kwa gharama za TBN.
NB;- Kwa watakaohitaji katiba ya TBN watapewa pia ofisini coppy, lakini coppy hiyo ataigharamia wenyewe. Utaratibu unafanywa wa kuichapa kwenye soft coppy na zitatumwa mikoani kwa gharama za TBN.
Imetolewa na:
Joachim Mushi, 0756469470
Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN)
Joachim Mushi, 0756469470
Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN)
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment