Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WATENDAJI wa Wilaya za Mkoa wa Njombe, wametakiwa kutumia fursa ya
uwepo wa Baraza la Biashara la Mkoa kuunganisha sekta ya umma na binafsi
kujadili kutatua changamoto zilizopo katika biashara na kutumia fursa
hiyo kutangaza vivutio vya biashara zilivyopo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza hilo, Mkurugenzi wa Biashara
wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC), Arthur Mtafya, alisema wajumbe
wa baraza hilo hawana budi kuzingatia fursa za uchumi zilizo katika mkoa
huo na kujadiliana juu ya vikwazo vya biashara, ili kupanua wigo wa
uwekezaji mkoani humo.
“Nia ya kuanzisha baraza katika ngazi ya mkoa na wilaya ni kurahisisha
utendaji kutoka ngazi ya taifa mpaka wilayani, kwani kuna mambo
yanayoweza kushughulikiwa katika ngazi ya mkoa,” alisema.
Mtafya alisema sera za nchi zinaruhusu baadhi ya changamoto zinazohusu
mkoa fulani zitatuliwe katika ngazi ya mkoa na kwamba hiyo inasaidia
utendaji na uwajibikaji na kuwa yanaposhindikana ndipo huwasilishwa
katika ngazi ya taifa, ili kufanyiwa kazi. Alisema ushiriki kamilifu wa
sekta hizo mbili katika ngazi ya mkoa na wilaya utasaidia kwa kiwango
kikubwa katika kuinua hali ya biashara na uwekezaji katika mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Kapteni Mstaafu Asei Msangi, alisema baraza
hilo jipya litakuwa chachu ya maendeleo kwa kuunganisha sekta ya umma na
binafsi katika kujadili vikwazo vya biashara, ili kukuza uchumi wa mkoa
huo na taifa kwa ujumla.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment