Home » » KATIBU MKUU WA CCM ABDURAHMAN KINANA AWASILI

KATIBU MKUU WA CCM ABDURAHMAN KINANA AWASILI

 

 
2
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana ukiwasili mpakani mwa mikoa ya njombe na Iringa katika kijiji cha Idofi ambapo alikopkelewa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Njombe akitokea mkoani Iringa ambako aliwasili leo asubuhi akitokea jijini Dar es salaam akiongozana na Katibu wa Itikadi Siasa na Uenezi ndugu Nape Mosses Nnauye, Ndugu Kinana na ujumbe wake watakuwa ni ziara ya siku saba mknoani Njombe ambapo watatembelea wilaya za Njombe, Makete na Ludewa na Wanging’ombe wakiimarisha chama na kusikiliza matatizo ya wananchi, huku wakikagua miradi ya maendeleo katika kusimiamia serikali ili kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM 3Katibu Mkuu wa CCM akiwasili mpakani mwa mikoa ya Iringa na Njombe akitokea mjini Iringa 5Katibu Mkuu wa CCM akivishwa skafu na chipukizi wa mkoa wa Njombe 7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Ludewa Ndugu Deo Filikunjombe 8Ndugu Abdurahman Kinana akifurahia jambo na Deo Sanga Jah People Mbunge wa Njombe Kaskazini kulia ni Mbunge wa Mwibara Kange Rugora. 9Mjumbe wa Kamati Kuu na mbunge wa viti Maalum Mkoawa Njombe Pindi Chana akicheza na akina mama wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana 10Abdurahman Kinana akifurahia ngoza iliyokuwa ikitumbuizwa na kikundi cha ngoma cha mkoani Njombe huku Nape Nnauye akipiga ngoma 12
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akizungumza na wananchi wa mkoa wa Njombe mara baada ya kuwasili mpakani mwa mikoa hiyo katika kijiji cha Idofi.
1
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika mapokeizi hayo
13
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akiwa katika kikao cha kamatiya siasa mkoani Njombe kulia ni Deo Sanga Jah People Mbunge wa Njombe Kaskazini na kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa Itikadi Siasa na Uenezi 14Baadhi ya wajumbe wa kaqmati ya siasa mkoa wa njombe wakiwa katika mkutano huo. 15
Baadhi ya wajumbe wa kaqmati ya siasa mkoa wa njombe wakiwa katika mkutano huo.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa