
NJOMBE – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, tarehe 24 Machi,2025 alifanya ziara mkoani Njombe ambapo, aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, alitembelea Kiwanda cha Muricado Fruit Supplies kujionea uwekezaji mkubwa unaofanyika katika kuongeza thamani ya zao la parachichi.Akizungumza baada ya kutembelea kiwanda hicho, Mhe. Prof. Mkumbo alimpongeza muwekezaji kwa juhudi zake katika kukuza sekta ya viwanda na kilimo. "Huu ni uwekezaji wenye tija kwa wakulima wa parachichi na uchumi wa taifa kwa ujumla. Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wa ndani ili kuhakikisha viwanda vya...