Home » » WAKAZI MAKETE WATAKIWA KUIUNGA MKONO SRIKALI.

WAKAZI MAKETE WATAKIWA KUIUNGA MKONO SRIKALI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKUU wa Wilaya ya Makete mkoani Njombe, Daud Yassin amewaambia wananchi wa wilaya hiyo kwamba Uchaguzi Mkuu umekwisha na sasa kilichobaki ni wananchi na viongozi wa ngazi zote kuiunga mkono kwa dhati Serikali inayotekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), chini ya Rais John Magufuli.
Yassin alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na wananchi katika Kata ya Iwawa wilayani humo na kuwataka kumpa ushirikiano kwa pamoja, ili kutekeleza ilani hiyo pamoja na kuijenga Makete yao.
“Uchaguzi Mkuu umekwisha na sasa kilichobaki ni kwetu sote kuiunga mkono Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli ili kutekeleza ilani yake, kusaidiana naye katika kutimiza yote aliyoyaahidi kuwafanyia Watanzania,” alieleza.
Alisema hadi sasa Rais Magufuli ameonesha moyo wa dhati wa kuwatumikia wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vyao, hivyo anahitaji kuungwa mkono na wana Makete ili maendeleo yaweze kupatikana.
“Kinachotakiwa kwa sasa ni kuungana kwa pamoja na kushirikiana ili wilaya yetu izidi kusonga mbele,” alieleza na kuongeza kuwa milango ipo wazi kwa yeyote mwenye ushauri au maoni, ama mwenye kero yoyote afike ofisini kwake na atasikilizwa.
 CHANZO ; HABARI LEO.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa