HII NAYO NOMA: KIJANA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUFANYA MAPENZI NA NGURUWE WILAYANI LUDEWA, SOMA HAPA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Kijana mmoja aitwaye Simon Dustan Mwanjavala maarufu kama Mwachakala (15) mkazi wa kijiji cha Mbwila kata ya Luana wilaya ya Ludewa mkoani Njombe amefariki dunia muda mchache baada ya kukutwa akifanya mapenzi na Nguruwe.

Tukio hilo la kustaajabisha limetokea leo wilayani Ludewa baada ya kijana huyo "kufumaniwa" akifanya mapenzi na mnyama huyo, ndipo walipomkamata na kumfunga kamba mikono yake na miguu ili asikimbie.

Baada ya majirani kumuona kijana huyo akimbaka nguruwe huyo kwenye banda la mnyama huyo walikwenda kumwambia baba yake mdogo ambao kwa pamoja walimkamata kijana huyo, ambaye alikiri kufanya kosa hilo.
Alipoulizwa sababu zilizomfanya kufanya mapenzi na nguruwe, alisema alikuwa na hamu ya kufanya tendo hilo.

Kutokana na kitendo hicho waliamua kumvua nguo zote na kumfunga kamba na kumpa kichapo  kisha wakamuacha kwa muda kwenye eneo la tukio, na walipokuja kumfungua kamba na mwenyekiti wa kijiji hicho, alidondoka na kufariki dunia papo hapo.
Chanzo Kijukuu cha Bibi K blog

PHILIP FILIKUNJOMBE AOMBEWA USHINDI KURA ZA MAONI UBUNGE LUDEWA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 
Na Matukiodaima Blog , Ludewa
WAKATI wanachama wa  chama  cha mapinduzi (CCM)  jimbo la  Ludewa mkoani  Njombe  kesho jumanne wanapiga kura za maoni  ili  kumpata mgombea wa  ubunge atakayezipa pengo  lililoachwa  wazi na aliyekuwa mbunge wa  jimbo  hilo kwa  kipindi  cha miaka  mitano iliyopita na na mgombea  ubunge marehemu Deo Filikunjombe  ,wananchi wa  jimbo  hilo wameomba wajumbe wa CCM kurudisha  jina la mdogo wa marehemu Bw Philip Filikunjombe ili akawatumikie bungeni.

Wakati  mchungaji  wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKT) usharika  wa  Ludewa mjini mchungaji Tafuteni Mwasonya akidai  kuwa tayari Mungu amekwisha wapatia  wananchi  wa Ludewa mbunge hivyo wagonje taratibu  za  kidunia  zifanyike.

Kwani  alisema anaetoa   uongozi ni  Mungu na  kikubwa kwa  wananchi wa Ludewa wanapaswa kuomba kwa Mungu badala  ya kusikiliza  wanadamu na  kuongeza  kuwa wanaemtaka ni yule ambae anaijua  Ludewa  vizuri na mwenye  kuwaletea maendeleo .

Wakizungumza na mtandao  wa  www.matukiodaima.co.tz  kwa  nyakati  tofauti    wananchi hao   walisema  kuwa imani na matumaini  yao ni  kuona  wajumbe wa mkutano wa CCM wanamchagua  Philip Filikunjombe kuendeleza  mipango  mbali mbali ya kimaendeleo iliyoachwa na marehemu Filikunjombe.

Kwani  wamesema  kuwa Philip ambae  alikuwa ni msaidizi  na mratibu  wa mipango  ya  jimbo  hilo wakati  wa uhai  wa kakake Filikunjombe  wanaimani  kuwa ataweza kuwatumikia  vema kama  ilivyokuwa kwa kaka  yake hivyo ili  kuweza kuwafuta machozi  yao  juu ya maendeleo ya jimbo  hilo wanaomba  jina la Philip  kuweza kuchaguliwa .

John Haule  mkazi  wa Mavanga akiungumza kwa niaba ya wananchi wenzake  alisema  kuwa ni  wagombea   zaidi ya  watano  wamejitokeza  ila kwa wote  hao  bado  wao kama  wananchi  wa jimbo  hilo ambae wanaona anaweza  kuwatumikia ni Filikunjombe .

" Tunaomba  sana kama  ingekuwa ni  wananchi  tunaamua  ni nani awe mbunge  wetu  basi tusingehitaji kupiga kura   za maoni kwa  kauli  moja tungempa Philip Filikunjombe .....ila kwa  kuwa ni taratibu  ndani ya  CCM na sehemu ya  Demkrasia basi tunalazimika  kuzama  katika maombi  kuona azma yetu  inatimia kwa  kumpata  yule  tulie mtegemea  baada ya kifo  cha  kipenzi  chetu Deo"
Jumla ya  makada  10 wa CCM waliochukua na kurejesha fomu na wanataraji  kuchujwa  katika mchakato   huo  wa ndani ya CCM ili  kumpata  mmoja atakapambana na  mgombea wa Chadema mbali ya Philip Filikunjombe wengione ni   Edgar Lugome.Johnson Mgimba,Emmauel Mgaya, James Mgaya,  Jackob Mpangala, Saimon Ngatunga, Evaristo Mtitu, , Deo Ngalawa na Zephania Chaula,

Kwa upande  wake Bw  Philip  akielezea vipaumbele  vyake  iwapo  atachaguliwa katika  mchakato  huo wa  kura za maoni ndani ya chama  na wananchi  kumchagua  kuwa mbunge wao  kwanza ni  kuendelea mipango yote  iliyoachwa na marehemu ambayo mipango  mingi anaitambua  na  kuwa suala la nidhamu na uwajibikaji  katika kazi kwake  litakuwa ni msingi  wa  kweli  wa kuwaletea wana Ludewa maendeleo .

Alisema Ludewa mbali ya kumpoteza mbunge  wao bado wanayonafasi ya kuamua  na  kumchagua  ili  kuendeleza yote mazuri  kwa ajili ya maendeleo yao  na  kuona kasi ya maendeleo katika wilaya   hiyo inaendelea  kukua kwa kasi na kuwaomba  wana CCM kumwamini kwani hata waangusha na kuwa anachoomba wana CCM kumkopesha  kura  zao za ndio ili  ndani ya  miaka mitano awe  kuwalipa maendeleo .
ELIMU
wakili wa mahakama kuu, mtafiti shahada uzamivu, katika sharia (PHD) Chuo Kikuu huria cha Tanzania , Shahada ya uzamili katika sharia (LLM), Chuo kikuu cha Stratchclyde, Uingereza,  Diploma ya juu ya Mafunzo ya sheria kwa vitendo, Chuo cha Mafunzo ya Uwakili Tanzania, Dar es Salaam 2012, Stashada ya sheria (LLB), 2007 Chcha Tumaini Iringa, Cheti cha Lugha ya Kifaransa. Chuo kikuu cha Blida, Algeria 2004, Cheti cha Uandishi wa Habari, Dar es Salaam School of Journalism 2003.

Elimu ya kidato cha sita, shule ya sekondari Mzumbe 2002, Elimu ya Sekondari, Njombe Sekondari 1999, Elimu ya Msingi, Shule ya msingi Ludewa mjini 1995.

UZOEFU WA KAZI.
mwanasheria mwandamizi, Mamlaka ya ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) 2012 mpaka sasa, Mkufunzi wa sheriaKikuu Huria cha Tanzania, 2010-2012, Mkufunzi wa Sheria, Chuo kikuu cha Matakatifu Augustino 2010-2912, Mkufunzi wa Sheria Chuo kikuu  Tumaini Iringa 2007-2010.

UJASILIAMALI NA BIASHARA BINAFSI.
Mkurugenzi na mmiliki wa Kampuni ya uwakili wa Reliance Legal Consultants, Dar es Salaam, Mkurugeni mmiliki wa kampuni ya usafiri ya Matatu Logistics, Dar es Salaam na Mkurugenzi na mdau wa Kampuni ya Jumbo Camera House, Dar es Salaam.


  Deo  Filikunjombe pamoja na watu  wengine watatu alifariki kwa ajali  ya  Chopa katika  hifadhi  ya Selou akitokea  jijini Dar es Salaam  kuelekea jimboni Ludewa mnamo Octoba 15  mwaka 2015
 
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa