ERIC SHIGONGO: NENDA KAMANDA WANGU DEO‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

chopa
Aliyekuwa Mbunge wa Ludewa kwa tiketi ya CCM, Deogratias Filikunjombe, enzi za uhai wake akipanda chopa yake.
Nakupenda Deo
Nimesikitishwa sana na kifo chako. Kweli kifo kipo na kila mmoja wetu atakipitia lakini cha aina hii, cha kijana aliyekuwa akipigania watu wake kiasi hiki? Kinaumiza sana, hata hivyo, hatuna budi zaidi ya kukubali kuwa Deo Filikunjombe, jembe la mkono limeondoka.
chopa 2
Chopa iliyosababsha kifo cha Filikunjombe, Capt. William Silaa na watu wengine wawili.
Nasema kutoka ndani ya moyo wangu, taifa limepoteza mtu muhimu sana, hakusita kupigania alichokiamini bila uoga wala hofu! Wakati mwingine alitofautiana na msimamo wa chama chake kwa maslahi ya Watanzania maskini, kwako ukweli ulikuwa nguzo. Nenda Deo, nenda kapumzike muda si mrefu tutaungana nawe, kila mwanadamu atafariki dunia maana ndivyo ilivyoandikwa.
Lakini cha muhimu ni mtu atakuwa anafanya nini wakati anakufa! Je, atakuwa akiiba au akifanya uzinzi? Deo umekufa ukitumikia watu wako, umekufa kifo chema na Wanaludewa watakuombea. Nenda Deo, pumzika Deo, mema yako yamekutangulia.
Hayo ndyo yatakutetea mbele ya Maulana! Mwisho nasema kwa uchungu na ninakuahidi, pale ulipoishia, sisi tutaendelea bila kujali tupata nini mpaka siku moja wananchi wa taifa hili wafaidi mema ya nchi yao.
Nenda Deo, kapumzike kwa amani, umekufa katika mapambano. Natoa pole kwa familia yako, mkeo, watoto, wazazi na wananchi wote wa Jimbo la Ludewa, msiumie sana, Mungu anajua ni kwa nini ameamua jambo hili litokee. Naamini Deo yuko mahali sahihi, kutokana na kile alichokuwa akikifanya wakati anakutwa na mauti, kwetu sisi, kibinadamu ni maumivu lakini kiimani, Deo yuko mahali salama. Nenda kaka Deo. Pumzika kwa amani kaka!
Eric James Shigongo,
Mkurugenzi, Global Publishers Ltd.
Nenda kamanda wangu Deo

MCHUNGAJI MTIKILA AZIKWA ,FILIKUNJOMBE JAJI MUTUNGI WATOA YA MOYONI HELKOPTA YA FILIKUNJOMBE YAWA KIVUTIO‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Mwenyekiti  wa CCM wilaya ya  Ludewa Bw Stanley Kolimba  akiweka shada la maua katika kaburi ya mwenyekiti wa DP mchungaji Mtikila leo
 Viongozi  wa kitaifa wa DP na  mkoa wa Iringa na Njombe wakiwa katika kaburi la Mtikila
 Mmiliki wa mtandao huu wa matukiodaima Bw Francis Godwin  wa pili kushoto akimhoji Live kupitia radio Country Fm naibu katibu mkuu wa DP Taifa Bw Abduli Mluya juu ya kifo cha Mtikila 
Wananchi  wa kijiji cha Milo Ludewa wakitazama Chopa aliyotumia Deo Filikunjombe kufika msibani hapo leo
ACT Wazalendo na DP  waungana katika msiba wa Mtikila
Mwenyekiti wa DP mkoa wa Iringa na mgombea ubunge jimbola Iringa mjini Robart Kisinini kushoto akiungana  kubeba jeneza lenye mwili wa Mtikila
 mkuu  wa mkoa wa Njombe Dr Rehema Nchimbi kulia akiwa na Deo Filikunjombe mgombea  ubunge jimbo la Ludewa na mbunge aliyemaliza muda  wake katikati kushoto ni msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi leo  wakati wa mazishi ya Mchungaji Mtikila
 Mchungaji Patrick Mgaya aliyekuwa  safari moja na marehemu Mtikila wa pili kulia akiwa katika mazishi hayo
 Waombolezaji wakiwa msibani

 Filikunjombe akitoa salamu zake wakati wa mazishi ya Mtikila
 Wananchi wakimsikiliza Filikunjombe



 Filikunjombea akitoa mkono wa pole  kwa wafiwa  katikaati ni mjane Bi Jojina Mtikila

 Filikunjombe akiwasili msibani kwa chopa

 Jaji Francis Mutungi kushoto Bw MGaya na Askofu Mtetemela na Filikunjombe wakiwa msibani
 Filikunjombe akijiandaa kubeba jeneza

 Mjane  wa Mtikila  akiweka shada la maua

 Na MatukiodaimaBlog
MWENYEKITI wa chama cha DP mchungaji Christopher Mtikila azikwa kijijini kwake Milo Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe vilio vyatawala aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi  watao ya Moyoni wasema alikuwa kiungo mhimu katika Taifa .

Wakati Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji  Mutungi  akiwataka watanzania hasa viongozi wa vyama vya siasa kumuenzi Mchungaji Mtikila kwa kuenzi Amani wakati huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu octoba 25 mwaka huu ,Filikunjombe asema mbali ya ukorofi wa Mtikila kwa kile alichokiamini ila kwake alikuwa ni mshauri mkubwa wa Ubunge wake katika jimbo la Ludewa.

Wakitoa salamu za rambi rambi wakati wa mazishi hayo yaliyofanyika leo  kijijini kwake Milo Wilaya ya Ludewa ,Jaji Ntungi alisema kuwa katika Enzi zake marehemu Mtikila alikuwa akisimamia kile anachokiamini.

Alisema kuwa mbali ya misimamo yake ya kusimamia alichokiamini bado alikuwa ni mtu wa kujenga hoja na ambae hakupenda kuhatarisha Amani ya nchi hakuwa anapenda njia za mkato katika kupata majibu ya kile asichokiamini.

" Njia za mkato marehemu hakupenda kabisa kwani hata Kama jambo la kutisha ambalo wengine huogopa yeye alikuwa tayari kwenda mahakamani kusaka Haki yake bila kuhatarisha Amani ya nchi Mimi nafikiri kila mmoja akafuata misingi yake katika kudai Haki bila kuvuruga amani naamini tutafanikiwa

" Alisema kuwa kuna mapungufu yanaweza kujitokeza ila Jambo la msingi kila mmoja kutanguliza kwanza amani ya nchi badala kuipa kisogo Amani na kupenda machafuko katika nchi"

Hivyo aliwataka watanzania bila kujali itikadi zao za vyama kuendelea na siasa huku wakitanguliza Amani ya nchi.

Mbunge aliyemaliza muda wake wa jimbo la Ludewa ambae ni mgombea Ubunge wa jimbo hilo Bw Filikunjombe alisema kuwa pamoja na Mchungaji Mtikila enzi za uhai wake alisimamia jambo ambalo
alikuwa akiamini ila kwake amekuwa msaada mkubwa katika ushauri wa kuwatumikia wananchi wa Ludewa .
Alisema Mchungaji Mtikila hakuwa tayari kumuunga mkono mbunge wa Ludewa ambae hakuwa msaada wa kimaendeleo kwa wananchi ila kwa upande wake alikuwa akimuunga mkono na hata kutosimamisha mgombea katika jimbo la Ludewa.

" Mchungaji Mtikila hakuwa tayari kuungana na mbunge asiyefanya Kazi za maendeleo jimboni Ludewa ila kwangu alikuwa akiniunga mkono na hata kunipingeza kwa Kazi nzuri ..... Kicho chake ni pigo kubwa kwa Taifa hasa kwa wana Ludewa ambao tulijivunia sana uwepo wake"

Hata hivyo alisema njia pekee kwake ya kumuenzi Mchungaji Mtikila ni kuendelea kuwatumikia vema wananchi wa Ludewa kwa kuleta maendeleo zaidi Kama alivyohitaji katika uhai wake.

Filikunjombe alisema katika kuamini kwake na kusimamia anachokiamini hadi mauti inamkuta alikuwa akitetea kuwepo kwa nchi ya Tanganyika na ndio maana kazikwa na bendera ya Tanganyika na kudai kuwa hakuna na kosa kupigania Tanganyika kwani Tanganyika inahitajika.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr Rerema Nchimbi alisema kuwa Mkoa wa Njombe umepoteza kiongozi makini na kuwa katika kumuenzi ni vema kwa vyama vya siasa kuendesha kampeni za amani na utulivu zaidi na kuwa wakati taifa linaelekea katika uchaguzi mkuu ni vema kila chama kumuenzi Mtikila kwa kulinda Amani .

Naibu Katibu mkuu wa DP Taifa Abdul Mluya alisema kuwa suala la kifo cha mwenyekiti wake ni utata mtupu na bado wanaendelea kuchunguza.

Wakati huo huo Chopa ya Filikunjombe aliyotumia kufaria kwenda katika mazishi hayo iliwafanya wananchi kuacha kusikiliza Salam mbali mbali za viongozi na kukimbilia kutazama na kumlaki Mgombea huyo Ubunge jimbo la Ludewa.

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa