UANDIKISHAJI WANACHAMA 'TANZANIA BLOGGERS NETWORK' (TBN).




Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' - TBN kinapenda kuwajulisha wanaotaka kujiunga na chama hicho kuwa fomu za kujiunga zinatolewa. Wahusika ni wamiliki na waendeshaji wote wa mitandao ya kijamii (blogs na forums) Tanzania na Watanzania wanaofanya kazi kama hiyo nje ya nchi.

Sifa kuu kwa mwanachama ni kuwa na blog ambayo ina umri wa miezi sita tangu ianze kuendeshwa mfululizo. Kwa wa kazi wa Dar es Salaam wenye sifa ambao wanataka kujiunga fomu hizo zinapatikana kwenye Ofisi za Muda za Tanzania Bloggers Network (TBN) kwenye Jengo la Dar Free Market lililopo mkabala na Barabara ya Ally Hassan Mwinyi.

Mwanachama muitaji wa kujiunga kabla ya fomu atatakiwa kutoa shs 25,000/- ikiwa ni Kiingilio cha mwanachama, shs 15,000/- yakiwa ni malipo ya ada ya miezi mitatu kwa mwanachama na shs 10,000/- ikiwa ni malipo ya kadi ya TBN kwa mwanachama (utambulisho). Jumla kuu kila mwanachama anatakiwa kulipa shs 50,000/- na kupewa risiti halali ya malipo ya TBN. 

Fomu zitatolewa siku za kazi kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni. Zoezi la utoaji fomu litasimamiwa na Mweka Hazina wa TBN, Shamim Mwasha (0767418941). Fomu pia zinapatikana Ofisi za Michuzi Media, mjini Jengo refu karibu na Hospitali ya Ocean Road ghorofa ya pili. 

Kwa wanachama wa mikoani utaratibu unafanywa namna ya kusambaza fomu hizo mara moja na wanachama watalipa moja kwa moja benki ya NMB kwenye akaunti ya TBN. Utaratibu unafanywa kupata viongozi wa kanda wa muda watakaoratibu usajili kwa kushirikiana na viongozi wa muda wa TBN taifa. Viongozi wa muda wa mikoa na kanda watapewa maelekezo namna ya kusimamia na kuratibu zoezi la kujiunga uwanachama wa TBN.

Mikoani TBN itagawanyika kwa kanda, yaani Kanda ya Pwani (ikijumuisha mikoa ya Tanga na Pwani yenyewe), Kanda ya Zanzibar (ikijumuisha Unguja na Pemba), Kanda ya Dar es salaam, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (inayojumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Rukwa, Simiyu), Kanda ya Kusini (jumuisha mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma), Kanda ya Kati (mikoa ya Dodoma, Tabora, Morogoro na Singida), Kanda ya Magharibi (inayojumuisha mikoa ya Kigoma na Rukwa), Kanda ya Ziwa (yenye mikoa ya Kagera, Geita, Mara na Mwanza), na Kanda ya Kaskazini (inayojumisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara).

Kwa wahitaji unaombwa kuchukua fomu yako mapema kwani usajili wa wanachama wa TBN utafanyika kwa muda wa wiki tatu kisha zoezi hili litafungwa ili kutoa fursa kwa viongozi na kamati husika kutathmini wanachama waliopatikana na litafunguliwa tena baada ya miezi sita.

NB;- Kwa watakaohitaji katiba ya TBN watapewa pia ofisini coppy, lakini coppy hiyo ataigharamia wenyewe. Utaratibu unafanywa wa kuichapa kwenye soft coppy na zitatumwa mikoani kwa gharama za TBN.

Imetolewa na:
Joachim Mushi, 0756469470
Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN)
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Irene Paul na Mzee Chilo ndani ya uzinduzi wa narudi Bongo‏

Mwigizaji Mkuu wa Filamu hiyo Ernest Rwandalla akiwa na wadau waliojitokeza kwenye uzinduzi

Akiwa na baadhi ya wasanii waliojitokeza

Akihojiwa na waandishi wa habari

Uzinduzi ulifanyika katika Bustani ya Wanyama ya Bahari Zoo iliyopo Tegete

Mzee Chilo akiwa na mwigizaji Mkuu wa filamu hiyo

Irene Paul nae alikuwapo pia kushuhudia uzinduzi huo

It was a happy day

Na Mwandishi Wetu
FILAMU Going Bongo ilizinduliwa rasmi juzi na kuhudhuriwa na mamia ya wadau wa filamu nchini, ulifanyika katika eneo la Bahari Zoo.


Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuizindua filamu hiyo, Mwigizaji Mkuu wa Going Bongo Ernest Rwandalla  alisema kuwa filamu hiyo imeshaanza kuoneshwa kimataifa zaidi kwa kuwa watu mbalimbali duniani wameanza kuifuatilia kwa njia ya I tune.


Alisema kuwa ni filamu ambayo inahusiana na suala la afya kwa hapa nchini ambapo inamuonesha mwigizaji kutoka Marekani ambae ni yeye akifanya kazi hapa nchini ya masuala ya Afya.


Alisema kuwa inaonesha ni kwa kiasi gani kuna thamani katika sekta hiyo na yeye akiwa kama mhusika mkuu ameamua kuigiza hivyo ili kuzionesha changamoto mbalimbali za sekta ya afya hapa nchini.
Alisema kuwa imetumia zaidi ya mwaka mmoja na nusu kuikamilisha filamu hiyo na kuwa imehusisha wasanii mbalimbali wa ndani ya nchi pia.


Alisema kuwa imehusisha maeneo kama vile Kariakoo, Sinza na kwengineko huku mahala ambapo palikuwa pakitumiwa kama hospitali ni Mwananyamala.


Alisema kuwa kwa upande wake anaona kuwa kwa sasa kuna mafanikio makubwa katika sekta ya uigizaji hapa nchini kwa kuwa wasanii wengi wanaonesha hali ya kujituma na kufanya kazi yao kwa umakini zaidi.


" Going Bongo ni filamu ambayo inaweza kuandika historia mpya katika ulimwengu wa sanaa ya uigizaji kwa Tanzania kwa kuwa hadi sasa wapo watu wengi ambao wameanza kuiangalia filamu hii ndani na nje ya nchi" alisema.


Kwa upande wake mwigizaji mahiri wa filamu, Ahmed Olotu, Mzee Chilo ambae nae ameigiza kama mmoja kati ya wataalamu wa afya alisema kuwa filamu hiyo inaweza kuitangaza Tanzania kimataifa zaidi.


" Hii ni filamu ambayo imeigizwa vema na ikiwa na kila umakini katika kuigiza na kuandikwa kwake na hata mpangilio wa habari ni mzuri pia" alisema Mzee Chiro.
 Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa