Home » » FILIKUNJOMBE AKABIDHI MSAADA WA TSH MILIONI 40 KIJIJI CHA MAVANGA ASEMA CCM SI MBAYA WABAYA WATU‏

FILIKUNJOMBE AKABIDHI MSAADA WA TSH MILIONI 40 KIJIJI CHA MAVANGA ASEMA CCM SI MBAYA WABAYA WATU‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Deo  Filikunjombe akiwhutubia  wakazi  wa  kijiji  cha Mavanga  wilayani Ludewa  muda mfupi  baada ya  kukabidhi msaada wa  vitu mbali mbali  vya  ujenzi vyenye thamani ya Tsh milioni 40 katika  kijiji hicho

  Viongozi  wa  kijiji  cha Mavanga  akiwemo mwenyekiti wa kijiji Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema )kulia  wakipokea  misaada  ya vifaa vya  ujenzi  toka kwa mbunge Filikunjombe kushoto
 Wananchi  wa Mavanga  wakiwa  wamepanda  juu ya magari na  miti kumwona  mbunge  Filikunjombe
 Wananchi  wakiwa juu ya miti  wakifuatilia  hotuba ya  mbunge  wao  Deo Filikunjombe

 Mbunge  Filikunjombe  akifurahia  jambo  wakati  mkazi  wa  Mavanga akimtaka kuwa  mbunge hadi atakapochoka yeye


 Mwanahabari  wa  kituo cha Radio  Best  Ludewa Deo  Nyoni  akiwa makini  kufuatilia matukio
 Wananchi  wa Mavanga  wakiwa wamebeba  kitanda  cha  kujifungulia  wanawake  wajawazito kilichotolewa na mbunge  Filikunjombe kitanda  chenye thamani ya Tsh milioni 5.2

 Mwenyekiti  wa kijiji  Cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema )akimpongeza  mbunge Filikunjombe kwa  misaada  yake
 Paroko  wa kanisa la Anglicana   kushoto  akipokea  msaada  wa bati  300  kutoka kwa mbunge  Deo Filikunjombe
 
 Mbunge Filikunjombe  kati  akikabidhi  saruji kwa ajili ya shule ya  msingi kijiji  cha Mavanga
 Saruji   iliyotolewa na  mbunge  Filikunjombe Mavanga
 Mbunge Filikunjombe akikabidhi  kitanda cha  wanawake wajawazito  kujifungulia
 Mbunge  Filikunjombe akiwakabidhi  wajawazito  kitanda  cha  kujifungulia
 Mwenyekiti  wa  kijiji  cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema )akiwa  amepokea msaada wa Darubini toka kwa mbunge Deo  Filikunjombe
 Filikunjombe  akiwahutubia  wananchi  wa Mavanga
 Wananchi  Mavanga  wakiwa katika   foleni ya  kuuliza maswali na  kumpongeza  mbunge wao

 Mbunge  Filikunjombe akimkabidhi mpira  kijana wa Chadema kijiji  cha Mavanga
 Kijana  wa  Chadema  akimpongeza mbunge Filikunjombe
 Wananchi  Mavanga  wakimkabidhi  zawadi ya  kuku mbunge  wao Filikunjombe
 Mbunge Filikunjombe akipokea zawadi  ya  mbuzi toka kwa  vingozi wa kanisa la Anglicana  baada ya kuwasaidia bati 300 za  ujenzi wa kanisa
 Mwenyekiti  wa  kijiji  cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema )akimongeza mbunge Filikunjombe
 Filikunjombe akizungumza na mlemavu  aliyefika  katika mkutano  wake

 Wananchi  wa  kijiji  cha Mavanga  wakiwa  wamembeba mbunge  wa Ludewa  Deo Filikunjombe




 Msafara  wa  mbunge  Filikunjombe kijiji  cha Mavanga
 Mbunge wa  Ludewa  Deo Filikunjombe akiwapungia mikono  wananchi wa kata ya Mavanga

 Waendesha  boda  boda  wakiongoza msafara wa mbunge Filikunjombe kwa mbwembwe
 Mbunge  Filikunjombe akiwasikiliza wanafunzi katika  kijiji  cha Mavanga
 Mbunge Filikunjombe akicheza mpira na  wanafunzi  hao  baada ya kuwapa msaada wa mpira na sukari kwa mwaka  mzima

 Wasanii  wa ngoma katika  kijiji  cha Mavanga  wakishiriki kupiga ngoma na mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe kushoto
 Katibu  mwenezi mkoa wa Njombe Honoratus  Mgaya akishiriki  kucheza  ngoma
Mbunge Filikunnjombe na katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe Bw Mgaya  wakicheza ngoma
..............................................................................................................................................................
Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe asema baadhi ya wabunge ,mawaziri na watendaji wabovu serikalini wanakichafua chama cha mapinduzi ( CCM )

Filikunjombe alisema kuwa Ccm ni chama makini na kinachopendwa sana ila shida ipo kwa baadhi ya watu waliopo ndani ya Ccm na serikali ni bomu

mbunge huyo alitoa kauli hiyo leo  katika kijiji cha Mavanga wakati akijibu maswali ya wananchi na viongozi wa vyama vinavyounda katiba ya wananchi ( Ukawa) kuhusiana na Ccm kuwateulia wananchi viongozi wasio na sifa kugombea nafasi mbali mbali.

Alisema kama kila mmoja angetimiza wajibu wake katika nafasi yake hakuna mpinzani ambae angechaguliwa ila kuchaguliwa kwa wapinzani ni kushindwa kwa wale waliowaamini kutoka Ccm kushindwa kuwajibika kwa wananchi waliowaamini

Filikunjombe alisema atakuwa mbunge wa mwisho kunyoshewa kidole na watanzania wakiwemo wananchi wake wa Ludewa kwa kushindwa kuwatumikia wananchi na chama chake cha Ccm .

Kwani alisema hakuomba ubunge kwa ajili ya kujinufaisha binafsi ila aliamua kugombea ili kuwatumikia wana Ludewa kwa kuwapelekea maendeleo hivyo Kazi Yake kwa sasa hadi mwisho wa ubunge wake ni kuleta maendeleo kwa wananchi wake na kuona ahadi zake zinatimia kwa muda uliopangwa na si kujinufaisha kwa wakati.

" Naomba kwanza mtambue kuwa wabunge wote tulipo fika bungeni kwa mara ya kwanza tulikopeshwa Tsh milioni 90 kwa ajili ya kununua gari la kutembelea na Mimi kwa kuwa nilikuwa na gari pesa hizo niliamua kununua gari la wagonjwa Mlangali ambao hawakuwa na gari la wagonjwa ....lengo langu kutumikia wananchi na kuwatatulia kero zao si vinginevyo"

Akielezea msaada huo wa vitu mbali mbali vyenye thamani ya Tsh milioni 40 alivyotoa alisema ni pamoja na kitanda cha kujifungulia wajawazito chenye thamani ya Tsh milioni 5.2,Darubini ,pesa ya taslimu Tsh milioni 1 bati zaidi ya 500 ,rangi debe 20 ,saruji zaidi 525 na vifaa vingine vingi kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa miradi mbali mbali ya kijiji na ujenzi wa makanisa,shule na wodi la wazazi

Awali viongozi ukawa wa kijiji cha Mavanga kata kata ya Mavanga walimpingeza mbunge Filikunjombe kwa kuwa mbunge wa mfano Ludewa japo wapo viongozi wengi ndani ya chama chake ni wabovu.

Mwenyekiti wa Ukawa Mavanga John Mligo akishukuru kwa msaada huo wa vifaa na fedha toka kwa mbunge Filikunjombe alisema kama wabunge na viongozi wote wangefanya kama Filikunjombe kamwe wananchi wasingechukia chama hicho.

Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti huyo wa Ukawa na mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema ) walisema wao kama viongozi wa upinzani hawana shaka na uwakilishi wa mbunge Filikunjombe ndani ya jimbo hilo na nje ya jimbo hilo

" Tumekuwa na wabunge 7 ambao wametangulia kabla ya Filikunjombe ila uwakilishi wake umekuwa wa kuigwa na wabunge wengine na kama wabunge kote nchini wangekuwa watendaji hivyo huenda upinzani nchini usingekuwepo"alisema Mligo

Kwani alisema kuwa Chanzo cha kijiji hicho kuchagua mwenyekiti wa Serikali ya kijiji kutoka Chadema ni baada ya viongozi wa ccm kuonyesha kuwa mbali na wananchi na baadhi Yao kutafuna pesa za michango ya wananchi .

Bw Mligo alisema shida ndani ya Ccm ni vita ya wenyewe kwa wenyewe ndio ambayo imekuwa ikiwachanganya wananchi na kujikuta wananchi wanaingia katika mgawanyiko na kuchagua wapinzani

Alisema wakati wa kampeni hata wasio na sifa wanataka kuchaguliwa kwa kutumia rushwa ,hivyo kutaka kwa Ludewa kutambua wazi mbunge anayekubalika ni Filikunjombe pekee na kuwa hawahitaji mtu zaidi ya mbunge wao aliyewavusha katika maendeleo

Huku mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Bw Mpambichaka akiwataka wananchi wa Ludewa kuacha kuonja sumu kwa kubadili wabunge na kuwa utendaji wa Filikunjombe hakuna wa kumfananisha nae

Alisema kuwa wamepata kushuhudia utendaji wake ndani ya bunge kupitia kamati ya PAC kwa kupambana na ufisadi kupitia Escrow na kuwafanya mawaziri zaidi ya watatu kujiuzulu

Pia kupitia utendaji wake ndani ya jimbo amefanikiwa kuwavuta wana Ludewa ambao siku zote walikuwa wakiona aibu kuweka wazi kuwa ni wakazi wa Ludewa na badala Yake kudanganya kuwa wao ni wazaliwa wa Mkoa wa Ruvuma kutokana na awali Ludewa kuwa nyuma kwa maendeleo .

" Toka Filikunjombe ameingia madarakani mwaka 2010 na kuwepo kwa kasi ya maendeleo ndio tunashuhudia wana Ludewa wakirejea Nyumbani na kujitangaza kuwa wao ni wakazi wa Ludewa tofauti na zamani wengi walikuwa wakijificha kwa aibu "

Hata hivyo alisema wapo wabunge ambao wamekaa majimboni muda mwingi kama akina Mzindakaya huko Sumbawanga ila siku zote ni mtu wa kueleza jinsi alivyofanya Kazi na Mwl Julius Nyerere ila si kujipambanua namna gani alivyoleta maendeleo jimboni

Kuhusu misaada mbali mbali iliyotolewa na mbunge huyo kijijini hapo mwenyekiti huyo alisema kwa mara ya kwanza toka wabunge 7 waliopita kijiji hicho kimepata kupata misaada mingi kutoka kwa mbunge

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa