JESHI LA POLISI NJOMBE LAWAFUKUZA KAZI ASKARI WAKE WATATU‏

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhNftsDNOw2CJKBZ7CUiRXt0awr0nI2gKYSSgx87XRw9nZpGQCHcRrszMlGc2whjhuwQ3vCauDm7-hDufryU0HekZQdqc5ET2D7ka9VPGP-PZ04df9urW3JPGX0Rf9TqKttqOUC9dyDonBz/s640/RPC+NJOMBE.JPG 
Jeshi la polisi mkoani Njombe limeamua kuchukua uamuzi mgumu wa kuwafukuza kazi askari polisi wake watatu kwa makosa mbalimbali waliyoyafanya ikiwemo vitendo vibaya kinyume na sheria za jeshi hilo

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa mtandao huu na kamanda wa polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani (pichani) askari hao waliofukuzwa kazi ni EX.G. 3172 PC Ramadhani Iddi Saidi, EX.G. 9693 PC Emmanuel Morson Lyimo pamoja na EX.G. PC Miraji Jumanne Mtea

Kamanda Ngonyani amesema Jeshi la polisi limeamua kutoa adhabu hiyo kali kutokana na vitendo mbalimbali vya utovu wa nidhamu walivyovifanya ikiwemo tukio la hivi karibuni la kupigana hadharani Septemba 2 mwaka huu Mjini Njombe

Amesema wanategemea adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa askari wengine wenye tabia kama hiyo kwani jeshi halitawavumilia askari wake ambao wanakwenda kinyume cha sheria

Katika hatua nyingine Kamanda Ngonyani amewataka wananchi kuwa makini na askari hao waliofukuzwa kazi huku akisisitiza wananchi kutambua kuwa askari hao si watumishi tena kuanzia Oktoba 24, mwaka huu

Na Edwin Moshi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

NGOMBE WA MILIONI 400/- WAPOTEA NARCO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwenyekiti wa PAC,Deo Filikunjombe.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema Shirika la Ranchi za Taifa (Narco), halistahili kupewa Sh. bilioni 17 walizoomba serikalini kutokana na kushindwa kusimamia uendeshaji na upotevu wa ng’ombe 376 katika Ranchi ya Ruvu mkoani Pwani.

Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe, jana alitoa maelekezo ya kamati kwa viongozi wa Narco na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, baada ya kuwahoji juu ya taarifa ya ukaguzi maalum iliyofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Alisema ukaguzi huo ulibaini kuwa ngombe 376 wamepotea kwa kipindi cha miezi mitatu, makato ya mifuko ya hifadhi ya jamii ya wanachama haipelekwi, kushindwa kuendelea kwa ujenzi wa machinjio licha ya serikali kutoa fedha na kuendelea kudidimia kwa Shirika hilo siku hadi siku.

Ng’ombe hao wana thamani ya Sh. 413,600,000 ikiwa kama kila ng’ombe atakuwa na kilo 220 na kuuzwa kwa Sh. 5,000 kwa kilo moja.

“Kamati tumeona hamstahili kupewa fedha hizi kutokana na kushindwa kwa menejimenti, fedha nyingi imepotea na mifugo pia imepotea, hatupendekezi mpewe fedha hadi mbadilike,” aliagiza Filikunjombe.

Mwenyekiti wa Bodi ya NARCO, Salum Shamte, aliieleza kuwa shirika linakabiliwa na tatizo la ukosefu wa mtaji wa kujiendesha, miundombinu duni jambo ambalo ni gumu kutengeneza faida.

Alisema Narco ilichukua mkopo katika benki ya  CRDB ambako riba ni kati ya asilimia 16 na 18 na kwmba kwa mkopo wa Sh. milioni 400 walilipa Sh. milioni 700 na kwmaba mkopo wa benki ya TIB ni wa kununua ng’ombe na kunenepesha ambao hauwezi kulivusha shirika hilo.

Shamte alisema ujenzi wa machinjio ulisitisha baada ya kuingia mkataba na Suma JKT ambao walijenga chini ya kiwango na kuvunja mkataba nao na kwamba ujenzi utaendelea siku za karibuni na unatarajiwa kukamilika mwakani.

Baada ya maelezo hayo, kamati hiyo iliagiza Msajili wa Hazina kupitia taarifa ya uchunguzi ya CAG akishirikiana na Wizara na kuchukua hatua kwa kipindi cha wiki tatu.

Pia, Bodi ya NARCO ijitathmini iwapo menejimenti ya Narco Taifa na Ruvu, zinastahili kuendelea kuwepo na umri wa kustaafu ni miaka 60, lakini Mkurugenzi Mkuu ana miaka 61. Mwenyekiti wa Bodi pia ametakiwa kujitathimini kama anastahili kuendelea kuwepo.
SOURCE: NIPASHE

USAFI POLISI WAPONZA CHADEMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Nyanda za Juu Kusini, Alatanga Nyagawa

Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe juzi liliwashikilia kwa saa tatu wafuasi na viongozi  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Njombe kwa tuhuma za kuingia kwa jinai kwenye kambi yake.

 Makamu Mwenyekiti wa Chadema Nyanda za Juu Kusini, Alatanga Nyagawa, alidai kuwa viongozi na wafuasi hao walitiwa mbaroni  baada ya kuingia kwenye kambi hiyo kwa lengo la kufanya usafi kwenye makazi ya askari na kituo cha polisi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Nyerere maarufu kama Nyerere Day.

Alisema wafuasi hao na  Diwani wa Kata ya Njombe Mjini, Agrey Mtambo, mwenyekiti wa wilaya, kamanda wa vijana mkoa, na katibu wake walikamatwa na kupelekwa kituoni na kwamba waliachiwa baada ya kuhojiwa.

Aliyataja maeneo mengine ambayo walipanga kufanya usafi kuwa ni masoko ya mjini, kituo cha mabasi.

Alisema  ratiba yao ilionyesha kwamba walitakiwa kuanza kufanya usafi katika kambi hiyo ya polisi, kituo cha polisi na mkoa, mahakama na hospitali teule ya wilaya ya Njombe ya Kibena.

Hata hivyo hawakuweza kukamilisha zoezi hilo kutokana na kutiwa mbaroni. 

Kamanda  wa Polisi mkoa wa Njombe,  Fulgence Ngonyani, alithibitisha kukamatwa kwa viongozi hao hao baada ya kuingia kwenye kambi ya jeshi hilo bila ya kuwa na kibali wala kutoa taarifa

Kamanda Ngonyani alisema watuhumiwa hao wana kosa la jinai kwa kuvamia eneo la jeshi hilo bila kutoa taarifa na kuwa watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
CHANZO: NIPASHE

SERIKALI YAOMBWA KUWEZESHA ASASI NDOGO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WAJAS IRIA MALI zaidi 191 katika Halmashauri ya Mji wa Makambako wamepatiwa mafunzo ya nadharia na vitendo yakutengeneza bidhaa mbalimbali.

Mafunzo hayo yametolewa kwa muda wasiku sita namkufunzi kutoka mkoani Morogoro Elisante Kazimoto ambaye alisema,kwa kipindi cha mwaka 2013/14 ameshatoa mafunzo kwa wajasiriamali wasiopungua 680, katika Mkoa wa Njombe.

Akizungumzia kuhusu mafunzo alis emakuwa nimuhimu kwa wajasiriamali kwani ni kati ya kazi ambazo zinaweza kuwa kwamua na kuondokana naum askini.

Alisema kuwa mafunzo hayo yalihusu utenge nezaji wabatiki, sabuni zamche na zamaji,zakuoshea sakafu,mishumaa ,mapishi ya vyakula mbalimbali,pia wamejifunza kutotolesha vifaranga vya kuku kwa kutumia njia ya kawaida si mashine.

Pia ma funzo hayo yalihusu jinsi yakuotesha uyoga, kutengeneza viatu vya ngozi (Kimas ai)najinsi yakutengeneza mafuta ya mgando, na bidhaa nyinginenyingi,ambapo mafunzo hayo yamewajengea uwezowa kufanya kazi zauzalishaji kwa manufaa ya kuinua uchumi wao .

Kati ya wadau hao wa Zena Mnyika ni mm ojawapo wa wanufaika wamafunzo hayo alis ema, kutokana na mafunzo hayo,uwezeka no wakupata mabadiliko makubwa kiuchumi upo kwa sehemu kubwa na hivyo hali ya utegemezi kwa baadhi ya wanawake itapu ngua.

Bi. Zena alisema pamoja na mafanikio hayo kuna tatizo ambalo kama halitatatuliwa kwa wajasiriamali hao mafunzo kwa ujumla ya takuwa hayana manufaa na kuishia kuwa na kumbukumbu za kwenye daftari.

"Nikweli mafunzo haya yametupa mwelekeo wa maisha wengi hatukuwa nachochote kati kaujuzi,lakini mafunzo haya yanahitaji malighafi na mitaji wanawake wengi hatuna mitaji ya kutosha kuweza kuendesha miradi inayoibuliwa kupitia mafunzo haya," alisema Bi.Zena.

Kupitia gazeti hili aliiomba serikali kutoa hamasa kwa asasi za kifedha za kiserikali nazisizokuwa zakiserikali kuanga lia uwezekano wakuwapa mikopo wajasiriamali wadogowado goiliwaweze kujikwa muaki uch umi nakuongezau za lisha jinakukuza pato la Taifa lakini pia kwa kuongeza pato la kaya.

Mafunzo hayo yamelenga kuwapa uelewa wananchi ambao mitaji yao ni ya chini; na kwamba mchakato uliopo nikuwafikia w anawake au wajasiriamali wengi zaidi katika mikoa mbalimbali ikiwepo Kanda ya Kati Kanda ya Kusini mafunzo ambayo yanatarajiwa kutolewa ndani ya mwaka 2014

Chanzo;Majira

BRN IMEWAJALI WANAFUNZI, SI WALIMU- CWT NJOMBE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) wilayani Njombe mkoani Njombe kimeitaka serikali kufanya tafiti za kutosha katika miradi yake ukiwemo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), wakidai unawazidishia mzigo wa kuwajibika bila kuongezwa ujira.

Pia chama hicho kimeitaka Serikali kusitisha biashara huria ya vitabu vya kiada kutokana na kukinzana kwa baadhi ya vipengele hivyo; kusababisha ugumu katika ufundishaji.

Katibu wa CWT wilayani humo, Bi. Salama Lupenza, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika risala yake aliyoisoma Siku ya Walimu Duniani iliyofanyika mjini Makambako.

Alisema kama Serikali itashindwa kudhibiti hali hiyo iwe inahariri vitabu hivyo na kuvigonga mihuri ili kuwahakikishia walimu.

Aliongeza kuwa, yapo mafanikio katika BRN, lakini wanasikitishwa na mradi huo kutowaangalia walimu badala yake wamewaongezea majukumu bila kuongeza ujira jambo linaloweza kuhatarisha maendeleo ya elimu kwa wanafunzi nchini.

"Waandaaji BRN hawakufanya utafiti wa kutosha kwa sababu kama unashindwa kumwezesha mwezeshaji wa mradi, usitegemee majibu mazuri...mradi huu umewaangalia zaidi wanafunzi si mwalimu ambaye bado ana vilio vingi kama mshahara mdogo, pesa za likizo; hivyo Serikali iwe inatushirikisha katika mipango yake," alisema.

Kwa upande wake, mgeni rasmi mkuu wa wilaya hiyo, Bi. Sara Dumba, aliwataka walimu waendelee kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na taratibu yakiwemo mavazi.

Aliwataka waache tabia ya kukopa katika taasisi za fedha ambazo zimekuwa haziweki wazi masharti yao wakati Serikali ikiendelea kutatua kero zao.

"Elimu ni msingi bora wa maisha, mwalimu ni kioo cha jamii na Serikali kwa upande wake, itaendelea kutatua kero zenu pamoja na kuboresha mazingira mazuri ya kazi.

"Naamini siku moja kelele zote zitaisha kutokana na mipango jinsi ilivyo, miradi ya BRN imewekwa kwa ajili ya jamii iweze kupunguza matatizo mbalimbali," alisema Bi. Dumba.

Sikujua Joel ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi, alisema ili kila mtoto aweze kupata elimu bora, ipo haja ya Serikali kutochanganya siasa na elimu hasa kwenye vitabu vya ufundishia, kuuchunguza upya mradi huo na kuufanyia marekebisho

Chanzo;Majira
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa