WAFAHAMU MAMA SHUJAA WA CHAKULA KUTOKA MKOA WA NJOMBE ANAYETARAJIA KUINGIA KIJIJI CHA MAISHA PLUS SIKU YA JUMAPILI WIKI HII!

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

SANTINA MAPILE (27) mkazi wa Njombe namba yake ya ushiriki ni MS 20 ni mfugaji na anafuga nguruwe.

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu amewahi kupata mafunzo ya ujasiriamali na akabahatika kupata mkopo na kurejesha kwa wakati. Anasema "Nina shamba lenye ukubwa wa ekari 1.5. Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 15"
















NEEMA GILBERT UHAGILE (28) mkazi wa Njombe namba yake ya ushiriki ni MS 19 ni mkulima na mfugaji ana ekari 2 anazolima mahindi, maharagwe na maparachichi na anafuga kuku na ng’ombe.



ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu anapenda kazi ya kilimo  na ufugaji na pia anajiamini katika kazi yake. Anasema "Nina shamba lenye ukubwa wa ekari 2. Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 10 na ninapata mayai trei 200"

MAISHA PLUS/MAMA SHUJAA WA CHAKULA

HERI YA SIKU YAKO YA KUZALIWA BLOGGER EDWIN MOSHI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 
Wadau, "Nakushukuru mwenyezi MUNGU kwa kunifikisha siku hii ya leo Alhamisi Aprili 24 ambapo naadhimisha siku ya kuzaliwa, ni kwa neema yako tu mimi kufika hapa nilipo, nakuomba unisaidie kwa kila kitu katika maisha yangu nizidi kukutumikia vyema". 
Nawashukuru wanalibeneke wenzangu wote, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki kwa kuniunga mkono katika siku hii muhimu kwangu, Asanteni Sana
 
Edwin Moshi, 
 
C.E.O 

MVUA ZAZIDI KUHARIBU MIUNDOMBINU YA BARABARA MAKETE‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Makete mkoani Njombe, baadhi ya barabara zimeharibika vibaya na kusababisha kero kwa watumiaji wa barabara hizo. 

Pichani ni hali ya barabara ya Tanesco iliyopo Makete mjini inavyoonekana ikiwa imejaa mashimo na tope kwa wingi, huku vifusi vya kuikarabati vikiwa vimelundikwa pembeni na kazi ya kuikarabati kushindwa kufanyika kutokana na mvua nyingi zinazonyesha wilayani hapo.(Picha na Edwin Moshi)

ISAACK CHEYO:MIVUTANO HAITALISAIDIA KUNDI LOLOTE KUSHINDA VITA YA KATIBA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.
 
Mjumbe  wa Bunge Maalum la Katiba, amesema kwamba mivutano inayoendelea katika bunge hilo haitasaidia kundi lolote kwa sababu hapatakuwapo na mshindi.
Mjumbe huyo kutoka kundi la 201, Isaack Cheyo, amesema kwamba kinachotakiwa kufanyika ni pande zote zinazovutana kukaa chini na kutafuta maridhiano.
Jumatano jioni wiki hii, wajumbe kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) pamoja na wajumbe wengine 25 wa kuteuliwa kutoka kundi la 201 walitoka nje wakilalamikia pamoja na mambo mengine, kauli za vitisho na ubaguzi zilizotolewa katika Kanisa la Medhodist Jumamosi iliyopita mjini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuteka mapendekezo ya rasimu ya Tume ya Warioba kuhusu Muungano.

 Cheyo alisema kwamba kutoka nje ni suala la kawaida katika mabunge yote duniani kwa upande husika kuonyesha hisia zake kuwa suala fulani hawakubaliani nalo.

Cheyo ambaye anatoka katika Chama cha United Democratic (UDP), aliliambia NIPASHE kuwa: “Pale msipokubaliana nkatafute maridhiano kwamba sisi tunataka haya, na hawa haya.”

Alisema kwamba katika hali ya sasa ya bunge hilo kwa sheria na kanuni, hakuna mshindi kwa sababu zinasema kuwa thelithi mbili ya wajumbe wa pande zote wanatakiwa kukubaliana.

“Kwa hali ya ndani Bara inawezekana theluthi mbili ikapatikana, lakini kwa upande wa Zanzibar haitapatikana, hivyo katiba hakuna,” alisema Cheyo, abaye pia ni Kaimu Katibu Mkuu wa UDP.

Aliongeza: “Hata ikipelekwa kwenye referendum (kura ya maoni) Bara inaweza kupata theluthi mbili, lakini kwa Zanzibar haiwezi kupatikana.”

Alisema kuwa ili kuondoa hali hiyo, yatafutwe maridhiano kwa viongozi wa vyama kukutana na kuwashirikisha viongozi wa dini pamoja na makundi mengine ya wananchi, vinginevyo katiba haitapatikana na matokeo yake itarudi katiba ya zamani.

“Kwa CCM kubadili sura zilizomo katika rasimu na kuleta ya zamani, kwa nini wasilipeleke katika Bunge la Muungano na hili lingeepusha lawana kwa tume,” alisema. 

“Kama ni hivyo basi, Bunge la Katiba lisingeitishwa na kusababisha gharama kubwa kuanzia za kugharamia tume,” alisema.

“Baadhi yetu tunachojiuliza ni kwamba kama kutashindawa kutondoka bila katiba, wananchi huko nje watatuonaje,” alisema.

Alisema kuwa muda wa mapumziko kwa ajili ya kupisha Bunge la Bajeti unaweza kutumika kukutana na kutafuta maridhiano.

“Kama wengi wanakataa rasimu, kwa nini tusiandae kura ya maoni kuuliza wananchi muundo wa Muungano wanaoutaka kisha turejee na kupendekeza muundo walioutaka na hilo litapunguza gharama,” alisema Cheyo na kuongeza kwamba: “Tumeanza vibaya, tungeanza na wananchi.”
 
CHANZO: NIPASHE

RC NJOMBE ATAKA HALMASHAURI KUUNDA SHERIA KWA WANAFUNZI WASIWASILI SEKONDARI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kila mwaka mkoani Njombe  kutowasili ili kuendelea  na masomo mkuu wa mkoa wa Njombe  Capten Msaafu Aseri Msangi ameshauri halmashauri  nchini  kuunda sheria ndogo zitakazoweza kuwabana  wanafunzi  pamoja na wazazi wao ili  kuwapeleka watoto wao  shule.

Akiongea mara baada ya kupokea taarifa  ya matokeo makubwa sasa BRN kwenye sekta ya elimu ya msingi na sekondari  katika halmashauri ya wilaya ya  Njombe akiwa kwenye ziara ya siku tatu   mkuu huyo wa mkoa ameshauri  kuundwa kwa sheria ambayo itawabana mzazi na mtoto  ili sekta ya elimu iweze  kusonga mbele kwa kufikia malengo  ya kusomesha watoto wote wanaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza ikiwa kwa asilimia 21 katika halmashauri iyo bado hawajaripoti.


Amesema kuwa kutokana na shule nyingi kuwa na upungufu wa madawati  hasa katika shule alizoweza kutembelea katika  kata  Mtwango  na Igongolo  aliwataka viongozi wa kata kuhakikisha tatizo hilo linatatuliwa  mara moja huku akiahidi kuchangia madawati kumi ya darasa la awali katika shule ya msingi Ilunda 'B' na kusititiza kutolifanyia mzaha suala la elimu.


Wakiwasilisha taarifa ya elimu makaimu  afisa elimu  wa sekondari na shule ya msingi  walisema sekta hiyo imejipanga  kuhakikisha madai yote ya walimu yaliyondani uwezo wake zikiwemo posho, fedha za uhamisho na likizo wanazilipa mpaka kufikia mwezi june mwaka huu  watakuwa wamemaliza.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa Njombe alishauri wananchi
  kulima kilimo kwa kufuata  kanuni mbalimbali  kutoka kwa wataalamu ili kunufaika na kilimo hicho  ikiwa pamoja na kilimo cha mahindi  kwa kutumia mbolea ya Minjingu Mazao.

Akiongea mara baada ya kukagua shamba darasa la  zao mahindi katika  kijiji cha Itipingi  ikiwa ni sehemu ya  miradi ya matokeo makubwa sasa  amesema,  Kuwa wakulima wengi wamekuwa wakishindwa kupata manufaa kwenye kilimo chao  kutokana na kutokufuata taratibu katika kilimo hicho.
 

TUKIO LA KUSIKITISHA: MZEE WA MIAKA 60 AUAWA KINYAMA KWA TUHUMA ZA USHIRIKINA WILAYANI MAKETE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA

Daktari Luvanda kutoka hospitali ya wilaya ya Makete akionesha majeraha ya kichwa cha mwili wa marehemu yanayohisiwa kupelekea kifo chake.
Mwili wa marehemu baada ya kuondolewa eneo la tukio.
 Polisi kutoka kituo cha Tandala na Makete wilayani wakichukua taarifa za mauaji hayo kwenye shamba ulipokutwa mwili wa marehemu.
 Askari akizungumza na wananchi waliofika eneo la tukio na kuwaonya kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi pamoja na kushirikiana na jeshi hilo kuwapata watuhumiwa wa mauaji hayo.
Mkazi wa kijiji cha Masisiwe kata ya Ukwama Wilayani Makete Mkoani Njombe amefariki Dunia baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mguuni na mtu/watu wasiojulikana mwishoni mwa wiki iliyopita

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa niaba ya mkuu wa polisi wilaya, Mrakibu mwandamizi wa Polisi ambaye pia ni afisa upelelezi Wilaya ya Makete Bw.Gozbert Komba  amesema walipokea taarifa ya mauaji hayo kutoka kwa uongozi wa kijiji hicho na kumtaja marehemu kuwa ni Masori Sanga(60) mkazi wa kijiji cha Masisiwe Kata ya Ukwama Wilayani Makete


Bw. Komba amesema kuwa marehemu huyo aliuawa usiku wa kuamikia Ijumaa wiki iliyopita na watu wasiojulikana kwa imani za kishirikina kwa kuwa marehemu alikuwa mzee na pia kwa mujibu wa maelezo ya mashuhuda wa tukio hilo waliohojiwa na polisi

Pia amesema mpaka sasa Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi kwa ajili ya kuhakikisha wahusika wote wa tukio hilo wanakamatwa kwani kitendo walichokifanya ni cha kinyama  na baada ya tukio hilo muuaji/wauaji hao walitokomea kusiko julikana

Bw.Komba amekemea  vikali suala la wananchi kujichukulia sheria mkononi wilayani hapo na kuwaomba wananchi wasiwe na tabia hizo za kuwaua wazee kwa imani za kishirikina na kuwataka watii sheria bila shuruti ili kuishi kwa Amani katika wilaya yao na nchini kwa ujumla
Mwili wa marehemu ulikutwa kwenye shamba la mahindi ukiwa na majeraha sehemu za kichwani na mguuni ambayo yanadhaniwa kusababisha kifo chake, baada ya watu kupita eneo hilo na kuukuta mwili huo
katika kipindi cha hivi karibuni wilayani Makete kumekuwa na matukio ya mauaji kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo wivu wa kimapenzi na imani za kishirikina jambo linalotia doa wilaya hiyo kutokana na ongezeko la watu kuchukua sheria mikononi kwa kuwaua watuhumiwa wa matukio mbalimbali


Habari/picha na Edwin Moshi, Eddy Blog.

MATUKIO KATIKA PICHA WAKATI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA ELIMU MKOA WA NJOMBE‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Baadhi ya wanafunzi wa shule zilizopo mkoa wa Njombe wakifurahia maadhimisho ya wiki ya elimu yaliyofanyika kimkoa katika wilaya ya Makete Aprili 11, 2014.
Mkuu wa wilaya ya Makete Mhe. Josephine Matiro akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kimkoa katika wilaya yake.
Mkuu wa mkoa wa Njombe kapteni mstaafu Aseri Msangi (Katikati) akipata maelezo kutoka kwa mwalimu aliyetunga vitabu kama njia mojawapo ya kuinua elimu mkoani humo, wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya makete Mh. Josephine Matiro na anayefuata na afisa elimu mkoa wa Njombe Bw. Said Nyasiro.
 Wanafunzi wa shule za msingi wakiingia kwa maandamano katika viwanja vya mabehewani.
 Wanafunzi wa sekondari nao wakiingia katika viwanja hivyo.
Kutoka kushoto mkuu wa wilaya ya Ludewa Mhe. Juma Madaha, Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe. Aseri Msangi, mkuu wa wilaya ya Makete Mhe. Josephine Matiro  na Mkuu wa wilaya ya Njombe Mhe. Sara Dumba.
 Mkuu wa mkoa akikabidhiwa risala kutoka kwa wanafunzi.
 Afisa elimu mkoa wa Njombe Bw. Said Nyasiro akisoma taarifa ya elimu kimkoa.
 Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe. Aseri Msangi akihutubia katika maadhimisho hayo.
 Mkuu wa wilaya ya Makete akimpongeza mwalimu wa shule ya msingi kitulo kwa kupewa kikombe na Mkuu wa Mkoa baada ya shule hiyo kufanya vizuri katika mtihani wa taifa mwaka jana.
 Kikundi cha SUMASESU kutoka Makete kikitumbuiza katika maadhimisho hayo.
Picha ya pamoja.PICHA ZOTE NA EDWIN MOSHI

MAADHIMISHO YA WIKI YA ELIMU MKOA WA NJOMBE YAFANA, MKUU WA MKOA ATILIA MKAZO SUALA LA ELIMU‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni mstaafu Aseri Msangi akihutubia mamia ya wananchi waliofurika viwanja vya mabehewani wilayani Makete mkoani Njombe katika maadhimisho ya wiki ya elimu kimkoa.(Picha/habari na Edwin Moshi, Makete)
Licha ya serikali kuendelea kutatua changamoto lukuki katika sekta ya elimu nchini, wadau wa elimu mkoani Njombe wametakiwa kuwajibika kila mmoja kwa nafasi yake, ili kuinua kiwango cha elimu mkoani humo kwa kuwa ni agizo la serikali hasa katika mkakati wa matokeo makubwa sasa (BRN)

Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Aseri Msangi ameyasema hayo wilayani Makete mkoani hapa katika maadhimisho ya wiki ya elimu kimkoa na kusema kwamba ushirikiano wa pamoja kila mtu kwa nafasi yake kutasaidia kuzidi kuinua kiwango cha elimu kwa mkoa wake

Mh. Msangi amesema suala la kuongeza kiwango cha ufaulu ni la kila mmoja hivyo kuagiza maafisa elimu wilaya zote za mkoa huo kupita kwenye kila shule za sekondari na msingi kubaini changamoto zinazopelekea wanafunzi kufanya vibaya kwenye mitihani yao, na kuwashirikisha wazazi kwa kufanya nao kikao na baada ya hapo watagundua changamoto nyingi ambazo wataweza kuzitatua na zile zilizozidi uwezo wao watazipeleka sehemu husika ili zitatuliwe

"Nyie maafisa elimu wa wilaya zote, nawaagiza tembeleeni shule zenu hasa zile zinazofanya vibaya, mtagundua changamoto nyingi sana, pia muwashirikishe wazazi kwa kufanya nao kikao na muandike kwenye muhtasari maana mwisho wa mwezi huu nitaihitaji ili nione kama mmetekeleza, nawahakikishieni mtagundua mambo mengi sana huko" amesema Msangi

Amesema kwa sasa wanafunzi 538 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu bado hawajaripoti hivyo kutoa agizo kuwa wanafunzi hao watafutwe popote walipo ili waripoti shuleni tayari kwa masomo

Mwanafunzi Noela Msinangila akisoma risala.

Awali akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake mkoani Njombe, Noela Msinangila amesema wanaipongeza serikali kwa kuongeza idadi ya waalimu kila mwaka, kuongeza vitabu, kujenga mabweni pamoja na nyumba za waalimu huku wakiomba serikali kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa, kuongeza idadi ya waalimu wa sayansi na hisabati, pamoja na kuwasaidia wanafunzi yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Naye afisa elimu mkoa wa Njombe Bw. Said Nyasiro amesema mkoa wa Njombe umejipanga vilivyo katika kuinua kiwango cha elimu siku hadi siku kulingana na mipango iliyowekwa ikiwemo kuhskikisha wanafunzi wanasomea katika mazingira mazuri

 Afisa elimu mkoa wa Njombe Bw. Said Nyasiro akisoma taarifa ya elimu kimkoa.

Bw. Nyasiro amesema kwa sasa watahakikisha shule zote katika mkoa huo zitatoa chakula kwa wanafunzi wake kwa kuwa itasaidia wanafunzi hao kuzingatia masomo ipasavyo wawapo darasani, pamoja na kutoa zawadi kwa shule 10 za sekondari na msingi zinazofanya vizuri kimkoa kama motisha katika kuinua elimu

Katika maadhimisho pamoja na mambo mengine zimetolewa zawadi kwa shule 10 za sekondari na msingi zilizofanya vizuri pamoja na halmashauri 3 zilizoongoza kielimu

SERIKALI YASIFU MCHANGO WA SHULE BINAFSI NCHINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Profesa Sifuni Mchome.
Serikali  imesifu mchango unaotolewa na shule za msingi na sekondari binafsi katika kukuza kiwango cha elimu nchini na imeahidi kuwa nao bega kwa bega katika kutekeleza mpango wa Matokeo Makubwa Sasa katika elimu.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, wakati akifungua mkutano wa Taasisi ya Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (Tamongsco) Kanda ya Dar es Salaam.

Alisema lazima elimu ikue kwa ubora na kwa idadi ya wanafunzi wanaojiunga na sekondari na vyuo kuongezeka mwaka hadi mwaka ili kuwa na taifa lililojaa wasomi kama ilivyo kwa mataifa yaliyoendelea.

"Hivi sasa kuna changamoto ya uchache wa wanafunzi wanaojiunga na shule za sekondari na vyuo vya elimu ya juu wakati wanaomaliza darasa la saba imekuwa kubwa," alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tamongosco Kanda ya Dar es Salaam, Albert Katagira, aliiomba serikali kuendelea kutoa ushirikiano kwa shule binafsi ili kufikia malengo ya mpango wa matokeo makubwa sasa.

Alisema shule binafsi zimekuwa na mchango mkubwa katika kukuza kiwango cha elimu nchini hivyo itakuwa vyema iwapo serikali itazipa ushirikiano wa kutosha na kuziwekea mazingira mazuri ya utendaji wa kazi wa kila siku.
SOURCE: NIPASHE
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa