MVUA YAKIHARIBU KITUO CHA MABASI NJOMBE, KERO YAWA KUBWA KWA WATUMIAJI‏

 
 Hii ndiyo hali halisi, baada ya mvua kunyesha hii leo mkoani Njombe, kituo hicho kimegeuka matope matupu, na kusababisha watumiaji wa kituo hicho kupata tabu ya kutembea kwa shida na kutafuta eneo la kukanyaga ili wapite

Kamera yetu imeshuhudia abiria wakikanyaga matope na madimbwi ya maji machafu yaliyoshamiri kituoni hapo huku pia wakirushiwa maji machafu na magari kituoni humo
Hali halisi ndiyo hii.
 Abiria ambaye jina lake halijajulikana mara moja akipita kwenye matope yaliyosheheni kwenye kituo hicha cha mabasi Njombe.
Ni mwendo wa kuchagua eneo la kukanyaga, wengine wanapandisha suruali zao juu zisipate matope.
 Huwenda upande huu unaafadhali kwa abiria hawa lakini wapi, tope tuu.
Tope lenyewe.

Licha ya tabu hii inayowakumba watumiaji wa kituo hiki cha mabasi Njombe, ushuru umekuwa ukikusanywa kama kawaida, lakini miezi michache iliyopita halmashauri ya Njombe ilitangaza kuwa haina mpango wa kukikarabati kituo hicho na badala yake imetenga eneo lingine kwa ajili ya kujenga kituo kipya cha mabasi.

Eddy Blog inaamini kuwa hii adha itaendelea kuwakumba wananchi na watumiaji wa kituo hiki kwa pamoja hivyo kwa kauli ya halmashauri inabidi abiria hao wazidi kuwa wapole na kuvumilia hali hii mpaka kijengwe kituo kipya!

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

BIL.7 KUSAFISHA BARABARA YA MCHUCHUMA NA LIGANGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Zaidi ya shilingi bilioni saba zinatarajia kutumika  katika matengenezo ya  barabara  ya kutoka  katika kijiji cha Nundu  Wilayani Njombe hadi  Wilayani  Ludewa   ili kuweza kupitisha magari yatakayoanza utekelezaji 
wa mradi wa makaa ya mawe  ya mchuchuma na  mradi wa Liganga  wa 
mchuchuma  uliopo Wilayani Ludewa.

Hayo yamesemwa na mkuu wa Mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Asery 
Msangi wakati alipofanya kikao na waaandishi  juu ya ziara  aliyoifanya 
katika Wilaya za Mkoa wa Njombe tangu januari mwaka huu mpaka hivi sasa  ambapo alisema kuwa kutokana na 
magari hayo jinsi alivyoyaona kwenye picha hivyo ofisi yake imeandika  
barua kwenda serikali kuu  kwa ajili ya kuomba fedha hiyo.

Halmashauri  amezitaka   kamati itakayosimamia suala la mchakato wa ufikishaji nishati ya umeme vijijini kupitia wakala wa nishati vijijini REA,MCC, pamoja na Tanesco ili kuendana na ilani ya uchaguzi mkuu ya mwaka 2010/2015 ambapo katika mpango huo  wa matokeo makubwa sasa  kwenye suala la umeme jumla ya vijiji 74 katika mkoa wa Njombe vinatarajia kunufaika na mradi huo.

Akizungumzia suala la mradi wa maji unaendelea mjini njombe Msangi alisema kuwa  jumla ya shilingi bilioni 1.5 zimepokelewa kutoka serikalini ili kuweza kuedeza mradi huo ambao mpaka kumalizika kwake itanghalimu kiasi cha shilingi bilioni 3.5 na kuongeza kuwa kufika mwezi june mwaka huu itakuwa imekamilika kwa asilimia 80.

Amebainisha kuwa  jumla ya miradi 41 katika wilaya nne za mkoa wa njombe imekaguliwa miradi ambayo ipo chini  mpango wa matokeo makubwa sasa  ambayo ni katika sekta za kilimo, maji, uchukuzi , nishati, na elimu na kubaini changamoto mbalimbali ambazo amewaagiza watendaji kutatua changamoto hizo na kuwazitaka Halmashauri kuwa makini wanapotoa tenda kwa wazabin.

MKUU WA MKOA AWAKOROMEA WANAOHARIBU VYANZO VYA MAJI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Mkuu wa  mkoa wa Njombe  Kapteni Mstaafu Asery Msangi amewaka wananchimkoani    hapa kuitunza na kuiendeleza miradi ya maji inayotekelezwakatika maeneo mbalimbali kwa ufadhili  wa watu wa nje pamoja na
kuvitunza nyanzo vya maji.

Keptein Mstaafu  Msangi  ametoa kauli hiyo  katika wilaya
ya Makete  ambapo amezindua  tenki la maji lenye ujazo wa lita 20,000  litakalo pinguza hitaji la watumia maji ambapo jumla ya lita 1400 zinahitajika kwa matumizi ya siku moja ambapo tatizo la maji wilayani humo ni kubwa.

Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya NjombeBi. Sara Dumba amewapongeza wananchi wa vijiji ambavyo  vimenufaika katika kutekeleza miradi wa maji huku akiwataka kutunza vyanzo vya maji kwa njia ya kupanda miti rafiki ili visikauke.

Katika taarifa ya utekelezwaji wa mrida wa maji mtiririko wa kijiji
cha Limage iliyosomwa kwa mgeni rasmi ilieleza kuwa kijiji hicho kina jumla ya vituo 15 vya maji ambavyo vinatoa huduma za maji kwa watu 2,119 ,mradi ambao umeanza  kutekelezwa  mwezi januari 2013 na ulitarajiwa kukamilika mwezi disemba 2014.

CUF LAWAMANI KWA KUVAMIA OFISI YA CCM NA KUJERUHI KIONGOZI WA CCM UBENA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye akizungumza na Mwenyekiti wa UWT Kata ya Ubena Jesca Daudi ambaye alivunjwa mkono na Viongozi wa CUF waliovamia ofisi ya kata kwenye kijiji cha Tokamisasa.
 Katibu wa Wilaya ya Makete Miraji Mtaturu akizungumzia tukio lililomkuta  Mwenyekiti wa UWT Kata ya Ubena Jesca Daudi ambaye alivunjwa mkono na Viongozi wa CUF waliovamia ofisi ya kata kwenye kijiji cha Tokamisasa kuwa ni kitendo cha kinyama na cha kupingwa kwa nguvu zote na kitendo hicho kimemvua sifa za kuwa mgombea ubunge  wa CUF.

MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI MKOA WA NJOMBE YAFANA KATIKA VIWANJA VYA MABEHEWANI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni mstaafu Aseri Msangi akipata maelekezo kwenye banda la idara ya maji kuhusu bili za maji, katika wiki ya maji kimkoa katika viwanja vya mabehewani Makete mjini.
Mkuu wa mkoa Kapt. Msangi akisikiliza maelekezo toka kwa mtaalamu wa maji, katikati ni mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro.
Mkuu wa mkoa akipata maelekezo kuhusu mfumo mzima wa maji Makete mjini unavyofanya kazi.
 Kikundi cha sanaa cha SUMASESU kikitumbuiza kwenye maadhimisho hayo ya wiki ya maji.
 Kikundi cha sanaa kijulikanachoa kama Mchana Hasarani kikikonga nyoyo za washiriki wa maadhimisho hayo.
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza kwenye maadhimisho ya wiki ya maji kimkoa katika viwanja vya mabehewani Makete mjini.
 Mkuu wa mkoa wa Njombe kapteni Mstaafu Aseri Msangi akihutubia wananchi waliofika kumsikiliza katika maadhimisho ya wiki ya maji kimkoa katika viwanja vya mabehewani makete mjini.
Mkuu wa mkoa akihutubia wananchi.
Picha zote na Edwin Moshi, Makete.

WAFANYABIASHARA WALALAMIKIA UCHAKAVU WA SOKO KUU MAKAMBAKO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

WAFANYABIASHARA katika soko kuu la Makambako mkoani Njombe wameilalamikia Halmashauri ya Mji kushindwa kukarabati soko hilo  kwa muda mrefu.

Uchakavu huo umedaiwa  unasababisha bidhaa ambazo zinahifadhiwa ndani yake kuharibika hususani kipindi hiki cha Mvua.

Wafanyabishara hao wamesema, hali ya soko kwa sasa ni mbaya na usalama wa mali zao umekuwa  wa mashaka licha ya kwamba ushuru umekuwa ukitolewa hata hivyo maombi yao ya kufanyika ukarabati hayajasikilizwa na uongozi.

Mrundikano wa taka katika dampo  pia umekuwa kero na kuhatarisa usalama wa afya zao,hali inayotokana na kuchelewa kuzizoa taka hizo.

Mkurugenzi wa Halamashauri ya Mji Makambako Tina Sekambo amesema  kuwa katika bajeti ya mwaka 2014/15 jumla ya  sh, Milioni 150 zimetengwa kwaajili ya ukarabati wa soko hilo.
 

WARSHA YA UBORESHAJI WA KILIMO CHA APPLES MAKETE KWA MAAFISA KILIMO YAFUNGULIWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba+255765056399.
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza wakati akifungua warsha kwa wataalamu wa kilimo katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Makete hii leo. 
Mwezeshaji kutoka shirika ka TAHA Bw. Isaac Ndamanhyilu akizungumza kwenye warsha hiyo. 
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza na wataalamu wa kilimo wa kata na vijiji vya wilaya ya Makete. 
Wataalamu wakifuatilia mafunzo hayo. 
 Mwezeshaji Manfred Bitala akiwawezesha washiriki wa warsha hiyo.
Na Edwin Moshi
Halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe imedhamiria kuinua kilimo cha matofaa maarufu kama apples, ili kiweze kuinua uchumi wa wakulima pamoja na wilaya kwa ujumla

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili kwa mabwana na mabibi shamba wa kata na vijiji, Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro amesema wilaya imeanza kutekeleza agizo la rais Jakaya Kikwete alipofanya ziara wilayani hapo kuwa ni lazima kilimo cha apple kiwe cha biashara wilayani Makete

Mh. Matiro amesema mafunzo watakayopatiwa maafisa hao wa kilimo, wanatakiwa kuyafuata na kwenda kuyatekeleza kwa vitendo katika kata na vijiji vyao ili mabadiliko yaanze kuonekana na ndiyo maana halmashauri imeshirikiana na shirika la TAHA kuwapatia mafunzo ya namna ya kuboresha kilimo hicho katika maeneo wanayotoka

Amesema kwa kuwa jambo hili halihitaji masihara anatarajia kuona mabadiliko mara moja pindi mafunzo hayo yatakapo malizika kwa kwenda kuwaelekeza wakulima kitu cha kufanya ili apples zizalishwe kwa wingi na kwa ubora unaohitajika kwani hilo linawezekana kwa mujibu wa utafiti ambao umefanyika wilayani hapo

Mh. Matiro amesisitiza pia badala ya wananchi kupanda miti mingi ya mbao kwa sasa wanatakiwa wabadilike na wapande miti ya matunda hasa apples kwa kufuata elimu ya wataalamu hao wa kilimo ambayo wamepatiwa katika mafunzo hayo 

Kwa upande wake Bw. Isaac Ndamanhyilu kutoka shirika la Tanzania Hoticultural Association maarufu kama TAHA ambao ni watoaji wa mafunzo hayo, amesema lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuongeza uzalishaji wa apples pamoja na uuzaji wa matunda hayo

Amesema kwa wilaya ya Makete imekuwa ikizalisha matunda hayo kwa wingi lakini hakuna kumbukumbu zinazoonesha kama uzalishaji huo upo Makete, na pia hakuna taarifa zinazoonesha kama wilaya hii ni miongoni mwa maeneo ndani ya Tanzania yanayozalisha apples

Bw. Ndamanhyilu amesema kufuatia kukosekana kwa kumbukumbu hizo, ndiyo maana wameamua kushirikiana na halmashauri kuhakikisha elimu inatolewa kwa mabwana shamba na mabibi shamba na wao wawaongoze wakulima kulima kilimo cha kisasa ili matunda hayo yazalishwe kwa wingi na yenye ubora unaotakiwa tofauti na ilivyo sasa

"Kulikuwa kuna maonesho fulani jijini Arusha, na mgeni rasmi alikuwa Rais Kikwete na alibahatika kuona apples pale, na alipoambiwa kuwa zinazalishwa Makete kwa kweli alishangaa, na ndiyo maana alisema atafika Makete kujionea, na kweli alifika na amesisitiza kilimo hiki kiwe cha biashara na ndio maana tunatoa hii elimu kwenu" alisema

Naye mwezeshaji wa mafunzo hayo Bw. Manfred Bitala amewaasa mabwana na mabibi shamba hao kubadilika kwani wapo baadhi ya wataalamu hao wamekuwa wakihubiri elimu bila kufanya kwa vitendo jambo linalowakatisha tamaa wakulima

"Yaani wakati mwingine ukiliangalia shamba la mabwana na mabibi shamba nia aibu, yaani unakuta shamba la mkulima linaubora kuliko la ninyi wataalam, sasa hii inakatisha tamaa, lazima ninyi muwe mfano wa kuigwa" alisema Bitala

Amesema wao wananafasi kubwa ya kuibadilisha hii nchi kutoka hapa ilipo na kuonekana mabadiliko makubwa na yenye tija katika sekta ya kilimo kama kila mmoja ataamua kufanya kazi yake ipasavyo

Katika mafunzo hayo wamefundishwa mambo mengi ikiwemo dalili na aina za magonjwa yanayoshambulia matunda, na namna ya kulima na kupata mazao mazuri zaidi ya ilivyo sasa

UAWA KWA KUCHOMWA KISU NA MUME MWENZIE, KISA WIVU WA KIMAPENZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mkazi wa kijiji cha Mago kata ya Lupalilo wilayani Makete mkoa wa Njombe Bw. Frenk Sanga (35) ameuawa kikatili kwa kuchomwa kisu kifuani upande wa kushoto ambao ndipo moyo ulipo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Machi 17 mwaka huu majira ya saa 7 usiku, ambapo mtuhumiwa aitwaye Yohana Sanga alimchoma kisu kifuani baada ya kumfumania akiwa na mpenzi wake(hawara) aliyetambulika kwa jina la Matilda Sanga ambaye pia ni mkazi wa kijiji hicho cha Mago

Imeelezwa kuwa siku ya tukio marehemu ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Bi. Matilda, waliongozana usiku hadi nyumbani kwa mwanamke huyo kwa ajili ya kulala pamoja, na ndipo mtuhumiwa ambaye ni Yohana, ambaye inadaiwa alikuwa akifuatilia nyendo zao aliwavamia nyumbani kwa mwanamke huyo na kumchoma kisu kifuani marehemu hadi akapoteza maisha

Baada ya mtuhumiwa kutenda mauaji hayo katika nyumba ya huyo hawara yake alichomoa kisu hicho na kumshikisha marehemu mkononi, kwa lengo la kupoteza ushaidi ili ionekane kuwa alijiua mwenyewe

Akizungumzia tukio hilo Afisa upelelezi wa polisi wilaya ya Makete ambaye pia ni Kaimu OCD wilaya ya Makete, Mrakibu wa polisi Gosbert Komba amesema wao kama jeshi la polisi walipewa taarifa na Bw. Emannuel Sanga (25) ambaye aligundua kuuawa kwa marehemu Frenk na wao kama polisi walifuka eneo la tukio na kuthibitisha mauaji hayo


BIBI WA MIAKA 70 AUAWA KWA KUKATWAKATWA NA PANGA NA MWANAYE UNYANGOGO MAKETE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Jehi la polisi wilaya ya Makete mkoani Njombe linamshikilia Bw. Sadick Sanga (28) mkazi wa kijiji cha Unyangogo kata ya Iniho wilayani hapa, kwa tuhuma za kumuua kikatili Bibi Meluti Mbwilo (70) ambaye ni mama yake wa kambo

Tukio hilo limetokea Machi 14 mwaka huu ambapo mtuhumiwa alitenda mauaji hayo kwa kumkatakata na panga kichwani na miguuni wakati marehemu akiwa jikoni kwake

Akizungumzia tukio hilo Afisa upelelezi wilaya ya Makete ambaye pia ni kaimu OCD, Bw. Gosbert Komba amesema kuwa baada ya wananchi kugundua mauaji hayo, walimkamata mtuhumiwa na kisha wakatoa taarifa kwa jeshi hilo ambapo walifika mara moja na kumtia mbaroni mtuhumiwa

BOFYA HAPA KUENDELEA KUSOMA HABARI HII>>

Baba adaiwa kumuua mwanaye wa miaka 8 mkoani Njombe‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


Picha ni ya kamanda wa polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani

Na Edwin Moshi, Njombe
Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia Bw. Yusufu Sadick Mkalile (33) kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kumzaaa mwenyewe kwa kumziba pua na mdomo

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani  imesema kuwa mtuhumiwa alitenda mauaji hayo Machi 16 mwaka huu majira ya saa 03:20 asubuhi, ambapo alimziba pua na mdomo mwanaye huyo aitwaye Udai Yusufu (8) hali iliyosababisha kukosa hewa na kufariki

Tukio hilo limetokea chumbani, nyumbani kwao mtaa wa Nazareth, kata ya Mjimwema tarafa ya Njombe Mjini wilaya ya Njombe, na hadi anafariki marehemu alikuwa akisoma darasa la pili katika shule ya Msingi Meta mkoani Mbeya

Mtuhumiwa wa mauaji hayo ambaye ni mkulima mkazi wa Stereo mkoani Mbeya amekamatwa na polisi na anaendelea kuhojiwa kuhusiana na mauaji hayo na chanzo bado hakijafahamika



BASI LA JAPANESE EXPRESS LATUMBUKIA MTONI WILAYANI MAKETE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 
Habari zilizotufikia katika chumba chetu cha habari  kwamba basi la kampuni ya Japanese Express linalofanya safari zake kati ya Makete - Njombe, limetumbukia kwenye mto eneo la Lwamadovela wilayani Makete
Basi hilo lilikuwa likitokea Njombe kuja Makete na ajali hiyo imetokea majira ya saa 11 jana jioni kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo
Wapo baadhi ya abiria waliojeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya Ikonda Consolata
credit: Eddy Blog

NEWS:Uongozi wa Chadema wilaya ya Makete waondolewa madarakani, uongozi wa mpito wawekwa madarakani‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
  Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Makete Shaaban Mkakanze.
 

Hatua hiyo imefikiwa baada ya mkutano wa wanachama uliofanyika jumamosi machi 8, mwaka huu kwa pamoja kuazimia kuung'oa madarakani uongozi uliokuwepo baada ya kujadiliana kwa kina katika mkutano huo

Miongoni mwa viongozi waliong'olewa ni pamoja na mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Makete Bw. Sahaaban Mkakanze na katibu wake pamoja na uongozi mzima uliokuwa ukiongoza chama hicho wilaya

Mkutano huo ambao pia uliowashirikisha viongozi wa chadema mkoa wa Njombe akiwemo mwenyekiti Bw. Lulandala, ulibaini kuwa kasi ya kukua kwa chama hicho wilayani Makete ni ndogo ukilinganisha na maeneo mengine licha ya jitihada zinazofanywa na ndiyo maana wakaona wabadilishe uongozi

Katika mkutano huo waliazimia kuchagua uongozi wa muda ambao umepewa miezi miwili ya matazamio kuhakikisha wanakiimarisha chama katika kata zote za wilaya ya Makete ikiwemo kuunda uongozi wa kila kata ambao unaweza kufanya kazi kama inavyotakiwa

Viongozi wa wa muda waliochaguliwa kushikilia chama hicho ngazi ya wilaya kwa muda ni Bw. Ibrahim Ngogo ambaye ni mwenyekiti, Bw. Ilomo ambaye ni katibu na Bw. Stephano Kasanga ambaye ni katibu mwenezi

Mkutano huo umewapa miezi miwili ya kukiimarisha chama kabla ya kuitishwa mkutano mwingine ambao utakuwa wa uchaguzi wa wanachama kuwachagua viongozi wa wilaya wa kukiongoza chama hicho.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa