PSPF YAZINDUA MPANGO MPYA WA UUZAJI NYUMBA KWA BEI NAFUU, SOMA HAPA KUJUA BEI ZAKE





Mfuko wa Pensheni wa PSPF unapenda kuutaarifu Umma kuwa umezindua Mpango Mpya wa uuzaji nyumba zake zilizojengwa kwa ajili ya makazi katika mikoa ya Dar es Salaam- Ilala (Buyuni), Morogoro (Lukobe), Tabora (Usule), Mtwara (Mang’amba), Shinyanga (Ibadakuli) na Iringa (Mawelewele).
Bei za nyumba ni kati ya sh. 52,000,000.00 hadi sh. 71,000,000.00 (bila VAT). Bei hizi ni kulingana na ukubwa wa nyumba na mkoa nyumba ilipo.   Ukubwa wa nyumba ni kuanzia vyumba viwili hadi vinne.
Chini ya utaratibu huu mpya unaoanza kutumika kuanzia Februari 2014; Muombaji atapaswa kuainisha kwenye fomu ya maombi aina ya nyumba anayohitaji na Mkoa ilipo.  Malipo yanaweza kufanyika kwa njia zifuatazo:
1)                           UNUNUZI KAMA MPANGAJI (HIRE PURCHASE):
Mnunuzi atalipia kwa mpango wa mwezi mmoja mmoja au miezi mitatu kwa mkupuo (installments) kulingana na thamani ya nyumba. Katika mpango huu, mnunuzi anaweza kulipia kutokana na vyanzo vingine vya mapato yake mbali na mshahara wake. Mwanachama wa PSPF aliyechangia chini ya  miaka mitano (5) atatakiwa kulipia kiasi cha sh. 5,000,000.00 kama malipo ya mwanzo ya nyumba na asiye mwanachama wa PSPF atatakiwa kulipia kiasi cha sh. 10,000,000.00 kama malipo ya mwanzo ya nyumba kukidhi vigezo vya kununua nyumba (kama mpangaji).

Mpango huu wa Ununuzi kama Mpangaji (Hire Purchase) utamwezesha mnunuzi kulipa kati ya sh. 450, 000.00 (laki nne na hamsini tu) na
sh. 813,000.00 (laki nane na kumi na tatu tu) kwa mwezi kama malipo ya nyumba zinazouzwa na Mfuko kulingana na ukubwa na eneo nyumba ilipo.

2)                           MALIPO YA MARA MOJA (OUTRIGHT PURCHASE)
Mnunuzi atalipia gharama ya kununua nyumba kupitia akaunti ya Mfuko na kisha kusaini makubaliano kabla ya kuhamishiwa umiliki (transfer).

3)                           MKOPO WA NYUMBA KUPITIA BENKI (MORTGAGE BASIS):
Mnunuzi anaweza kuchukua mkopo katika mojawapo ya Benki ambazo Mfuko wa PSPF ina mikataba nazo na kutumia mkopo huo kununulia nyumba. Mabenki hayo ni; CRDB, Azania, Exim na NMB. 
MUHIMU! Iwapo utanunua nyumba kupitia mkopo wa benki (Mortgage) utapaswa kuwa umesajiliwa kwenye Mfuko na kuchangia kwa muda wa miaka mitano au zaidi. Muda wa kurejesha mkopo ni mpaka miaka ishirini na mitano (25) kulingana na matakwa ya Benki husika.
Mwombaji anayehitaji kuona au kukagua nyumba awasiliane nasi kupitia simu: +255 22 2120912/52 au +25522 2127375-6 au E-mail: pspf@pspf-tz.org.

Kwa maelezo zaidi fika Makao Makuu ya PSPF yaliyopo jengo la Golden Jubilee Towers, Barabara ya Ohio au ofisi zetu zilizopo katika kila mkoa.

Imetolewa na

Mkurugenzi Mkuu,
Mfuko wa Pensheni wa PSPF 

Wajasiriamali 191 wapatiwa mafunzo Makambako

WAJASIRIAMALI zaidi ya 191 katika Halmashauri ya Mji wa Makambako wamepatiwa

mafunzo ya nadharia na vitendo ya kutengeneza bidhaa mbalimbali.
Mafunzo hayo yametolewa kwa muda wa siku sita na mkufunzi kutoka mkoani Morogoro Elisante Kazimoto ambaye alisema, kwa kipindi
cha mwaka 2013/14 ameshatoa mafunzo kwa wajasiriamali wasiopungua 680, katika mkoa
wa Njombe.
Akizungumzia kuhusu mafunzo alisema kuwa ni
muhimu kwa wajasiriamali kwani ni kati ya kazi ambazo zinaweza kuwakwamua na kuondokana na umaskini.
Alisema kuwa mafunzo hayo yalihusu utengenezaji wa batiki, sabuni za mche na za maji za kuoshea sakafu, mishumaa, mapishi ya vyakula mbalimbali, pia wamejifunza kutotolesha vifaranga vya kuku kwa kutumia
njia ya kawaida si mashine.
Pia mafunzo hayo yalihusu jinsi ya kuotesha yoga, kutengeneza viatu vya ngozi (kimasai) na
jinsi ya kutengeneza mafuta ya mgando na bidhaa nyingine nyingi, ambapo mafunzo hayo
yamewajengea uwezo wa kufanya kazi za uzalishaji kwa manufaa ya kuinua uchumi wao.
Kati ya wadau hao Zena Mnyika ni mmojawapo wa wanufaika wa mafunzo hayo alisema, kutokana na mafunzo hayo, uwezekano wa kupata mabadiliko makubwa kiuchumi upo kwa sehemu kubwa na hivyo hali ya utegemezi kwa baadhi ya wanawake itapungua.
Bi. Zena alisema pamoja na mafanikio hayo kuna tatizo ambalo kama halitatatuliwa kwa wajasiriamali hao kupatiwa mafunzo kwa ujumla yatakuwa hayana manufaa na kuishia kuwa na kumbukumbu za kwenye daftari.
“Ni kweli mafunzo haya yametupa mwelekeo wa maisha wengi hatukuwa na chochote katika ujuzi, lakini mafunzo haya yanahitaji mali ghafi na mitaji wanawake wengi hatuna mitaji ya kutosha kuweza kuendesha miradi inayoibuliwa kupitia mafunzo haya,”alisema Bi.Zena.
Kupitia gazeti hili aliiomba serikali kutoa hamasa kwa asasi za kifedha za kiserikali na zisizokuwa za kiserikali kuangalia uwezekano wa kuwapa mikopo wajasiriamali wadogo wadogo ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuongeza uzalishaji na kukuza pato la Taifa lakini pia kwa kuongeza pato la kaya.
Mafunzo hayo yamelenga kuwapa uelewa wananchi ambao mitaji yao ni ya chini na kwamba mchakato uliopo ni kuwafi kia wanawake au wajasiriamali wengi zaidi katika mikoa mbalimbali ikiwepo Kandaya kati ya kanda ya kusini mafunzo ambayo yanatarajiwa kutolewa ndani ya mwaka 2014.

Chanzo;Majira

MH. MWIGULU NCHEMBA AKUTANA NA WAFANYABIASHARA MKOA WA NJOMBE


Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Mwigulu Nchemba hii leo amekutana na Wafanyabiashara wa Mkoa wa Njombe kuzungumza nao Kuhusu Wajibu wao wa Kulipa Kodi,Matatizo wanayokumbana naYo kwenye Biashara na namna ya Kuinua Uchumi wao kama Wafanyabiashara wadogo na wakubwa ndani ya Mkoa wa Njombe na Taifa kwa Ujumla.Sehemu ya Wafanyabiashara waliofika kwenye Ukumbi wa Turbo hapa Njombe mjini kwaajili ya Kuzungumza na Naibu waziri wa Fedha Mh;Mwigulu Nchemba.Kubwa zaidi linaloendelea hapa ni Mkutano wa Kubadilishana mawazo kati ya Naibu waziri,Viongozi wa Uchumi Mkoa,TRA na Taasisi mbalimbali za Uchumi pamja na Wafanyabiashara wa Mkoa huu.

NAIBU KATIBU MKUU(CCM-BARA)MH;MWIGULU NCHEMBA, AKUTANA NA WAZEE WA CCM WILAYA YA NJOMBE


Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mh;MWigulu Nchemba akiwasili Ofisi za CCM Mkoa wa Njombe mapema hii leo asubuhi kusiani Kitabu na Kukutana na Wazee wa Chama Cha Cha Mapinduzi Wilaya ya Njombe(M).
 Mh;Mwigulu Nchemba akiteta mambo mbalimbali na Wazee wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Njombe hii leo.Pia Mh;Mwigulu amepokea Salamu za Wazee Mkoa wa Njombe zililzotolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mh;Jah People (Japipo) za Kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha ikiwa ni ishara ya Wazi kabisa kuwa Rais anaimani na Utendaji kazi wake na ni mwadilifu vya kutosha ndio maana akapewa Wizara Nyeti ya Fedha.

CHADEMA yawatoa hofu wafanyakazi

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewataka wafanyakazi wa serikali na umma nchini kote kuondoa hofu ya kukosa ajira endapo chama hicho kitaingia madarakani baada ya Uchaguzi Mkuu mwakani.
Hayo yamebainishwa jana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, katika hotuba zake kwenye mikutano tofauti ya Operesheni M4C Pamoja Daima inayoendelea nchini kote, yenye lengo la kuwaunganisha Watanzania kuelekea chaguzi zijazo, ukiwemo Uchaguzi Mkuu.
Akifafanua zaidi kuhusu hofu iliyojengeka kwa wafanyakazi wengi nchini kutokana na propaganda zinazoenezwa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), alisema kuwa kamwe chama hicho hakitawabagua au kuwaondoa kazini wafanyakazi wa serikali, kwa sababu tu walikuwa kwenye serikali iliyokuwepo madarakani.
“Ni mtu mwenye akili finyu tu ndiye anaweza kufikiria hivyo, kwa sababu CHADEMA kaiwezi kuongoza kuwaondoa wafanyakazi wa serikali waliopo sasa na kutegemea wafanyakazi wapya, wapo wanaosema eti  CHADEMA ikiingia madarakani watatoa wapi wafanyazi, au Ikulu wataipata wapi, hao waliopo ambao ni wasafi ndio watakaoendeleza gurudumu,” alifafanua.
Alisema Ikulu iliyopo si mali ya CCM au chama chochote ni mali ya serikali na kiongozi atakayechaguliwa kutoka chama chochote atakwenda Ikulu hiyo hiyo na wafanyakazi waliopo ndio watakaoendelea kuitumikia serikali hiyo mpya.
“Kwa hiyo nawataka wafanyakazi wote nchini wakiwemo askari polisi na wanajeshi waondoe hofu hiyo, tutakachofanya ni kuchuja wafanyakazi waadilifu na wasio waadilifu, kwa mfano askari polisi ambaye ni mla rushwa au mfanyakazi ambaye ni fisadi, hatutakuwa naye,” aliongeza.
Katika hatua nyingine, Dk. Slaa amemtaka Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, kutekeleza kauli yake aliyoitoa hivi karibuni kwamba serikali itamega sehemu ya ardhi aliyopewa mwekezaji katika mashamba ya mpunga mkoani Mbeya ili kuwarudishia wananchi ambao wanahangaika kutafuta ardhi ya kilimo.
Alisema serikali mara nyingi imekuwa na kauli zisizotekelezeka, hivyo kuwafanya wananchi kutokuwa na imani na serikali yao.
Aidha, katika hotuba zake hizo, Dk. Slaa amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kukemea na kuchukua hatua kwa vyama ambavyo vinaweka makambi ya kuwafundisha vijana wao kufanya vurugu, ikiwamo kupiga watu wakati wa uchaguzi.
Alisema CHADEMA kimekuwa chama kivumilivu sana kutokana na vurugu hizo ambazo mpaka sasa zinafanyika katika baadhi ya miji, jambo ambalo linahatarisha amani nchini.
“CHADEMA hatuamini katika vurugu, lakini tuna uwezo wa kujitetea, vijana wetu wamepigwa na wengine kupoteza maisha kutokana na vurugu zinazofanywa na vijana wanaoitwa Green Guards, tunaamini msajili aliyepo sasa atalifanyika kazi jambo hili, kama mnavyojua  hata hapa Mbeya yapo makambi ambayo yanaendelea kutoa mafunzo hayo,” aliongeza
Chanzo;Mwananchi

Chadema waanza kampeni za urais

Njombe. Viongozi mbalimbali wa Chadema wameanza kupiga kampeni za urais mwaka 2015 kupitia Operesheni Pamoja Daima.
Akihutubia mamia ya wakazi wa Mkoa wa Njombe huku mvua kubwa ikinyesha jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa aliwatahadharisha vigogo wa Serikali wanaoiba fedha za umma kuwa, atawashtaki na kuwafilisi iwapo chama hicho kitashinda uchaguzi mwaka 2015.
Alisema chama hicho kikishinda dola, kitaboresha masilahi kwa watumishi waadilifu lakini mafisadi wanaotafuna fedha za Serikali watapata wakati mgumu.
“Tutakuwa wakali kwa walarushwa,” alisema Dk Slaa.
Dk Slaa alisema watendaji walarushwa na wezi watashtakiwa ili mali walizowaibia Watanzania zirejeshwa Serikalini.
“Ninawapa miezi 15 kabla ya uchaguzi mkuu, vigogo hao kurudisha mali walizoiba vinginevyo watajuta kwa sababu tutawashtaki tutakapoingia madarakani.” alisema.
Naye Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo alisema chama hicho kitatumia kila aina ya ‘silaha’ kilichonayo kuhakikisha majimbo yote ya Mkoa Kilimanjaro yananyakuliwa na chama hicho 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ndesamburo alisema hakuna kikwazo kuyatwaa majimbo hayo kwa vile CCM, kimeshindwa kuwaletea Watanzania maisha bora kama waliyojinadi mwaka 2010.
Kwa sasa Chadema kinashikilia majimbo ya Moshi Mjini kwa vipindi vitatu mfululizo (2000-2015), Jimbo la Hai na Jimbo la Rombo wakati Chama cha Mapinduzi (CCM) kikishikilia majimbo matano.
CCM kinashikilia majimbo ya Moshi Vijijini, Siha, Mwanga, Same Mashariki na Magharibi wakati Tanzania Labour Party (TLP), kikishikilia Jimbo la Vunjo kupitia Mbunge wake, Augustine Mrema.
Akizungumza mjini Singida jana, Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu aliwataka Watanzania kumchagua rais mwadilifu siyo anayehonga hata mapadri fedha chafu zilizotokana na ufisadi.
Alisema baadhi ya viongozi (bila kuwataja) hivi sasa wanapita kwenye nyumba za ibada kutoa rushwa na kudai kwamba zamu yao ya kuwa rais imewadia.
Chanzo;Mwananchi

Operesheni M4C Pamoja Daima yaunguruma Njombe na Chimara

Slaa kuwasili Chimara
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwasili katika mji wa Chimara mkoani Mbeya, ambako alifanya mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika jana.
Katibu wa CCM
Aliyekuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tawi la Isitu, Chimara mkoani Mbeya, Felix Komba akizungumza katika mkutano wa Operesehni M4C Pamoja Daima mbele ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, baada ya katibu huyo kujiunga na Chadema wakati wa mkutano huo uliofanyika Chimara jana.
Kumnadi Mgombea Njombe
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Cadema), Dk. Willibrod Slaa akimnadi mgombea udiwani katika Kata ya Njombe Mjini kupitia chama hicho, Agrey Mtamba, wakati wa mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika mjini Njombe jana.
Slaa kuhutubia Makambako
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwahutubia wananchi wa mji wa Makmabako, katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika jana.
Mkutano Njombe
 Wananchi wa mji wa Makambako wakiwa katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), uliofanyika jana.
Slaa Njombe
Sugu kuhutubia Chimara
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, akihutubia mkutano wa hadhara ikiwa ni mfululizo wa mikutano ya Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika katika mji wa Chamara mkoani Mbeya jana.

PSPF YATOA PONGEZI KWA WAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WA WIZARA YA FEDHA



MFUKO WA PENSHENI WA (PSPF)
                       
SALAMU ZA PONGEZI

Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum (MB)
 Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Mh. Adam K. Malima. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha; Mh. Mwigulu L. Nchemba.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini na wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wanatoa pongezi za dhati kwa Mhe. Saada Mkuya Salum (MB) kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha.


Vile vile, PSPF inatoa pongezi kwa kuteuliwa kwao Naibu Mawaziri wapya wa Wizara ya Fedha; Mh. Mwigulu L. Nchemba (MB) na Mh. Adam K. Malima.

Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wote wamepokea kwa furaha uteuzi wenu mliopewa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. PSPF ipo tayari wakati wote kushirikiana nanyi katika kuleta tija katika utendaji wa Wizara ya Fedha na sekta nzima ya Hifadhi ya Jamii kwa ujumla hapa nchini.

PSPF - Tulizo la Wastaafu

Mkurugenzi Mkuu
Mfuko wa Pensheni - PSPF

PSPF YATOA PONGEZI KWA WAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WA WIZARA YA FEDHA



MFUKO WA PENSHENI WA (PSPF)
                       
SALAMU ZA PONGEZI

Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum (MB)
 Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Mh. Adam K. Malima. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha; Mh. Mwigulu L. Nchemba.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini na wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wanatoa pongezi za dhati kwa Mhe. Saada Mkuya Salum (MB) kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha.


Vile vile, PSPF inatoa pongezi kwa kuteuliwa kwao Naibu Mawaziri wapya wa Wizara ya Fedha; Mh. Mwigulu L. Nchemba (MB) na Mh. Adam K. Malima.

Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wote wamepokea kwa furaha uteuzi wenu mliopewa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. PSPF ipo tayari wakati wote kushirikiana nanyi katika kuleta tija katika utendaji wa Wizara ya Fedha na sekta nzima ya Hifadhi ya Jamii kwa ujumla hapa nchini.

PSPF - Tulizo la Wastaafu

Mkurugenzi Mkuu
Mfuko wa Pensheni - PSPF

MAOFISA WA AFYA NJOMBE WATAKIWA KWENDA KUFANYA UKAGUZI MITAANI

Diwani wa Kata Ya Mjimwema Jimmy Ngumbuke
Uongozi wa Kata ya Mjimwema Mjini Njombe Umewataka Wananchi na Wafanyabiashara Mbalimbali Kuyaweka Mazingira Yao Katika Hali ya Usafi Hasa Katika Kipindi Hiki cha Mvua Ili Kuepuka  Magonjwa ya Mlipuko.

Rai Hiyo Imetolewa na Diwani wa Kata Hiyo Jimmy Ngumbuke Kufuatia Baadhi ya Wananchi na Wafanyabiashara wa Maeneo ya Kata ya Mjimwema Kutupa Uchafu Ovyo Hali Inayotishia Afya za Wakazi wa Maeneo Hayo.

Diwani Mgumbuke Ameuomba Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Kuwaagiza Wataalam wa Afya na Mazingira Kuyafanyia Ukaguzi Mara Kwa Mara Maeneo ya Biashara Zikiwemo Hoteli , Migahawa , Vilabu Vya Pombe za
Kienyeji Pamoja na Makazi ya Watu.

Kwa Upande Wao Baadhi ya Wakazi wa Mitaa ya Mpechi na Joshoni Wameuomba Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Kuwajengea Ghuba la Kutupia Taka , na Kuongeza Kuwa Kwasasa Wamekuwa Wakihifadhi Takataka Kwenye Ndoo na Mifuko na Kisha Kuziweka Barabarani  Jambo Linalohatarishaa Afya Zao Kwani Wakati Mwingine Takataka Hizo Hukaa Zaidi ya Siku Mbili Bila Kuondolewa.

Alfani Ngulwa ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Joshoni Ambaye Amekiri Kuwepo Kwa Tatizo Hilo Katika Mitaa Hiyo na Kusema Kuwa Hali Hiyo Inatokana na Kutokuwepo Kwa Ghuba la Kutupia  Takataka Hizo.
Chanzo; gabriely kilamlya blog

WAFANYABIASHARA WA SOKO KUU NJOMBE WALILIA MAJI NA UMEME

Wafanyabiashara wa Soko Kuu Mjini Njombe Wamerejea Tena Kauli Yao ya Kuutaka Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Kukamilisha Ukarabati wa Miundombinu ya Maji na  Umeme Ndani ya Soko Hilo.
Akiongea na tovuti hii Sokoni Hapo Baadhi ya Wafanatbiashara Hao Wamesema Kuwa Kwa Muda Mrefu Wamekuwa Wakikabiliwa na Changamoto ya Ukosefu wa Huduma ya Umeme na Maji Hali Inayosababisha Soko Hilo Kuwa Chafu.

Wakielezea Suala la Usafi  Ndani ya Soko Hilo Wamesema Kuwa Licha ya Kutoa Fedha Kwa Ajili ya Kuzoa Taka  Lakini Bado Zoezi la Kuzoa Taka Hizo Limekuwa Likichelewa na Kusababisha Mlundikano wa Taka na Harufu Mbaya Inayohatarisha Afya za Wafanyabiashara na Wateja Wanaofika Sokoni Hapo Kwa Ajili ya Kujipatia Mahitaji Yao.

MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF) UNAWATAKIA WATU WOTE SIKUKUU NJEMA MAULID



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MFUKO WA PENSHENI WA PSPF






MAADHIMISHO YA SIKU YA KUZALIWA KWA MTUME MUHAMMAD (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam)
Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wanaungana na Waisalamu na Watanzania wote katika kusheherekea siku ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam)
“PSPF TULIZO LA WASTAAFU”
Mkurugenzi Mkuu,

PSPF

SALAM ZA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUTOKA MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF)

SALAM ZA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUTOKA MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF)






JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MFUKO WA PENSHENI WA PSPF





Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wanaungana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Ali Mohamed Sheni pamoja na wananchi wote wa Tanzania katika kuadhimisha miaka hamsini ya Mapinduzi ya Zanzibar, 12 Januari 2014. 

 


Kwa Mahitaji yako ya Hifadhi ya Jamii PSPF ni chaguo lako, Jiunge sasa

“PSPF TULIZO LA WASTAAFU”

Mkurugenzi Mkuu,

PSPF

MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF) WAOMBOLEZA MSIBA WA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA MAREHEMU DKT. WILLIAM A. MGIMWA


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MFUKO WA PENSHENI WA PSPF
Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unatoa salamu za rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Wizara ya Fedha na Familia ya aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. William A. Mgimwa
Mfuko utamkumbuka kwa ushauri wake na ushirikiano aliouonyesha akiwa Waziri wa Fedha katika kufanikisha maendeleo na ustawi wa Mfuko.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

AMIN

MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF) WAOMBOLEZA MSIBA WA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA MAREHEMU DKT. WILLIAM A. MGIMWA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MFUKO WA PENSHENI WA PSPF
Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unatoa salamu za rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Wizara ya Fedha na Familia ya aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. William A. Mgimwa
Mfuko utamkumbuka kwa ushauri wake na ushirikiano aliouonyesha akiwa Waziri wa Fedha katika kufanikisha maendeleo na ustawi wa Mfuko.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

AMIN
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa