Home » » WATENDAJI NJOMBE KUTUMIA VEMA BARAZA LA BIASHARA

WATENDAJI NJOMBE KUTUMIA VEMA BARAZA LA BIASHARA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
WATENDAJI wa Wilaya za Mkoa wa Njombe, wametakiwa kutumia fursa ya uwepo wa Baraza la Biashara la Mkoa kuunganisha sekta ya umma na binafsi kujadili kutatua changamoto zilizopo katika biashara na kutumia fursa hiyo kutangaza vivutio vya biashara zilivyopo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza hilo, Mkurugenzi wa Biashara wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC), Arthur Mtafya, alisema wajumbe wa baraza hilo hawana budi kuzingatia fursa za uchumi zilizo katika mkoa huo na kujadiliana juu ya vikwazo vya biashara, ili kupanua wigo wa uwekezaji mkoani humo.
“Nia ya kuanzisha baraza katika ngazi ya mkoa na wilaya ni kurahisisha utendaji kutoka ngazi ya taifa mpaka wilayani, kwani kuna mambo yanayoweza kushughulikiwa katika ngazi ya mkoa,” alisema.
Mtafya alisema sera za nchi zinaruhusu baadhi ya changamoto zinazohusu mkoa fulani zitatuliwe katika ngazi ya mkoa na kwamba hiyo inasaidia utendaji na uwajibikaji na kuwa yanaposhindikana ndipo huwasilishwa katika ngazi ya taifa, ili kufanyiwa kazi. Alisema ushiriki kamilifu wa sekta hizo mbili katika ngazi ya mkoa na wilaya utasaidia kwa kiwango kikubwa katika kuinua hali ya biashara na uwekezaji katika mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Kapteni Mstaafu Asei Msangi, alisema baraza hilo jipya litakuwa chachu ya maendeleo kwa kuunganisha sekta ya umma na binafsi katika kujadili vikwazo vya biashara, ili kukuza uchumi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.
Chanzo:Tanzani Daima 

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa