Home » » WAKULI MAMBOGA ZA MAJANI WAHIMIZWA KUTUMIA MBOLEA ASILI

WAKULI MAMBOGA ZA MAJANI WAHIMIZWA KUTUMIA MBOLEA ASILI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza,
 
Wakulima wa mboga za majani wamehimizwa kutumia mbolea za asili, ambazo mbali na kutumika kama kitoweo, pia hutibu na kukinga maradhi mbalimbali.
Mtakwimu wa Masuala ya Kilimo wa Taasisi ya Wanawake Wajasiriamali (Resewo), Joyce Urassa, alisema miongoni mwa changamoto kubwa kwa wakulima wa mboga na matunda ni jinsi ya kukabiliana na wadudu waharibifu.

Alisema hayo katika semina ya uchambuzi wa ripoti juu ya sera za kilimo barani Afrika na madhara yake kwa wanawake vijijini hivi karibuni na kuongeza kuwa mmea wa alovera, majivu na majani ya mwarobaini vikichanganywa pamoja ni dawa pekee yenye uwezo wa kuua wadudu wa aina yoyote katika mimea.

Afisa Biashara Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Ernest Elias, alishauri wakulima kufuata kanuni za ukulima bora kwa kutumia mbolea asili na kuongeza mbali na kuzipatia bidhaa za Tanzania masoko ndani na nje ya nchi, pia watajikwamua kimaisha.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Viongozi katika Kilimo na Mazingira (Tawlae), Dk. Sophia Mlote, alisema: “Serikali itilie mkazo katika kukuza na kuendeleza maarifa ya kilimo cha jadi, hasa katika kumuwezesha mwanawake kuzalisha na kusindika chakula.”
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa