Home » » SERIKALI YASIFU MCHANGO WA SHULE BINAFSI NCHINI

SERIKALI YASIFU MCHANGO WA SHULE BINAFSI NCHINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Profesa Sifuni Mchome.
Serikali  imesifu mchango unaotolewa na shule za msingi na sekondari binafsi katika kukuza kiwango cha elimu nchini na imeahidi kuwa nao bega kwa bega katika kutekeleza mpango wa Matokeo Makubwa Sasa katika elimu.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, wakati akifungua mkutano wa Taasisi ya Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (Tamongsco) Kanda ya Dar es Salaam.

Alisema lazima elimu ikue kwa ubora na kwa idadi ya wanafunzi wanaojiunga na sekondari na vyuo kuongezeka mwaka hadi mwaka ili kuwa na taifa lililojaa wasomi kama ilivyo kwa mataifa yaliyoendelea.

"Hivi sasa kuna changamoto ya uchache wa wanafunzi wanaojiunga na shule za sekondari na vyuo vya elimu ya juu wakati wanaomaliza darasa la saba imekuwa kubwa," alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tamongosco Kanda ya Dar es Salaam, Albert Katagira, aliiomba serikali kuendelea kutoa ushirikiano kwa shule binafsi ili kufikia malengo ya mpango wa matokeo makubwa sasa.

Alisema shule binafsi zimekuwa na mchango mkubwa katika kukuza kiwango cha elimu nchini hivyo itakuwa vyema iwapo serikali itazipa ushirikiano wa kutosha na kuziwekea mazingira mazuri ya utendaji wa kazi wa kila siku.
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa