Home » » RC NJOMBE ATAKA HALMASHAURI KUUNDA SHERIA KWA WANAFUNZI WASIWASILI SEKONDARI

RC NJOMBE ATAKA HALMASHAURI KUUNDA SHERIA KWA WANAFUNZI WASIWASILI SEKONDARI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kila mwaka mkoani Njombe  kutowasili ili kuendelea  na masomo mkuu wa mkoa wa Njombe  Capten Msaafu Aseri Msangi ameshauri halmashauri  nchini  kuunda sheria ndogo zitakazoweza kuwabana  wanafunzi  pamoja na wazazi wao ili  kuwapeleka watoto wao  shule.

Akiongea mara baada ya kupokea taarifa  ya matokeo makubwa sasa BRN kwenye sekta ya elimu ya msingi na sekondari  katika halmashauri ya wilaya ya  Njombe akiwa kwenye ziara ya siku tatu   mkuu huyo wa mkoa ameshauri  kuundwa kwa sheria ambayo itawabana mzazi na mtoto  ili sekta ya elimu iweze  kusonga mbele kwa kufikia malengo  ya kusomesha watoto wote wanaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza ikiwa kwa asilimia 21 katika halmashauri iyo bado hawajaripoti.


Amesema kuwa kutokana na shule nyingi kuwa na upungufu wa madawati  hasa katika shule alizoweza kutembelea katika  kata  Mtwango  na Igongolo  aliwataka viongozi wa kata kuhakikisha tatizo hilo linatatuliwa  mara moja huku akiahidi kuchangia madawati kumi ya darasa la awali katika shule ya msingi Ilunda 'B' na kusititiza kutolifanyia mzaha suala la elimu.


Wakiwasilisha taarifa ya elimu makaimu  afisa elimu  wa sekondari na shule ya msingi  walisema sekta hiyo imejipanga  kuhakikisha madai yote ya walimu yaliyondani uwezo wake zikiwemo posho, fedha za uhamisho na likizo wanazilipa mpaka kufikia mwezi june mwaka huu  watakuwa wamemaliza.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa Njombe alishauri wananchi
  kulima kilimo kwa kufuata  kanuni mbalimbali  kutoka kwa wataalamu ili kunufaika na kilimo hicho  ikiwa pamoja na kilimo cha mahindi  kwa kutumia mbolea ya Minjingu Mazao.

Akiongea mara baada ya kukagua shamba darasa la  zao mahindi katika  kijiji cha Itipingi  ikiwa ni sehemu ya  miradi ya matokeo makubwa sasa  amesema,  Kuwa wakulima wengi wamekuwa wakishindwa kupata manufaa kwenye kilimo chao  kutokana na kutokufuata taratibu katika kilimo hicho.
 

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa