Home » » MVUA YAKIHARIBU KITUO CHA MABASI NJOMBE, KERO YAWA KUBWA KWA WATUMIAJI‏

MVUA YAKIHARIBU KITUO CHA MABASI NJOMBE, KERO YAWA KUBWA KWA WATUMIAJI‏

 
 Hii ndiyo hali halisi, baada ya mvua kunyesha hii leo mkoani Njombe, kituo hicho kimegeuka matope matupu, na kusababisha watumiaji wa kituo hicho kupata tabu ya kutembea kwa shida na kutafuta eneo la kukanyaga ili wapite

Kamera yetu imeshuhudia abiria wakikanyaga matope na madimbwi ya maji machafu yaliyoshamiri kituoni hapo huku pia wakirushiwa maji machafu na magari kituoni humo
Hali halisi ndiyo hii.
 Abiria ambaye jina lake halijajulikana mara moja akipita kwenye matope yaliyosheheni kwenye kituo hicha cha mabasi Njombe.
Ni mwendo wa kuchagua eneo la kukanyaga, wengine wanapandisha suruali zao juu zisipate matope.
 Huwenda upande huu unaafadhali kwa abiria hawa lakini wapi, tope tuu.
Tope lenyewe.

Licha ya tabu hii inayowakumba watumiaji wa kituo hiki cha mabasi Njombe, ushuru umekuwa ukikusanywa kama kawaida, lakini miezi michache iliyopita halmashauri ya Njombe ilitangaza kuwa haina mpango wa kukikarabati kituo hicho na badala yake imetenga eneo lingine kwa ajili ya kujenga kituo kipya cha mabasi.

Eddy Blog inaamini kuwa hii adha itaendelea kuwakumba wananchi na watumiaji wa kituo hiki kwa pamoja hivyo kwa kauli ya halmashauri inabidi abiria hao wazidi kuwa wapole na kuvumilia hali hii mpaka kijengwe kituo kipya!

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa