UTENDAJI KAZI WA MBUNGE FILIKUNJOMBE WAWAVUTIA WAPIGA KURA WAAMUA KUMBEBA MGONGONI



Wananchi wa kata ya Manda Ludewa wakimfuta jasho mbunge wao Deo Filikunjombe kama kumpongeza kwa utekelezaji mzuri wa ahadi na uwakilishi uliotukuka bungeni
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiwa amebebwa na mpiga kura wake kama kumpongeza kwa utendaji wake mzuri
Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akifurahia baada ya kupongezwa kwa kubebwa mgongoni na mpiga kura wake
Mbunge Filikunjombe kati akipokea zawadi ya mbuzi kutoka kwa mkazi wa manda huku mkewe Habiba akishukuru (picha na Blogu ya Francis Godwin)

HIVI NDIVYO JINSI STENDI YA NJOMBE ILIVYOKUWA KERO KWA WANAINCHI

Mpiga picha  wa Clouds TV  akiwajibika   kuchukua  tukio la ubovu wa  stendi  ya Njombe 
Abiria   wakipita kwa shida katika  stendi ya  Njombe 
Mwanahabari  wa Clouds TV na Radio Recho akitafuta  eneo la  kupita  katika  stendi  hiyo ya Njombe 
Madereva  na  abiria   wanaotumia  stendi ya Njombe mjini  ambayo ni stendi kuu ya mabasi  yaendayo mikoani  wamelalamikia  ubovu  wa stendi  hiyo na kumwomba  mbunge wa  jimbo  hilo Anne  Simamba  Makinda  kushughulikia  tatizo  hilo.

Wakizungumza na mtandao  huu wa www.francisgodwin.blogspot.com  madereva hao na  wananchi  walisema  kuwa  ubovu wa stendi  hiyo umekuwa ni kero kubwa  kwao  na  kuiomba  Halmashauri  ya  mji  wa Njombe  kulishughulikia  suala   hilo

John Sanga  ni  mmoja  kati ya madereva  eneo hilo la stendi alisema kuwa  wameshangazwa na hatua ya  mbunge  wao ambae ni spika wa Bunge  kushindwa  kuwajibika kwa kusimamia utengenezaji wa  stendi hiyo.

Kwa  alisema  wakati wa jua  eneo hilo limekuwa  likiongoza kwa  kuwa na  vumbi na  wakati wa masika  linaongoza kwa kuwa na tope sana .

Hata   hivyo  alisema  kuwa uongozi  wa serikali ya  Njombe  umekuwa ukitoa ahadi ya  kutengeneza stendi  bila kutekeleza kwa wakati na pale  madereva  wanapotaka  kugoma wamekuwa  wakitumia polisi  kuwakamata  waanzilishi  wa migomo  hiyo.

Huku Sarah Ndelwa ambae  ni mmoja kati ya abiria   waliohojiwa akimtaka  mbunge Makinda  kusaidia  kuondoa aibu hiyo ya ubovu wa  stendi  nyumbani kwake.

KIJIJI CHA IKONDO KINAKABILIWA KERO MBALIMBALI.

WANANCHI wa kijiji cha Ikondo mkoani Njombe wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya askari wa jeshi la  polisi kuwadai fedha kama gharama ya kuwafikia kijijini hapo mara  wanapo ripoti kuwepo kwa matukio tofauti kama vifo na mengineyo.

Hayo yamebainishwa na wananchi katika mkutano ulioitishwa na serikali ya kijiji baada ya kutembelewa na kamati ya ushauri ya wilaya, ambayo imefika katika kata hiyo kufanya mkutano na wananchi ili kubaini mapungufu ya kiutendaji na kuyatafutia ufumbuzi.

Ezkieli Mhenga ni mmoja kati ya wananchi ambao wamefunguka kwa kulitupia lawama jeshi la polisi kuwa hutozwa fedha zaidi ya laki tano hadi milioni tano iwapo watatoa taarifa za kuwepo kwa matukio kama ya mtu kujinyonga fedha ambazo askari hudai kuwa ni kwaaajili ya mafuta ya gari.

Akizungumza kwa niaba ya jeshi la Polisi Mrakibu msaidizi wa jeshi la polisi Issa Asali amewashauri wananchi hao kuwa jeshi hilo linapaswa kutoa huduma bure na iwapo watakutana na askari anayedai fedha kama malipo ya kazi taarifa zitolewe kwa viongozi ili kumshughulikia kisheria askari atakaye bainika kupokea fedha hizo.
  
Katika hatua nyingine wameelekeza malalamiko yao katika sekta ya afya  wanawake wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kutozwa fedha , Conradi  Ugonile  ni mganga mkuu wa Wilaya  amesema, huduma za watoto na wajawazito ni bure, wakati mkuu wa Wilaya Sarah Dumba amesema kero za wananchi zinashughulikiwa, ikiwemo ukosefu wa dawa katika zahanati na bajeti ya mwaka 2013/14 fedha kwaajili ya kuboresha miundo mbinu imetengwa kinasubiriwa ni utekelezaji

WAGANGA WA JADI NJOMBE CHANZO CHA MAUAJI YA VIKONGWE

MAUAJI ya vikongwe yameendelea kushamiri katika mkoa wa Njombe kutokana na imani za kishirikina zinazochochewa na waganga wa jadi ambao hupiga ramri chonganishi na kusababisha jamii kutokuwa na amani na ndugu zao..

Imeelezwa katika mwaka 2013 mauaji yanayoshabihiana na Imani za kishirikiana yameripotiwa kwa watu zaidi ya 17 kuuawa kikatiri katika wilaya za Ludewa, makete,Njombe na Wangong’ombe.


Serikali kwa kushirikiana na jeshi la polisi limekuwa likitoa likitoa elimu kwa wananchi kutokimbilia kwa waganga wa tiba asilia, kupiga Ramri hizo  jambo hilo limeonekana kuwa tatizo sugu katika mkoa huo.



Akizungumaza katika kikao cha mwaka cha waganga wa jadi Dkt. Maria Lupenza amesema, kuwa  zaidi ya asilimia 60 ya wagonjwa hutumia tiba asilia kabla ya kufika katika vituo vya tiba za  hospitali na Zahanati jambo ambalo linaonesha ni kwa zaidi ya asilimia 50 ya watanzania bado wanaamini zaidi tiba za asili.

Salumu Mkalla ni Inspekta wa jeshi la polisi katika kikao hicho ameeleza kuwa mauaji ambayo yametokea katika kip[indi cha mwaka mengi kati ya hayo yanashabihiana na imani za kishirikina kutokana na mazingirz ya kifo hata hivyo ameonya waganga hao kukomesha mara moja huduma ya ramri.


Menyekiti wa chawatiata mkoani humo Salumu Lugenge amesema waganga wanaotoa huduma ya kupiga ramri ni wa kutoka nje ya mkoa na hufanya kazi hiyo kwa kujiotangaza kupitia vyombo vya habari kisha hutoweka mara yanapotokea mauaji ambayo ni matokeo ya kazi yao.

IDARA YA UHAMIAJI MKOA WA NJOMBE YAKABIDHI MSAADA KWA WATOTO YATIMA

 Bi.Rose Mhagama Akitoa Taarifa ya Gharama za Msaada walioutoa Kwa Watoto Yatima Leo
Watumishi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Njombe Wakiongozwa na Afisa Uhamiaji Mkoa Bi.Rose Mhagama Leo Wamekabidhi Misaada Mbalimbali Kwa Watoto Wanaoishi Kwenye Mazingira Magumu na Yatima Vyenye Thamani Ya Zaidi ya Shilingi Laki Nne.

Akizungumza Wakati wa Kukabidhi Misaada Hiyo Kwa Mwakilishi wa Watoto Yatima Afisa Uhamiaji Mkoa wa Njombe Bi.Rose Mhagama Amesema Kuwa Vitu Hivyo Wameamua Kuvitoa Kama Watumishi Kwa Kutambua Adha Wanazozipata Watoto Yatima Katika Mazingira Tofauti ya Mkoa wa Njombe.

Aidha Amesema Kuwa Miongoni Mwa Vitu Walivyovitoa ni Pamoja na Mchele Kilo Mia Moja,Chumvi,Mafuta Katoni za Sabuni,Dawa za Meno na Miswaki,Mafuta ya Kupikia Pamoja na Soda.

Akipokea Vitu Hivyo Kwa niaba ya Watoto Hao Bwana Sambala Amepongeza Jitihada Kubwa Zinazofanywa na Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Njombe na Kwamba Kitendo Hicho Kinawafanya Watoto Yatima Kufarijika na Kuto kata tamaa ya Kuishi.


Pia Bwana Sambala Amewaomba Wadau Wengine Kuendelea Kujitolea Kuwasaidia Watoto Hao Ambao Wamekuwa Wakipata Shida Katika Katika Maisha Yao.
Chanzo;Na Gabriel Kilamlya blog 

Namna ya kuishi na mtoto mwenye vvu-1

Wiki iliyopita tuliona uchunguzi na matibabu kwa mtoto mwenye virusi vya Ukimwi, leo tunaendelea na mada hiyo na tutaangalia jinsi ya kuishi na mtoto wa mwenye VVU.
Zingatia ushauri na matibabu.
Mzazi au mlezi kupata ushauri nasaha kutoka kwa wataalamu wa afya wenye mafunzo maalumu ya VVU na Ukimwi ni jambo muhimu sana kwani itakufanya ulifahamu tatizo na namna ya kukabiliana nalo. Kupata kwako elimu hiyo kutakusaidia kulinda afya ya mtoto wako.
Kama mtoto mwenye VVU alishaanza matibabu ya dawa za kufubaza makali ya VVU na dawa za kuzuia magonjwa nyemelezi, hakikisha kuwa mtoto anapata dawa bila kukosa kwani dawa hizi hupewa maisha yake yote. Ni muhimu kufuata masharti kwani dawa hizi ndizo zinazomwongezea muda wa kuishi, kadri anavyotumia dawa za ARV kinga ya mwili nayo huongezeka na afya ya mwili huimarika na hivyo kuishi vizuri.
Ushauri nasaha na kufahamu umuhimu wa dawa za ARV na ile hali ya kufuatilia matibabu ya mtoto inakusaidia kumjengea imani na dawa hizo tangu akiwa mtoto mpaka ukubwani.
Kumjenga kitabia mapema kuna faida kubwa kwani humfanya asiache kutumia dawa hata akiwa mkubwa.
Pale unapoona dalili za magonjwa yoyote ni vyema kumwahisha na kumpeleka katika huduma za afya mapema. Kumbuka kinga ni bora kuliko tiba, watoto wenye VVU wapo katika hatari zaidi kushambuliwa na maradhi ukilinganisha na wengine.
Mlo kamili
Mlo kamili huwa na vyakula mchanganyiko yaani wanga, proteini, mafuta, mboga za majani na matunda na unywaji wa maji ya kutosha. Vyakula hivi ndivyo vinavyotupa nguvu na joto, kujenga mwili na kinga ya mwili.
Mlo kamili haimaanishi ule wenye gharama kubwa. Jamii yetu imezungukwa na vyakula vya asili ambavyo hupatikana kwa urahisi mfano mboga za majani kama mchicha, matembele, karoti. Vyakula vya protini kama vile maharage ya soya, kunde, njegere na matunda kama maembe, machungwa, matikiti maji.
Hivyo ni jambo la msingi mzazi au mlezi kulima bustani za mboga na matunda na si vibaya kufuga kuku wa kienyeji kwa ajili ya mayai na nyama.
Mboga mboga, matunda na protini ni muhimu katika ujenzi wa kinga ya mwili ikumbukwe mtoto mwenye VVU ni rahisi kushambuliwa na maradhi kwani kinga inakua dhaifu na umri wake ni mdogo
Mtoto huyu anahitaji kupata mapumziko ya kutosha zaidi ya saa nane kwa siku kwani mapumziko husaidia kinga ya mwili kuimarika, kwa watoto wenye umri wa miaka 2 kuendelea michezo ya kitoto na wenzake humfanya kuwa na mwili imara na kuwa mwenye furaha.
Kumjenga kisaikolojia
Kwanza kabisa mzazi anatakiwa kukubaliana na hali halisi baada ya kuelewa ushauri aliopewa . Ni jukumu lake kumjenga kisaikolojia mtoto wake, mzazi au mlezi anapaswa kumkuza vizuri kwa kumuonyesha upendo na furaha na huna budi kumfanya asijione yuko tofauti.
Pale atakapofikia umri wa kuanza kutambua hali yake ni vizuri akaelimishwa kuhusu mambo mbalimbali yenye tija na afya yake. Akieleweshwa na kutiwa moyo atakubaliana na hali yake pasipo kumpa msongo wa mawazo au kupata sononeko, uwepo wa mambo haya mawili huweza kumfanya asiwe mwenye afya njema.
Chanzo;Mwananchi

ABIRIA WALIOKUWA WAKISAFIRI NA BASI LA UKINGA EXPRESS WANUSURIKA KIFO KUFUATIA AJALI MBAYA WILAYANI MAKETE


 Muonekano wa Basi la Ukinga Express likiwa kwenye eneo la ajali.
Abiria waliokuwa wakisafiri kwa basi la Ukinga Express kutoka Njombe kwenda Makete mkoani Njombe, wamenusurika kifo baada ya basi hilo walilokuwa wakisafiria kuigonga fuso kwa nyuma iliyokuwa imepata hitilafu na kuegeshwa barabarani

Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo katika eneo linalohofiwa na wengi la Lwamadovela kata ya Tandala wilayani Makete, baada ya dereva wa basi hilo kuigonga kwa nyuma fuso hiyo ambayo ilipata hitilafu kwenye eneo lenye kona

Wakizungumza na mwandishi wa eddy blog aliyefika eneo la tukio na kushuhudia ajali hiyo, mashuhuda hao bila kutaja majina yao wamesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi hilo kushindwa kulimudu gari lake licha ya kuwepo na kona kali, lakini pia mwenye fuso alishindwa kuweka ishara za kutosha kuonesha kama gari lake limepata hitilafu barabarani

"Unajua braza(akimaanisha kaka) dereva huyu wa hili basi alikuwa mwendo na ndio maana ghafla alipoanza kukunja kona akakutana na hii fuso mbovu, kwa kuwa alikuwa na mwendo kasi ilikuwa ngumu kushika breki ingawa alijitahidi kama unavyoona lakini ilishindikana, ndipo akaigonga hii fuso kwa nyuma" alisema shuhuda huyo

wamesema kutokana na ajali hiyo, baadhi ya abiria walipata majeraha hasa waliokuwa wamekaa viti vya mbele, ingawa mashuhuda hao hawakujua mara moja ni idadi ya abiria wangapi wameumia na hali zao zikoje

Hadi mwandishi wetu ambaye alikuwa akipita eneo hilo kuendelea na safari na kukutana na tukio hilo anaondoka eneo hilo, polisi walikuwa wakisubiriwa kuja kupima na kufanya taratibu za kijeshi kuhusu ajali hiyo, hivyo kuacha wananchi waliokuwepo eneo hilo wakiwasubiri

Ikumbukwe kuwa eneo hilo lililotokea ajali hiyo halina mtandao wa simu, hivyo aliyekuwa akitaka mawasiliano alikuwa akitembea umbali mrefu kutafuta mtandao, hali inayodaiwa kuchelewesha kufikisha taarifa hizo kwa polisi Makete mjini
Chanzo ni Edwinmushi.com

Picha: Mvua zaanza kuleta kizaazaa Wilayani Makete


Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa wingi hivi sasa wilayani Makete, zimeshaanza kuleta madhara baada ya magari kuanza kuteleza kutokana na aina ya kifusi kilichomwagwa katika eneo la Mang'oto wilayani Makete barabara ya Makete - Njombe, kuteleza kupita kiasi

Pichani hapo juu ni basi ma Mwafrika linalofanya safari zake kati ya Iringa-Makete likiwa limekwama kwa muda Kutokana na mvua zinazonyesha wilayani Makete, na hapa ni katika kata ya Mang'oto wilayani hapo, mita chache tu kabla ya kufika kwenye lami

Hii inatokana na kifusi kilichowekwa kwenye barabara hiyo kuonekana na utelezi wa hali ya juu pindi mvua inaponyesha hata kwa sekunde chache

Na Edwin Moshi


KINANA ATEMBELEA CHUO CHA VETA MAKETE

 Katibu mkuu wa CCM Ndg Kinana akisalimiana na wafanyakazi wa chuo cha ufundi stadi VETA Makete wakati alipotembelea chuo hicho mapema leo jioni
 Katibu wa NEC Siasa na uhusiano wa kimataifa Dkt. Asharose Migiro (wa pili kulia) akicheza muziki wa kuifagilia CCM wakati alipotembelea chuo cha VETA Makete, kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro naye akicheza muziki
 Mkurugenzi wa VETA kanda ya nyanda za juu kusini Monica Mbele akisoma taarifa ya chuo cha VETA Makete kwa katibu mkuu wa CCM ndg Abdulrahman Kinana
Mkurugenzi Monica akikabidhi taarifa ya chuo cha veta Makete kwa Ndugu Kinana
 Katibu wa NEC itikadi na uenezi Nape Nnauye akitumia cherehani katika darasa la ushonaji chuo cha VETA Makete
Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwenye darasa la ushonaji VETA Makete
 Hapa Kinana kapewa shati, analijaribu
 Ndg Kinana akipanda mti VETA Makete
Katibu NEC siasa na uhusiano wa kimataifa Dkt. Asharose Migiro akiwa na mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro wakila pozi lao kwenye chuo cha VETA Makete
picha ya pamoja
Chanzo;Edwin Moshi

Kevela Kamanda mpya UVCCM

Yono Stanley KevelaMBUNGE wa zamani wa Njombe, Yono Stanley Kevela  amechaguliwa kuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa UVCCM wa Wilaya ya Wanging’ombe katika mkoa mpya wa Njombe.
Kevela ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Njombe kati ya mwaka 2005-2010 anatarajiwa kusimikwa rasmi kwenye nafasi hiyo keshokutwa mkoani Njombe.
Akizungumza na gazeti hili mara baada ya uteuzi huo, Kevela aliwashukuru viongozi wote wa CCM kwa kumwamini na kusema kuwa amebaki na deni kubwa la kukitumikia chama hicho kwa uadilifu na uaminifu mkubwa.
“Nawashukuru wanaCCM wenzangu kuanzia ngazi ya mabalozi, tawi, kata, wilaya, mkoa hadi taifa kwa kuona ninafaa kukitumikia chama changu kwenye nafasi hii, nimebaki na deni la kukitumikia chama changu kwa unyenyekevu mkubwa na naahidi sitawaangusha,” alisema.
Kevela ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Yono Auction Mart, alisema wanachama wote wa CCM washikamane kutekeleza ilani ya chama chao na kuiga mfano wa Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete namna anavyotekeleza ahadi kwa vitendo.
“Mheshimiwa Rais Kikwete ametekeleza ahadi zake kwa kiwango kikubwa sana, ameipaisha Tanzania chati katika anga za kimataifa, hivyo wanachama wengine lazima tufuate nyayo zake kwa kuchapa kazi na kukiimarisha chama, tusitegeane, kila mwanachama atimize wajibu wake,” alisema Kevela ambaye anasomea Shahada ya Uzamivu (PhD), katika Masoko, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Pia alisifu ziara zinazofanywa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana na timu yake katika mikoa mbalimbali kuwa ni hatua nzuri ya kukiimarisha na kukijenga chama hicho.
Kevela aliwashangaa baadhi ya viongozi wa chama hicho wanaojigeuza miungu watu kwa kushindwa kuwasikiliza wanachama wanapokuwa na kero mbalimbali.
“CCM ni ya wanachama, na viongozi hawapaswi kuwapuuzia wanapokuwa na jambo badala ya kujigeuza miungu watu na kuendesha mambo wanavyotaka wao,” alisema Kevela huku akisisitiza kwamba wapinzani wataambulia patupu uchaguzi wa 2015 kutokana na namna CCM inavyotekeleza ahadi zake kwa wananchi.
Alisema atatumia nafasi hiyo kuwasaidia vijana kupata fursa mbalimbali za kiuchumi kwenye taasisi za fedha ili waweze kupata fedha za kufanya ujasirimali na biashara hivyo kujiondoa kwenye lindi la umaskini.
Chanzo;Tanzania Daima

HOT NEWS: ASKARI MAGEREZA WILAYANI MAKETE AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA


Juma Msam Swedi mtumishi wa wizara ya mambo ya ndani kitengo cha askari magereza wilayani Makete mkoa wa Njombe amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Makete kwa kosa la kushawishi na kupokea rushwa iliyokuwa na lengo la kumuachia huru mfungwa anayetumikia kifungo gerezani wilayani hapo.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya hakimu mkazi wa wilaya John Kapokolo mwendesha mashtaka wa TAKUKURU mkoani Njombe Bw. Colman Njau amesema kuwa mtuhumiwa anatuhumiwa kwa makosa mawili ambayo aliyafanya mwezi Julai mwaka huu eneo la Ivalalila wilayani hapo ambapo kosa la kwanza ni kushawishi kupewa rushwa ya laki mbili na elfu hamsini kutoka kwa Felix Kivengi Sanga ili kuweza  kumuachia huru Godfrey Mahenge ambaye bado anaendelea kutumikia kifungo kwa sasa.

Kosa la pili kupokea rushwa kiasi cha laki mmoja kutoka Felix  Mahenge ili kumwachia huru mfungwa huyo kinyume cha sheria TAKUKURU sura ya 15 kwenye mabano mmoja A ya mwaka 2007.

Hata hivyo mshitakiwa Juma Swedi alipoulizwa mahakamani hapo alikana kuhusika na tukio hilo na mheshimiwa hakimu Kapokolo ameiharisha kesi hiyo hadi Desemba 13 mwaka huu na mshitakiwa yupo nje kwa dhamana na upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea.
 
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa