KERO YA MAJI SHULE YA MSINGI NDULAMO WILAYANI MAKETE YAMALIZWA

Na Edwin Moshi, Makete
 
Kero ya muda mrefu ya ukosefu wa maji katika shule ya msingi Ndulamo wilaya ya Makete mkoani Njombe hatimaye imetatuliwa baada ya idara ya maji wilayani hapo kuamua kutilia mkazo suala hilo
 
Akizungumza na mtandao huu ofisini kwake mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw. Bosco Godigodi Malangalila (pichani) amesema maji yanapatikana kwa wingi shuleni hapo baada ya kuyakosa kwa kipindi kirefu hali iliyokuwa inaleta picha mbaya shuleni hapo.
 
Amesema tatizo hili limeondoka shuleni hapo baada ya idara ya maji kupeleka mabomba na kuyafunga kufidia yale ya awali yaliyokuwa yakivujisha maji ilihali yalikuwa mapya hali iliyosababisha kijiji cha Ndulamo kukosa maji ikiwemo na shule hiyo.Mwalimu Godigodi amesema awali walifanya maandamano hadi kwenye ofisi za serikali ya kijiji kushinikiza tatizo hilo la maji kuondolewa shuleni hapo na waliohusika na uzembe uliosababisha maji yasifike shuleni hapo wawajibishwe
 
“Hivi sasa ndugu mwandishi kuna uafadhali mkubwa kwani maji yapo, hata waalimu wanaoishi shuleni hapa wanauwezo wa kulima hata kabustani ka mbogamboga” alisema Mwalimu mkuu huyo.Mwanafunzi aliyejitambulisha kwa jina la Alexander Marko amesema kutokana na maji kutoka shuleni hapo yanawasaidia kunywa maji na kunawa mikono ukizingatia msimu huu ni wa kiangazi
 
Amesema hivi sasa ile kero ya kwenda kutafuta maji wakati wa masomo na wakati mwingine wanafunzi kuja na maji ya kunywa shuleni kwa sasa haipo kwa kuwa yapo maji ya kutosha.Naye mwanafunzi mwingine Timotheo Ibrahim amesema hivi sasa usafi wa vyoo ni mzuri tofauti na awali lakini pia hata mazingira ya shule yamekuwa masafi kwa kuwa maji hayo hutumia kupigia deki madarasani na vyooni
 
Katika hatua nyingine mwalimu Godogodi amesema ujenzi wa nyumba ya mwalimu uliokuwa ukamilike mwezi huu, hivi sasa unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba mwaka huu kwa kuwa ujenzi huo utaendelea kwa kasi baada ya maji kufika shuleni hapo
 
Amesema ujenzi huo ulisuasua kutokana na kukosekana kwa maji shuleni hapo lakini kwa kuwa kila kitu cha ujenzi hivi sasa kipo ujenzi huo utakamilika mwezi Septemba

Njombe wavalia njuga usafi wa mazingira



ASASI zizizokuwa za kiserikali zimeendelea kujadili utekelezaji wa  mpango wa kuboresha usafi wa mazingira shuleni,  kupitia mradi wa  TAWASANET  wa uboreshaji wa huduma za  maji na usafi wa mazingira shuleni ambao umefadhiriwa na shirika la kuhudumia watoto Duniani UNICEF.

Mpango huo ambao umeanza mapema mwaka huu, umehusisha wadau kutoka asasi za kiraia ambazo zimeshiriki katika kujadilli suala la usafi shuleni mradi ambao umetolewa na SWASH  asasi inayojihusisha na huduma za afya ya maji na usafi wa mazingira,  ambapo awali mafunzo yalitolewa kwa wadau wa mazingira ili kuwajengea uwezo wa kusimamia usafi wa mazingira,Mkoani Njombe na kuanza kwa shule  mbili za majaribio .

UNICEF kwa kushirikianana SNV shirika la Kiholanzi, wameelekeza jitihada za usafi wa mazingira shuleni katika Wilaya ya Njombe na kufanikisha kuzifikia shule tano ambazo zimeanza kwa majaribio.

Katika jitihada za kuhakikisha usafi wa mazingira shuleni unazingatiwa, baada ya kufanya majaribio la utoaji elimu kwa wadau hao, mabadiliko yameonesha kuanza kuchomoza katika shule ambazo mpango umeanza kutekelezwa, Dkt Rosmary Daniel ni mratibu wa TAWASANET anaeleza kuhusu mradi huo.
Insert Dkt. Rosemary Daniel mratibu TAWASANET. 

Waziri mkuu Pinda asema eneo la Ludewa litapata miradi muhimu ya kiuchumi.

Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, amesema kuwa wawekezaji wapo hatua za mwisho kuanzisha uzalishaji wa chuma na umeme katika eneo la Ludewa.

Kufuatia kuanza kwa miradi hiyo, Pinda aliagiza Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kuandaa wananchi kwa kutoa elimu kuhusu fursa, zilizopo za kazi katika eneo hilo.

Alisema kazi ya Serikali hivi sasa ni kuhakikisha inajenga barabara kupitisha mitambo inayotakiwa kwenye miradi hiyo na kwamba, tayari Sh7 bilioni za awali zimetengwa kwa upanuzi wa barabara
Kuhusu ujenzi wa barabara ya lami kutoka Itoni, Ludewa hadi Manda,

Waziri Pinda alisema tayari Serikali imetenga fedha za upembuzi yakinifu, hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi kuhusu miundo mbinu.

Akizungumzia sekta ya kilimo, Pinda alisema jembe la mkono haliwezi kumaliza matatizo ya mkulima, na kinachotakiwa ni kuangalia uwezekano wa kuwakopesha wakulima matrekta ya bei nafuu.
Serikali pia katika eneo hilo inapania kuanza kuzalisha megawati za umeme Megawati 600.

Pinda ahimiza kilimo cha mazao ya biashara Njombe

WANANCHI wilayani makete Mkoani Njombe, wametakiwa kuboresha mazao ya biashara ambayo yanastawi katika Wilaya hiyo,ili kukuza uchumi kupitia rasiliamali walizo nazo.

Akizungumza na wananchi waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda ameagiza wananchi kuimarisha mazao ambayo ni muhimili wa uchumi wao.

Amewaondoa shaka wakulima hao kuhusu wanunuzi wa zao la Pareto na kuongeza kuwa kilimo cha matunda, Pareto vinapaswa kuboreshwa ili kuutumia vema fursa ya kilimo katika uzalishaji mazao yanakubalika kimataifa.


Kambarage Sanga ni mkulima wa matunda  anayemiliki ekari 3000 za matunda, katika kijiji cha Iniho, akamweleza waziri mkuu jinsi anavyoendesha kilimo cha matunda aina mbalimbali.

Baada ya kutembelea bustani ya miche ya matunda na kujionea shughuli za uzalishaji zianazofanywa na wanakikundi wa kilimo cha matunda KIWAMAI ameahidi kuwapa mashine ya kukamilia juisi ya matunda yenye thmanai ya sh. milioni 5.2.

Afisa kilimo wa wilaya hiyo, akisoma tarifa ya kilimo cha matunda mradi ambao unahudumiwa na halmashauri hiyo, huku wanakikundi wa KIWAMAI wakaeleza changamoto ambayo ni kikwazo cha malengo waliyokusudia

Waziri Mkuu awaonya viongozi Wanging’ombe


WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameipa Wilaya mpya ya Wanging’ombe mkoani Njombe hadi mwisho wa mwezi huu kuhakikisha wanafunzi zaidi ya 800, waliofaulu kuingia sekondari lakini hawajafanya hivyo, wawe shuleni.
Alikuwa akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Ilemela katika siku ya kwanza ya ziara ya wiki mbili katika Mikoa ya Njombe na Ruvuma.

Ni dhambi kubwa kuwaacha wanafunzi hao wawe nje ya shule kwa kuwa wamefaulu na kwamba wenzao wengi wanaendelea na masomo na baadhi yao wanaweza kuwa viongozi wa kesho, alisema.

“Wasakeni hawa popote walipo na mhakikishe wanakuwa shuleni badala ya kuzurura mitaani. Nakuagiza DC (Mkuu wa Wilaya Esterina Kilasi) na RC (Mkuu wa Mkoa Assery Msangi) mlisimamie jambo hili na wanafunzi hao wawe shuleni ifikapo mwisho wa mwezi.

“Mtafanyaje, mtajua wenyewe, lakini wanafunzi hao hawawezi kuachwa tu, lazima wawe shuleni,” alisisitiza.

Asilimia 75 ya watahiniwa wote wa darasa la saba katika wilaya hiyo wamefaulu kuingia Ssekondari katika mtihani wa Taifa wa mwaka 2012, lakini kati ya waliofaulu 864 walikuwa hawajaripoti shuleni.

Kuna vyumba vya kutosha vya madarasa na ziada ya madawati katika wilaya hiyo yenye watu wapatao 160,000, ikiwa ni moja ya wilaya nne za mkoa mpya wa Njombe. Wilaya nyingine ni Njombe, Makete na Ludewa.

Waziri Mkuu pia aliagiza watendaji wakuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe wawe wanaishi na kufanya kazi ndani ya wilaya hiyo badala ya kuishi katika maeneo mengine.


CHANZO GAZETI LA MTANZANIA

MHESHIMIWA PINDA ZIARANI MKOA WA NJOMBE


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (wapili kulia) wakikagua shamba la nanasi la Katibu Mkuu kiongozi Mstaafu, Philemon Luhanjo (kulia) katika kijiji cha Madeke wilayani Makambako wakiwa katika ziara ya Mkoa wa Njombe Julai 10,2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kulia kwakena ) wakikagua shamba la nanasi la Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Philemon Luhanjo (kulia) katika kijiji cha Madeke wilayani Makambako wakiwa katika ziara ya Mkoa wa Njombe Julai 10,2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akivuna nanasi katika shamba la Katibu Mkuu Mstaafu, Philemon Luhanjo (katikati) lililopo katika kijiji cha Madeke wilayani Makambako akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Julai 10,2013. Kulia kwake ni mkewe Tunu.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la msingi la kiwanda cha kusindika mananasi katika kijiji cha Madeke wilayani Makambako akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Julai 10, 2013. Kulia ni Mkewe Tunu. 

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisalimiana na wanawake wa Makambako baada ya kuwasili kwenye mji mdogo huo akiambatana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika ziara ya mkoa wa Njombe Julai 10,2013.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


UJENZI WA TANKI LA MAJI SHULE YA MSINGI MAULU MAKETE UNAKARIBIA KUMALIZIKA


 Kwa mbali utawaona wananchi wakiangalia ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji linalojengwa katika shule ya msingi Maulu kata ya Kipagalo wilayani Makete, kutokana na shule hiyo kukumbwa na uhaba wa maji hasa wakati wa kiangazi hali inayopelekea wanafunzi kupata tabu ya kujisaidia kutokana na vyoo kutumia maji. Ujenzi huo umefadhiliwa na AMREF
 Hapa mafundi wakiwa kazini kama uonavyo
 bado kidogo tuu ujenzi huo utakamilika
Jamaa hasubiri apikiwe, hapa aliamua kuingia jikoni mwenyewe kujipikia ugali kwa ajili yake na mafundi wenzake wanaojenga tanki hilo
Picha zote na  Edwin Moshi
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa