RAIS WA VICOBA TANZANIA AITAKA SERIKALI KUVITAMBUA RASMI VICOBA, AZINDUA TAWI MAKAMBAKO

 Baadhi ya  wanavicoba wa Halmashauri ya mji wa  Makambako mkoani Njombe wakiwa katika maandamano siku yauzinduzi wa  Vicoba.

 Baadhi ya  wanavicoba wa Halmashauri ya mji wa  Makambako mkoani Njombe wakiwa na  mabango katika maandamano siku ya uzinduzi wa  Vicoba.
 Raisi wa Vicoba Tanzania Devotha Likokora (katikati) akiwa na kushoto ni makamu wake Scholastika Kevela wakiongoza maandamano siku ya uzinduzi wa Vicoba Makambako Njombe.


  Raisi wa Vicoba Tanzania Devotha Likokora akionesha mkasi juu kama ishara ya kutaka kukata utepe wa uzinduzi wa Vicoba Makambako Njombe.


 Burudani ya ngoma zikitumbuiza katika uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Green city Makambako mkoani Njombe
  Raisi wa Vicoba Tanzania Devotha Likokora akisakata ngoma siku ya uzinduzi wa Vicoba Makambako Njombe.

 Makamu wa Raisi wa Vicoba Tanzania Scholastika Kevela akipiga chekeche  siku ya uzinduzi wa Vicoba Makambako Njombe.
Na Blogger wa Njombeyetu, Makambako.
WANANCHI waliojiunga na Vicoba wameiomba Serikali kutunga Sera na Sheria zinazohusu fedha ili Taasisi hiyo itambulike na kuendeshwa kitaalamu kwa manufaa ya Watanzania.
Aidha wamesema Serikali inatakiwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wananchi ya kujiunga na Vicoba inayotekeleza Sera ya maisha bora kwa kila Mtanzania ambapo imetakiwa Serikali kuwawezesha kwa kufuata miongozo ya Taasisi za Fedha.
Mwito huo ulitolewa mwishoni mwa Wiki na Wanachama wa Vicoba wa Halmashauri ya Mji wa Makambako wakati wa Uzinduzi wa Vicoba katika Hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Green City Makambako Mkoani Njombe.
Raisi wa Vicoba Tanzania Devota Likokora, alisema mbali na Serikali kutambua uwepo wa Vicoba inatakiwa kutunga Sheria na Sera ili viweze kutambuliwa rasmi katika mifumo ya Fedha kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha, Uwekezaji na Benki kuu.
Likokora alisema Watanzania wengi wa vipato vya chini ndiyo wanaomiliki na wanachama wa Vicoba na kwamba mfumo wake ni kwa kila Mwanachama kumiliki uchumi wake pasipo kukatwa riba kubwa kama taasisi zingine zinavyofanya.
Akizungumza katika uzinduzi huo Likokora alisema tangu aanze harakati za kupigania Vicoba Mwaka 2002 wamefikisha idadi ya Wanachama zaidi ya Laki tano wakiwa katika Vikundi 9000 kwa Nchi nzima ambapo kwa sasa limeanzishwa daftari kwa ajili ya kuwatambua wanachama wote.
Kwa upande wake Makamu wa Raisi wa Vicoba Tanzania Scholastika Kevela Vicoba vipo kwa ajili ya Wananchi wenye vipato vya Chini kutokana na wengi wao kutokuwa na uwezo wa kupewa dhamana ya mikopo katika Mabenki.
Aliongeza kuwa lengo la Vicoba ni kumwezesha kila mwananchi kupata elimu namna ya kumiliki uchumi wake mwenyewe ili waweze kuchangia shughuli za maendeleo ya Taifa pasipo manung’uniko yoyote.
Alisema mara nyingi wananchi wanashindwa kuchangia shughuli za maendeleo kutokana na kutokuwa na vipato vya kutosha hivyo kupitia Vicoba kila mwananchi atakuwa tayari kuchangia kutokana na kuwa na uchumi mzuri.
Katika Uzinduzi huo Jumla ya Vikundi 12 vinavyounda Mji wa Makambako vilizinduliwa ambavyo ni kikundi cha Upendo, Twendepamoja, Ujamaa, Chinga group, Mshikamano, Umoja, Mani, Amka, Ukombozi, Agape, Twitange na Lukelo.
Mratibu wa Vicoba wa Mji wa Makambako Muhimba Payovela alisema Vicoba vilianzishwa rasmi mwaka 2010 ikiwa na wanachama 150 na vikundi 13 na lengo lao ikiwa ni kuwaunganisha nguvu na mawazo ili kuwa na chama cha kuwaletea maendeleo.
Alisema tangu kipindi hicho idadi ya Wanachama imeongezeka na kufikia wanachama 501 wanawake 401 na wanaume 100 wakiwa na fedha zaidi ya Shilingi Milion 10,800,000 ambapo wameweza kuwakopesha wanachama zaidi ya 1500 shilingi Milioni 168,930,000 na Milioni 60 zimetengwa kwa ajili ya Elimu na Afya.
Aliongeza kuwa katika Mkopo huo wamepata faida ya Shilingi Milioni 56,310,000 na Bima ya Shilingi 1,133,300 na kuongeza kuwa vikundi vingi vinakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na elimu ya utunzaji wa fedha licha kufanikiwa kuwa na fedha nyingi.
Aidha  katika uzindizi huo Raisi wa Vicoba alifuatana na makamu wake na timu ya wataalamu mbali mbali kutoka makao makuu ambao ni Mratibu wa michezo na ujasiliamali wa Vicoba Anna Basita, Makundi maalum Subira Msimbazi, Vijana Vicent Herman Sekta ya ukaguuzi Jojina Chai na kitengo cha mafunzo mikoani Aidani Bumburu.

Na blogs za mikoa.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa