Rais Jakaya Kikwete amwapisha Asery Msangi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe

 Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Kapt Asery Msangi kuwa Mkuu wa Mkoa
wa Njombe katika sherehe zilizofanyika leo asubuhi Ikulu jijini Dar es
salaam
Picha Kwa Hisani Ya Father Kidevu Blogu

KIFO CHA DIWANI WA CCM LUDEWA NI PIGO KWA CCM


Madiwani wa Ludewa 
Na Francins Godwin- NjombeDIWANI wa kata ya Mlangali wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Rudolph Chaula (CCM)ambaye pia alikuwa ni meneja wa Chama cha kuweka na kukopa cha Mlangali (SACCOS) ameamua kujinyonga ndani ya ofisi yake ya udiwani akidaiwa kukwepa madeni .


Diwani Chaula alijinyonga usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake Mlangali na kudaiwa kuacha ujumbe wa maandishi wenye utata mkubwa.


Imeelezwa kuwa chanzo cha diwani huyo kujinyonga ni kutokana na kuzidiwa na mzigo wa madeni kutoka katika Chama cha kuweka na kukopa cha Mlangali ( SACCOs) ambako alikuwa ni meneja.


Mmoja kati ya wanachama wa Mlangali Sacos ambaye hakupenda kutajwa jina lake katika vyombo vya habari kwa kuwa si msemaji wa Chama hicho alisema kuwa siku mbili nyuma walifika wakaguzi na kufanya ukaguzi katika Chama hicho cha ushirika na kubaini kuwepo deni kubwa lisilojulikana mkopaji.


" Mheshimiwa diwani wetu ambaye alikuwa ni Mhasibu ( meneja kwa sasa) katika SACCOS hiyo kabla ya wakaguzi hao alikuwa ni mchangamfu kupita kiasi ila baada ya wakaguzi kuja alionekana ni mtu mwenye Msongo mkubwa wa mawazo jambo ambalo liliwafanya wananchi wengi kuingia na Shaka juu ya usalama wa fedha zao" alisema


Kuwa Mlangali SACCOS kilikuwa ni moja Kati ya vyama vya ushirika vyenye nguvu kubwa katika wilaya ya Ludewa ila baada ya Mhasibu wao huo kuingia katika siasa kwa kugombea udiwani mwaka 2010 ndipo Chama kilianza kuyumba zaidi .




Hata hivyo alisema kuwa juzi mchana diwani huyo alionekana mitaani majira ya saa 7 mchana akitafuta kusajili lini yake ya simu ila hakufanikiwa kufanya hivyo akatoweka kusikofahamika.


Hata hivyo alisema kutokana na kutoonekana kutwa nzima usiku ndipo walipomkuta akiwa amejinyonga kwa Kamba katika chumba chake ambacho alikuwa akitumia Kama ofisi.


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangalla amethibitisha kwa njia ya simu kutokea kwa tukio hilo na kuwa taarifa zaidi itatolewa .

JUST IN: DIWANI WA CCM LUDEWA AJINYONGA USIKU HUU


Marehemu Rudolph CHaula a.k.a Kacheche kushoto



Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Ludewa mkoa mpya wa Njombe kimepata pigo kubwa kufuatia diwani wake wa kata ya Mlangali Rudolph Chaula maaarufu kwa jina la Kacheche kujinyonga .


Taarifa ambazo mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com umezipata hivi na kuthibitishwa na katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Eva Degeleki zinadai kuwa diwani huyo amekutwa akiwa kajinyonga katika moja kati ya vyumba vya nyumba yake ambavyo katika enzi ya uhai wake alikuwa akitumia kama ofisi yake ya udiwani.

Katibu huyo wa CCM Ludewa amesema kuwa hadi sasa hana taarifa za chanzo cha kifo chake ila anataarifa ya kujinyonga kwa diwani huyo na kuwa amepokea taarifa hiyo mida ya saa 8.15 usiku huu kujulishwa juu ya kifo hicho.


Imedaiwa kuwa diwani huyo toka mida ya mchana familia yake ilikuwa ikimsaka bila mafanikio baada ya wageni kufika kumuulizia na jitihada za kutafuta huku na kule zilimezao matunda usiku huu baada ya kuwa na wazo la kuvunja chumba hicho na kumkuta diwani huyo akiwa kajinyonga.
Taarifa zaidi inakuja

Kwa hisani ya Francis Godwin mzee wa matukio daima blog

Welcome to Njombe Region Tanzania




Coming Soon
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Njombe Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa